Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Ngoja,

Nchi ina serikali 2.
Moja ya Muungano, moja ya Zanzibar.

Sasa mambo ya kiserikali na kiutawala yasiyohusu muungano na yasiyo ya zanzibar, ni ya serikali ipi au uongozi upi?
 
Habari wanajamvi,

Wiki hzi tatu au mwezi huu tumekuwa na mijadala mingi hasa inayohusu uteuzi na teuzi mbalimbali.

Kinacholeta mjadala kingine ni katika masuala ya Muungano, Nacho nauliza kama ifuatavyo:

1. Je, inaruhusiwa kwa Mzanzibari kuongoza Wizara/taasisi ambayo haipo katika masuala ya Muungano, mfano Afya?

2. Kama ni sahihi, je mbona Watanganyika hatupewi nafasi za kuongoza wizara/taasisi zisizo za muungano kule Zanzibar?

3.Kama si sahihi, je ni kwa nini kinafanywa na nini kifanyike?

Katiba mpya, narudia tena katiba mpya.

Zanzibar kuna wizara ya fedha. Masauni anakuwaje tena huku kama waziri wa fedha?

Iko fyongo kwa wizara iliyoko Zanzibar kuwa na waziri au waajiriwa katika wizara ya kufanana huku.

Jipu hili laelekea kubaya.
 
Aisee,
Mkuu hivi ndo ilivyokaa ama umeamua wewe?
Mambo ambayo siyo ya Muungano ni mambo yanayohusu Tanganyika japo yatakuwa chini ya Rais wa muungano na hayahusu Zanzibar. Inakuwaje Mzanzibar ni Mtanzania lakini Manganyika si Mtanzania wakat Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Usiwe mgumu kuelewa mkuu.

Kuanzia April 27 1964 hakujawahi kuzaliwa Mtanganyika.
 
Nimejikuta nikicheka Kama kichaa, Yani kwa lugha nyepesi TANGANYIKA ni koloni la Zanzibar ndani ya Muungano , wao kila pembe ya nchi Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ruksa, ila Mtanganyika Zanzibar tumewekewa vitanzi , unaingia Zanzibar Kama vile unaenda USA,

Zanzibar tupeni Tanganyika yetu, vinginevyo twende sawa kwenye Muungano,
na baya zaidi wana sheria kandamizi ambayo inakinzana na tamaduni za watanganyika walio wengi, mfano watanganyika wanawake wanatamaduni ya kuvaa nguzo fupi' Zanzibar wakikutwa wanapigwa bakora, sisi watanganyika nikawaida yetu mwezi wa ramadhani kula hadharani na kunywa pombe, zanzibar ukikutwa unafungwa na kupigwa.
 
na baya zaidi wana sheria kandamizi ambayo inakinzana na tamaduni za watanganyika walio wengi, mfano watanganyika wanawake wanatamaduni ya kuvaa nguzo fupi' Zanzibar wakikutwa wanapigwa bakora, sisi watanganyika nikawaida yetu mwezi wa ramadhani kula hadharani na kunywa pombe, zanzibar ukikutwa unafungwa na kupigwa.
Nakataa.

Watanganyika hawana tabia hizo za kwenda uchi
 
ila na sisi tumewashika hao wazenji kwenye jeshi na polisi [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Hakuna Jeshi la Zanzibar sio?..kuna kambi moja hapo dsm kuna wapemba na waunguja tupu..huko zenji kuna kambi ambazo watanganyika ndo wengi?
 
Katiba ina mikanganyiko mingi. Nipo kwenye mashauriano na wanasheria tukianzia na hili la DC Iringa.

Wakiona kuna mashiko nitasonga mahakamani kuomba tafsiri sahihi.

..all the best.

..vyovyote itakavyokuwa tunaomba utupe mrejesho wa suala hili.
 
Kwa mantiki hii serikali inabaki kuwa ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na zanzibar inaenda kugawanywa kuwa miongoni mwa mikoa ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, nashangaa miaka yote tulikuwa tunazunguka......na leo ndo tunafika hapa.
 
Back
Top Bottom