Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Ni sahihi kabisa kwa Mzanzibari kuongoza taasisi ambayo sio ya muungano kwasababu kila Mzanzibar ni Mtanzania, hivyo ana haki zote za Watanzania wengine wote. Ila sio kila Mtanzania ni Mzanzibari, hivyo wenye haki kuongoza taasisi za Zanzibar ni Wazanzibari pekee.
P
Aisee,
Mkuu hivi ndo ilivyokaa ama umeamua wewe?
Mambo ambayo siyo ya Muungano ni mambo yanayohusu Tanganyika japo yatakuwa chini ya Rais wa muungano na hayahusu Zanzibar. Inakuwaje Mzanzibar ni Mtanzania lakini Manganyika si Mtanzania wakat Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
 
Zanzibar ipo lkn Tanganyika ilikufa siku ya muungano. Kwahiyo kuna watanzania na wazanzibari lkn hakuna watanganyika..

Kwahiyo ni ruksa kwa mzanzibari kushika nafasi yoyote ile.

Tatizo muungano wetu umekaa kigoloko Sana. Haiwezekani nchi 2 zikaungana halafu kukaendelea kuwa na nchi 2.
Mkuu kwani hujui kuwa 1+1=2
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo zaidi ni uwezo wao kushinda uzanzibari.

Huyo naibu wizara ya afya anaedili na mambo ya jamii inabidi aangalie activities za hizi asasi za jamii.

Swala la ulinzi wa watoto ni sensitive na hiyo ni vita ya serikali kwenye preventive measures na inataka ushiriki wa polisi, ustawi wa jamii na kujua unawapeleka wapi wahanga wa abuse kabla ujaingilia kati.

Sasa hizi taasisi zinazoanzisha vilabu na kuita kuzungumza na jamii waelezee changamoto za abuse zao; halafu baada ya mtu kumchongea abuser wake anarudi kuishi kwenye nyumba ile ile bila ya polisi involvement au ustawi wa jamii kumchukua kama ni mtoto.

Mjomba hizo taasisi wanawatengenezea hao watu mazingira magumu ya kuishi kuliko waliyokuwa nayo awali.

Vitu vingine sio kukurupuka na kudandia kama huna elimu navyo. Waziri inabidi aangalie hizi taasisi zinaweza kuwa na nia njema, ila intervention za social services ni technical sio mambo ya kukurupuka bila ya kujipanga.
 
Ni sahihi kabisa kwa Mzanzibari kuongoza taasisi ambayo sio ya muungano kwasababu kila Mzanzibar ni Mtanzania, hivyo ana haki zote za Watanzania wengine wote. Ila sio kila Mtanzania ni Mzanzibari, hivyo wenye haki kuongoza taasisi za Zanzibar ni Wazanzibari pekee.
P
Makubwa, mkuu maana nyingine wazanzibar wamenyonga Watanganyika , wao ndo wanafaidi Sana muungano kuliko Watanganyika , alafu wanapenda kulalamika , ili kutupumbaza Watanganyika
 
Umeuliza swali la msingi. Juzi hapa alipoteuliwa mzanzibari kuwa mkuu wa wilaya Iringa nilijiuliza swali kama hilo.

Katiba imeorodhesha mambo ya muungano 22. Tamisemi ambayo ndiyo wizara inayohusika na wakuu wa wilaya haimo kwenye orodha hiyo. Hata hivyo, namba 9 kwenye mambo hayo 22 ni utumishi katika serikali ys jamhuri ya muungano. Hapa ndipo mkanganyiko unaanzia.

Nipo kwenye mashauriano na wanasheria kabla ya kufungua shauri mahakamani kuomba tafsiri sahihi kisheria juu ya hili.

Kwa muono wangu, watumishi lengwa ambao ni kutoka Zanzibar wangekuwa exclusively kwenye mambo yaliyo kwenye muungano. Si hii ya kuletewa magavana kama sie ni koloni.

Ni jambo linalohitaji tafsiri ya mahakama tu.
Mkuu Gagi, hili liko straight forward wala halihitaji tafsiri yoyote ya kisheria. Muungano wetu ni muungano very unique. Kwa upande mmoja, kitaifa na kimataifa, muungano wetu ni union, hivyo Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye rais mmoja, rais wa JMT, uraia mmoja tuu, uraia wa JMT, na raia wote wa JMT wana haki sawa. Lakini ndani ya muungano, muungano wetu ni federation, wenye nchi mbili, marais wawili na uraia wa aina mbili. Raia wa JMT na Ukaazi wa Zanzibar. Wazanzibari wote ni Watanzania na haki zote za uraia, ikiwemo kuajiriwa kuteuliwa kuongoza taasisi yoyote. Ila kwa upande wa Zanzibar, wenye haki ya kuajiriwa ni Wazanzibari wakaazi pekee.
P
 
@Pascal Mayalla sababu ni kujipendekeza tu, mtu kujipendekeza uwe na faida hata iwe ni yakijinga mfano tunazinyima family zetu, tunaenda kuhonga vimada hiyo ni faida ingawa ni yakijinga lakini hii yakujipendekeza kwetu kwa wazanzibari, hakuna tunachofaidika na tunaishi kuhonga tu
Hatujipendekezi bali muungano ni kama ndoa, japo baba ndio kichwa cha nyumba, mke wako ndiye mtawala wa jikoni, na chumbani, japo mahari umelipia mwenyewe, na kuoa, umeoa wewe, lakini unapotaka zile huduma, lazima uombe, na ukubaliwe atakapojisikia yeye, na unaweza kunyimwa na magoti ukapiga.

