Wawekezaji Afrika kusini wanataka makubaliano kati ya ANC na DA

Wawekezaji Afrika kusini wanataka makubaliano kati ya ANC na DA

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Randi ya Afrika Kusini imeimarika kwa kiasi mapema leo Jumatatu, huku wachambuzi wakisema wanatarajia kwamba mazungumzo ya kisiasa wiki hii, kuunda serikali yatachochea zaidi thamani ya sarafu hiyo.

Hii ni baada ya chama tawala cha African National Congress ANC kushindwa kupata idadi ya viti vya bunge vinavyohitajika katika utawala wake wa miaka 30.

Randi inabadilishana kwa kiwango cha 18.73 dhidi ya dola moja ya Marekani, ikiwa imeimarika kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na ilivyokuwa Ijumaa wiki iliyopita.

Chama cha ANC kilipata asilimia 40.2 ya kura, ikiwa ni matokeo mabaya zaidi kuwahi kurekodiwa na chama hicho, na kitalazimika kufanya mazungumo na vyama vingine ili kuunda serikali.

Wawekezaji wana wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa ANC kuhusisha vyama kama EFF cha Julius Malema au uMkhonto we Sizwe cha rais wa zamani Jacob Zuma, na wangependelea ANC kifanye mazungumzo na Democratic Alliance chenye sera za kibiashara.

PIA SOMA
- Zama za chama cha ANC kutamba Afrika Kusini yafikia tamati
 
Tuko hapa miaka ijayo wananchi wa Afrika Kusini watakipa mamlaka ya uongozi hiki chama cha DA na kuachana na hivi vyama vya kihuni na vya kipigaji vya kiswahili ambavyo vinaleta umaskini kwa nchi na raia kwa ujumla.

Kaburu P.W. Bother aliwahi kusema, "kama unataka kuharibu nchi ni rahisi sana, mpe mtu mweusi atawale." Leo tunaona wenyewe kinachofanyika katika nchi za kiafrika.
 
Polepole nchi inarudi kwa mkabulu. Naanza kuamini huenda ni kweli mtu mweusi hawezi kujitawala
Ni ukweli mchungu, kinachozamisha afrika ni pamoja na ufisadi ulio kubuhu. Huu ni mwiba mchungu.
Bahati mbaya hawa majizi wanadhani huko tuendako wao watakuwa salama. Yaan hata vi NGO vya kusapoti ushoga wameshindwa kuvidhibiti. Basi tukubali kuwa mweusi ni alama ya laana
 
Mulemule, Wasouth Africa wakijitambuwa watawarudisha wazungu kuongoza nchi.
Wa South Africa ni wajinga sana, wana bahati ya kuwa na hiyo fursa ambayo mataifa mengine ya Afrika haina lakini wanashindwa kuitumia, ngoja wafanye kusota.
 
Back
Top Bottom