Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Saudi Arabia imechapisha upya vitabu vyote vya shule za nchi hiyo na kuondoa vipengele vilivyokuwa vikiwataja kwa ubaya Wayahudi pamoja na Wakristo. Baadhi ya vipengele hivyo ni kama vile utabiri wa kuzuka vita hapo baadae ambapo waislamu watawapiga vibaya mayahudi na kuwashinda. Kipengele kingine ni kuwa mayahudi ni maadui wa dini ya uislamu.
Vitabu vya awali pia vinawataja Wayahudi na Wakristo kuwa ni makafiri na kwamba matendo yao mema yote yataishia hapa duniani na kwamba huko akhera wataingia moto wa jahanamu milele.
Mbali na hayo ambayo ni mahasusi kwa mayahudi na wakristo, vitabu hivyo vipya vimekwenda mbali kwa kufuta adhabu ya mashoga na wachawi kuwa ni kuuliwa.
Mafanikio hayo yamekuja kufuatia juhudi za muda mrefu na za kichinichini za taasisi ya kiyahudi iitwayo IMPACT SE ambayo ni maalumu kwa kufuatilia mitaala ya nchi mbali mbali duniani hasa za kiislamu kuhakikisha kuwa maandishi yanayowataja vibaya mayahudi yanafutwa.
Pamoja na kwamba juhudi hizo ni za muda mrefu lakini zimetajwa kupata nguvu zaidi wakati wa uraisi wa Donald Trump wa Marekani na hasa baada ya kuchukua madaraka kwa mtoto wa mfalme Mohammed bin Suleiman wa Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa taasisi hiyo Marcus Sheff , mafanikio hayo si makubwa sana lakini kwa ujumla yanakwenda kwenye mstari na malengo yao.
Katika mkakati wa kupima mafanikio ya kazi zao taasisi hiyo inatambua kuwa takriban thuluthi mbili ya idadi ya wananchi wa Saudi Arabia wana umri ulio chini ya miaka 30 na kwamba bado viongozi wengi wa juu wa nchi hiyo na wanazuoni wa nchi hiyo wamekuwa ni kikwazo kutokana na misimamo yao ya kulinda dini na tamaduni zao.
Vitabu vinavyochapwa na wizara ya elimu vya nchi hiyo vinatumika na mashule takriban 30,000 yaliyo ndani ya nchi hiyo na nje ya nchi.