A
Anonymous
Guest
Kwa niaba ya wananchi wenzangu Wakazi wa Mtaa wa Miswe, Kata ya Mbwawa, Mkoa wa Pwani, naomba kutoa kero inayotusumbua tangu mwaka 2025. Kuna wawekezaji kutoka Nigeria waliofungua kiwanda cha unga katikati ya makazi yetu.
Kero yetu kubwa ni kelele kutoka kwenye mitambo ya kiwanda hicho. Kuna wazee, wagonjwa na watoto wachanga wanaoathirika na kelele hizo. Imefikia hatua ya kushindwa kuwasiliana ana kwa ana na mwanafamilia bila kusogeleana, na wakati mwingine kulazimika kutazama midomo wakati wa kuzungumza.
Tunaomba msaada kwa sababu Serikali ya Mtaa na Kata inatambua changamoto hii, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Tunajiuliza ilikuwaje Halmashauri kuruhusu kiwanda kujengwa katikati ya makazi ya watu. Isitoshe, kiwanda hicho kinaonekana kutokuwa na utambulisho wowote, kwani hakina bango wala jina linaloonekana.
Kiwanda hicho kipo kando ya Barabara ya Bagamoyo, kutoka Mlandizi, Mtaa wa Miswe, Kata ya Mbwawa.