Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Habari wanajamvi,

Wiki hzi tatu au mwezi huu tumekuwa na mijadala mingi hasa inayohusu uteuzi na teuzi mbalimbali.

Kinacholeta mjadala kingine ni katika masuala ya Muungano, Nacho nauliza kama ifuatavyo:

1. Je, inaruhusiwa kwa Mzanzibari kuongoza Wizara/taasisi ambayo haipo katika masuala ya Muungano, mfano Afya?

2. Kama ni sahihi, je mbona Watanganyika hatupewi nafasi za kuongoza wizara/taasisi zisizo za muungano kule Zanzibar?

3. Kama si sahihi, je ni kwa nini kinafanywa na nini kifanyike?
 
Zanzibar ipo lkn Tanganyika ilikufa siku ya muungano. Kwahiyo kuna watanzania na wazanzibari lkn hakuna watanganyika..

Hivyo ni ruksa kwa mzanzibari kushika nafasi yoyote ile.

Tatizo muungano wetu umekaa kigoloko Sana. Haiwezekani nchi 2 zikaungana halafu kukaendelea kuwa na nchi 2.
 
Hii ni serikali ya muungano, sio serikali ya Tanganyika, hivyo basi yeyote kutoka pande yeyote ya muungano ,anaweza kuwa waziri
Kasome vizuri mambo ambayo ni ya muungano na mambo yasiyo ya muungano.

Hivi unajua Rais wa Muungano kuna mambo ambayo hana mamlaka nayo upande wa Znz?
 
Zanzibar ipo lkn Tanganyika ilikufa siku ya muungano. Kwahiyo kuna watanzania na wazanzibari lkn hakuna watanganyika..

Kwahiyo ni ruksa kwa mzanzibari kushika nafasi yoyote ile.

Tatizo muungano wetu umekaa kigoloko Sana. Haiwezekani nchi 2 zikaungana halafu kukaendelea kuwa na nchi 2.
Nndo maana siye wengine tunataka serikali tatu ili tufufuwe Tanganyika yetu ilokufa kifo cha ghafla miaka ile ya 60

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Zanzibar ipo lkn Tanganyika ilikufa siku ya muungano. Kwahiyo kuna watanzania na wazanzibari lkn hakuna watanganyika..

Kwahiyo ni ruksa kwa mzanzibari kushika nafasi yoyote ile.

Tatizo muungano wetu umekaa kigoloko Sana. Haiwezekani nchi 2 zikaungana halafu kukaendelea kuwa na nchi 2.
siyo sahihi kwa mzanzibari kuongoza taasisi ambazo si za kimuungano. shida sisi watz tunaburuzwa kutokana na hili likatiba feki. kama hatutadai kwa nguvu zetu zote kupata katiba nzuri basi tutaendelea kuburuzwa na wazanzibari mpaka kitapokuja kizazi kingine ambacho kitajitambua lkn kwa katiba hii hatuwezi kutoboa.
 
Back
Top Bottom