Serikali tatu ni mzigo ,kutaongezea gharama bure kwa ajili ya faida ya wachache, hao wote watajipangia kujengewa mihekalu ya kufa mtu, watajipangia mibenzi, kifupi muungano usiwepo kila mtu achukue 50 zake. Ukisema serikali moja jamaa zetu wabishi watasema watamezwa , wao wanaona kama bara ndio tunawahitaji zaidi kuliko wao wanavyotuhitaji. Pia mimi naona zile sababu za kuwepo muungano kwa wakti huu hazina mshiko, mambo ya vita baridi kati ya nchi za Magharibi na Mashariki hayapo, hatuihitaji Zanzibar kwa ajili ya usalama wa bara!