Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Pale Posta ya zamani kwenye stand ya Temeke kipindi hicho, kulikuwa na jamaa wanachoma mihogo kwa mafuta ya mawese. Ukila mipande mitatu na maji ya kwenye ndoo siku inapita vizuri kabisa.
Hahahaha, kula sana mihogo huku mnatazama movie kibububu

Avalon ndio imekua Ofc za Tunakopesha eeh , na Empire mmevunja kabisa, odeon mmempa Mo ,dah kitambo

Ila yote Tisa ile story ya MTU kageuka chatu ,ilibamba sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji4][emoji4][emoji4]
_20191231_163147.JPG
 
Hio kweli mkuu, meli imeondoka ikaenda kule mbele ikaweka nanga kama wiki hivi,jamaa wanaibuka chimbo usiku kucheki mataa ya Oysterbay wakajua washafika kwa Madiba wakajitosa kwenye maji wameogolea kufika ufukweni wanakutana na kibao 'USIOGELEE HAPA' hapo ndio wakajua wameibukia coco beach!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu ilikuwa inaitwa Kinondoni stereo (KIBISA) walikuwa wanafanya maonesho kila weekend nafkiri, walikuwa wakipita barabarani kwa ajili ya PA walikuwa wanapita huku jamaa kabeba joka kubwa tu ila haling'ati ndio ikawa sababu mpaka leo ukiwa na dushe lililodhoofu unaitwa joka la kibisa...!
Umenikumbusha Mimi na mdogo wangu tulivyokuwa tunagombea hela mezani tukanunue vitu badala ya dada wa kazi na lazima atatuambia kaagizwa nini hapo manunuzi ni nusu ya pesa tunakusanya tupate Shs 20 ya Silent Inn siku ya Jumamosi utamaduni muungano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom