Wawili wakamatwa na Polisi kwa kuichapa sanamu inayofanana na sura ya Museveni

Wawili wakamatwa na Polisi kwa kuichapa sanamu inayofanana na sura ya Museveni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Polisi wa Uganda wamemkamata Mwanaume mmoja Barabara ya Kampala baada ya kukutwa akiichapa viboko sanamu akidai sanamu hiyo inafanana na Mtu ambae amehusika kuvuruga Uchaguzi wa Uganda na anastahili adhabu kwa makosa aliyoyafanya.

1613393287785.png


1613393310796.png


1613393353198.png


Polisi nchini Uganda Jumatatu waliwakamata wanaume wawili ambao walichapa viboko picha ya Rais Yoweri Museveni kwenye barabara yenye shughuli nyingi katika mji mkuu, Kampala.

Wawili hao, Luta Ferdinand Male na Nsereko Asharf, walijitambulisha kwa polisi kuwa wao ni wanaharakati. Walimshtaki rais kwa udanganyifu katika uchaguzi wa tarehe 14 mwezi Januari, ingawa Bwana Museveni hapo awali alikanusha madai hayo.

Msemaji wa polisi jijini Kampala Patrick Onyango amethibitisha kukamatwa kwa watu hao. Watakabiliwa na mashtaka ya kusababisha kero kwa Umma.

Gazeti la Daily Monitor lilichapisha picha za kukamatwa kwa watu hao kwenye mtandao wa Twitter:

Uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani mkubwa nchini Uganda ulimfanya Rais Museveni kutawala kwa muhula mwingine Mpinzani wake wa karibu, mwanamuziki aliyegeuka-mwanasiasa Bobi Wine, anapinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

Wiki iliyopita, bunge la Umoja wa Ulaya lilitaka vikwazo dhidi ya watu binafsi na mashirika yaliyohusika na ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi - ambayo walisema hayakuwa ya kidemokrasia na hayakuwa na uwazi
 
Polisi wa Uganda wamemkamata Mwanaume mmoja Barabara ya Kampala baada ya kukutwa akiichapa viboko sanamu akidai sanamu hiyo inafanana na Mtu ambae amehusika kuvuruga Uchaguzi wa Uganda na anastahili adhabu kwa makosa aliyoyafanya. #MillardAyoUPDATES

Picha na daily monitor
EuRBfQ_WYAEnkJm.jpg

EuRBfQ_XUAMRiE8.jpg

EuRBfQ_WgAEc1cR.jpg
 
Viongozi wa Afrika ni hovyo kabisa, sio masanamu yao tu yanayostahili viboko, hata makaburi yao pia.
Unaposea Afrika unakosea mkuu ,kwa hayo mbn URUSI yanatokea Belarusi n.k we sema viongozi kama hao. sio Wa Afrika yote
 
Inawezekana sheria za Uganda kuna kosa la kuchapa sanamu.
 
Back
Top Bottom