Wawekezaji baada ya kutengeneza faida lukuki wameamua kutufilisi kwa kufungua kesi huko Mahakama za kimataifa. Wanasheria wetu wanafanya nini?

Suluhisho ni hili walilokuja nalo wanasheria kwenye huu mkataba wa DPW, kwanza wameanzia bungeni ili kupata ulinzi wa kikatiba.

Pili wameweka kifungu namba 20 ambacho kinasema iwapo patatokea kutoelewana mbele ya safari tatizo litaanza kutatuliwa kwa kutumia amicable settlement na ikishindikana itaundwa kama ndogo ya IGA negotiation committe ili kutatua tatizo husika.

JPM alitanguliza akili ya kugombana na hawa wawekezaji na kuamua kuvunja mkataba moja kwa moja, hakujali hasara ambayo ilitusubiri mbele ya safari, na ndio hii imefika sasa.

Lipo somo la kujifunza upande wa wanasiasa, kuheshimu mikataba bila ya kutanguliza akili za kuburuza pande zote mbili zinazokubaliana kwenye kuingia makubaliano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…