Zanzibar ni sehemu ya JMT yenye haki zote za uraia wa JMT.
P
 
Aisee,
Mkuu hivi ndo ilivyokaa ama umeamua wewe?
Mambo ambayo siyo ya Muungano ni mambo yanayohusu Tanganyika japo yatakuwa chini ya Rais wa muungano na hayahusu Zanzibar. Inakuwaje Mzanzibar ni Mtanzania lakini Manganyika si Mtanzania wakat Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za uraia wa Tanzania kama Mtanzania mwingine yeyote, ila kwa upande wa Zanzibar, haki hiyo ni kwa Wazanzibari wakaazi pekee.
P
 
Waliapa kwa Vitabu vya Dini katiba ya Muungano kwa kuifuata na kuitekeleza so kama wanaivunja hukumu yao ipo ni vizuri kuwakumbusha kama ni wacha Mungu au Wanaomcha Maulana
 
Hutajipendekezi bali muungano ni kama ndoa, japo baba ndio kichwa cha nyumba, mke wako ndiye mtawala wa jikoni, na chumbani, japo mahari umelipia mwenyewe, na kuoa, umeoa wewe, lakini unapotaka zile huduma, lazima uombe, na ukubaliwe atakapojisikia yeye, na unaweza kunyimwa na magoti ukapiga.

Zanzibar ni sehemu ya JMT yenye haki zote za uraia wa JMT.
P
Wewe kuna thread ya Mtu kasema Raisi afuate Sheria ukasema unamuunga mkono and then unaongea nini hapa ebo!
 
Kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za uraia wa Tanzania kama Mtanzania mwingine yeyote, ila kwa upande wa Zanzibar, haki hiyo ni kwa Wazanzibari wakaazi pekee.
P
Nimejikuta nikicheka Kama kichaa, Yani kwa lugha nyepesi TANGANYIKA ni koloni la Zanzibar ndani ya Muungano , wao kila pembe ya nchi Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ruksa, ila Mtanganyika Zanzibar tumewekewa vitanzi , unaingia Zanzibar Kama vile unaenda USA,

Zanzibar tupeni Tanganyika yetu, vinginevyo twende sawa kwenye Muungano,
 
Umeuliza swali la msingi. Juzi hapa alipoteuliwa mzanzibari kuwa mkuu wa wilaya Iringa nilijiuliza swali kama hilo.

Katiba imeorodhesha mambo ya muungano 22. Tamisemi ambayo ndiyo wizara inayohusika na wakuu wa wilaya haimo kwenye orodha hiyo. Hata hivyo, namba 9 kwenye mambo hayo 22 ni utumishi katika serikali ys jamhuri ya muungano. Hapa ndipo mkanganyiko unaanzia.

Nipo kwenye mashauriano na wanasheria kabla ya kufungua shauri mahakamani kuomba tafsiri sahihi kisheria juu ya hili.

Kwa muono wangu, watumishi lengwa ambao ni kutoka Zanzibar wangekuwa exclusively kwenye mambo yaliyo kwenye muungano. Si hii ya kuletewa magavana kama sie ni koloni.

Ni jambo linalohitaji tafsiri ya mahakama tu.

..Rais Samia Suluhu ndiye waziri wa Tamisemi.

..Je, suluhisho ni kuundwa kwa serikali ya Tanganyika?
 
Mkuu Gagi, hili liko straight forward wala halihitaji tafsiri yoyote ya kisheria. Muungano wetu ni muungano very unique. Kwa upande mmoja, kitaifa na kimataifa, muungano wetu ni union, hivyo Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye rais mmoja, rais wa JMT, uraia mmoja tuu, uraia wa JMT, na raia wote wa JMT wana haki sawa. Lakini ndani ya muungano, muungano wetu ni federation, wenye nchi mbili, marais wawili na uraia wa aina mbili. Raia wa JMT na Ukaazi wa Zanzibar. Wazanzibari wote ni Watanzania na haki zote za uraia, ikiwemo kuajiriwa kuteuliwa kuongoza taasisi yoyote. Ila kwa upande wa Zanzibar, wenye haki ya kuajiriwa ni Wazanzibari wakaazi pekee.
P
Nini mantiki ya kuweka kwenye katiba yale mambo 22 ya muungano?!
 
Back
Top Bottom