Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Nimesikia muwekezaji mmoja Mkubwa tu ( Vasso Agroventures) kwenye media akilalamikia kutozwa kodi kubwa na zisizo eleweka pamoja na kuingiliwa miradi yake ya uwekezaj na mwaka 2021 amepata hasara ya shs Bilioni 8 huku akiwa ame ajiri wafanyakazi zaidi ya 1000.
Wahusika TRA na Kituo cha uwekezaji wamejitokeza kusema eti aandike barua na kwenda nayo huko ofisini kwao ili wajadiliane na kuona namna ya kumsaidia;
Kwa mwekezaji MZUNGU na kwa changamoto zetu za ndani za ajabu ajabu tunazijua wenyewe naona huo ushauri sio rafiki kabisa kwani nafikiri wangemtembelea kwenye miradi yake kujua changamoto zake na kumuelekeza namna nzuri ya kuwakilisha ili kupata msaada? au hawaruhusiwi kwenda field?
Jamani; Ajira zaidi ya 1000 kwa kipindi hiki ni za kulinda; watu wanateseka sana mitaani bila kazi; na tukumbuke analipa kodi kubwa tu indirect kupitia hiyo mishahara