Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Akina Johari?? Usitegemee miujiza, ni viazi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Suluhisho ni hili walilokuja nalo wanasheria kwenye huu mkataba wa DPW, kwanza wameanzia bungeni ili kupata ulinzi wa kikatiba.Pamoja na hasara kubwa tuliyopata kwenye mikataba ya madini na rasilimali nyingine ikiwemo gesi hali ya kuifilisi Tanzania inayoendelea huko mahakama za kimataifa inatia kinyaa
Kinachoendelea sasa hivi; mwekezaji akigombezwa kidogo tu na serikali anakwenda kufungua kesi nje. Akifungua kesi Tanzania tunaajiri mawakili wa kigeni kututetea wakishirikiana na mawakili wachache wa Tanzania.
Pamoja na kuajiri wageni hao kututetea kesi asilimia kubwa tunashindwa na kutakiwa kulipa fidia. Hakuna mtu anayekubali kesi tunazo shindwa zifahamike kwa watanzania zote ni siri hadi ziwe published huko nje.
1. Kama hatuna wanasheria wazawa wakututea tunaposhtakiwa kwa kukiuka masharti ya mikataba, tumepata wapi wanasheria wakiingia mikataba?
2. Tutaendelea kushtakiwa na kulipa fidia hadi lini?
3. Haiwezekani fedha nyingi zinazotokana na mkataba kama wa bandari zikatumika kulipa madeni tunayodaiwa kwa kuvunja mkataba?
4. Kama ndivyo, ni lini kama Taifa tutaamua kusubiri tuandae watu wakutusaidia kuingia mkataba na pia kutetea mikataba yetu hasa ya rasilimali zetu?
Pia soma: - Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260
Mtu mwizi hajali maslahi ya nchi, anachojali ni yeye na familia yake.Mikataba ya gas aliyetuingiza mkenge ni raisi wa awamu ya 4!
Na ndie anaongoza kwa kutuingiza mikataba mibovu kuliko raisi yoyote!
Sijui hizi pesa wanaenda zako kaburini!