Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Mkuu ukiwaambia vijana wa sasa kwamba pale ulipo ubalozi wa USA ndio kulikuwa na Drive-in cinema hawatakuelewa....enzi hizo kama huna hela unakaa pale nje unacheki Bruce lee na akina Fred Williamson bila sauti. Tulikuwa tunaita kiingilio mbu!
Hahahaha, kula sana mihogo huku mnatazama movie kibububu

Avalon ndio imekua Ofc za Tunakopesha eeh , na Empire mmevunja kabisa, odeon mmempa Mo ,dah kitambo

Ila yote Tisa ile story ya MTU kageuka chatu ,ilibamba sana
 
Hahahaha, kula sana mihogo huku mnatazama movie kibububu

Avalon ndio imekua Ofc za Tunakopesha eeh , na Empire mmevunja kabisa, odeon mmempa Mo ,dah kitambo

Ila yote Tisa ile story ya MTU kageuka chatu ,ilibamba sana
Hayo masinema ukipita hata huwezi kudhani yalikuwa yanabamba! Nilisahau Starlight Cinema
 
Hahahaha, ndio ikaibuka story mabaharia wamezamia meli bandarini wakashuka coco beach wakijua wamefika ughaibuni
Hio kweli mkuu, meli imeondoka ikaenda kule mbele ikaweka nanga kama wiki hivi,jamaa wanaibuka chimbo usiku kucheki mataa ya Oysterbay wakajua washafika kwa Madiba wakajitosa kwenye maji wameogolea kufika ufukweni wanakutana na kibao 'USIOGELEE HAPA' hapo ndio wakajua wameibukia coco beach!
 
Hahahaha. Work done = Zero hapo ,nilikua nacheka sana kipindi kile
 
Yolanda.sabuni kodrai.kampuni ya mafuta Bp na caltex.Jumba la sinema shani.sapna.avalon.baiskeli ya swala.avon.phoenix.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vituo vya mafuta vingi na vilivyo maarufu vilikuwa vya kampuni ya Shell au Shell na BP.
Ndicho chanzo cha hadi leo kila kituo cha mafuta kuitwa Shell hata kama kina jina mfano: Oil Com, Ngara Oil nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu ilikuwa inaitwa Kinondoni stereo (KIBISA) walikuwa wanafanya maonesho kila weekend nafkiri, walikuwa wakipita barabarani kwa ajili ya PA walikuwa wanapita huku jamaa kabeba joka kubwa tu ila haling'ati ndio ikawa sababu mpaka leo ukiwa na dushe lililodhoofu unaitwa joka la kibisa...!
 
Kati yenu wahenga hakuna mtu mwenye akili akili kidogo atusaidie kupata chanjo ya corona ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…