Wazanzibar Wamshangaa Warioba kwa kupendekeza serikali tatu!

Wazanzibar Wamshangaa Warioba kwa kupendekeza serikali tatu!

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Wazanzibar wamehoji na kumshangaa warioba wadai ameyatoa wapi maoni ya serikali tatu mpaka awe na ujasiri wa kuyaweka kwenye rasimu ya katiba?

source: gazeti RAIA mwema.

DUUUH wazanzibar sasa hamna shukrani..
 
Unaposema wazanzibari unamaanisha nini? Yaani maoni ya mtu mmoja unayaunganisha kwa watu wote. Umepita shule kweli wewe? Au ndiye walewale waliyoifanya serikali iunde tume kuchunguza matokeo?
 
Wazanzibar wamehoji na kumshangaa warioba wadai ameyatoa wapi maoni ya serikali tatu mpaka awe na ujasiri wa kuyaweka kwenye rasimu ya katiba?

source RFA gazeti Mtanzania.

DUUUH wazanzibar sasa hamna shukrani..

Wanaoshangaa ni magamba kwani wanaona watakosa fulsa za kupewa madaraka Bara kama walivyo zoea. Wazanzibari wa kawaida wanataka wawe na Full Sovereign Government ili wajiamulie mambo yao wenyewe kwa rasirimali zao. Watanganyika tunataka serikali yetu ili asiwepo wa kumtegemea mwenzake, wote tuchangie sawa kwenye Serikali ya Shirikisho.
 
Unaposema wazanzibari unamaanisha nini? Yaani maoni ya mtu mmoja unayaunganisha kwa watu wote. Umepita shule kweli wewe? Au ndiye walewale waliyoifanya serikali iunde tume kuchunguza matokeo?
Mbona nyiemnamsikiliza maakimu seif?
 
Wanaoshangaa ni magamba kwani wanaona watakosa fulsa za kupewa madaraka Bara kama walivyo zoea. Wazanzibari wa kawaida wanataka wawe na Full Sovereign Government ili wajiamulie mambo yao wenyewe kwa rasirimali zao. Watanganyika tunataka serikali yetu ili asiwepo wa kumtegemea mwenzake, wote tuchangie sawa kwenye Serikali ya Shirikisho.

Serikali ya Shirikisho la Afrika Mashariki Mkuu. Kitu kinaitwa Tanzania sahau!
Huko Afrika Mashariki ndo shirikisho tunataka tukakutane. Forget Shirikisho jengine hapa...
 
Pigeni kazi yakhee! Hamtalelewa tena na wabara. C mlianza chokochoko nyie! Mtageuka soko le2.
 
Tanzania tutaifkia kama tulivyowafukia waliyoileta, Tukishapata Tanganyika yetu tunaelekea kuzima na kufukia Mwenge kama tulivofukia waliouleta! Tanganyika kwanza mengine baadae. Tunataka Ilala na buguruni yetu
 
warioba alipokuwa anahojiwa na itv dk 45 alisema wanzanzibari wengi walioongea nao wakati wa ukusanyaji maoni ya katiba waliutaka muungano ila walitaka mambo fulani yarekebishwe, ila watanzania bara wengi waliukataa muungano, hii ikaonesha kuwa wabara hawautaki kuungano na wanzanzibari wanautaka mungano, sijui warioba alimaanisha alichokuwa anaongea au aliongea kwa makusudi fulani.
 
Wazanzibari ndio wamekuwa wanalilia serikali tatu kwa muda mrefu.

Maoni ya serikali tatu sio ya wajumbe wa Tume ya katiba bali ni ya wananchi.

Wazanzibari walitaka serikali tatu ili wapewe mamlaka kamili lakini baada ya kukuta mambo waliyotaka bado yako kwenye Muungano wameona ni heri kumwaga mboga ili wote tushindwe kula kwani Warioba kamwaga ugali.
 
Ndio lazima wamshangae kwa maana wao walitaka muungano wa mkataba na Zanzibar yenye mamlaka kamili na warioba akakiri ni wengi walotaka muundo huo
 
Kwa hiyo Wazanzibari wanataka wao wawe na Serikali na Tanganyika tusiwe na Serikali yetu. Wao wajulikane kama taifa sisi kama jimbo. Inapofikia hapo naona muungano ni kiini macho.

Tume za Majaji Kisanga na Bomani zote zilipendekeza serikali tatu. Tume ya Jaji Warioba ni ya tatu kupendekeza serikali tatu. Pendekezo hili ni muhimu na ndiyo mahitaji ya wananchi. Watawala wanaweza wakalipuuza hili kwa manufaa yao ya muda mfupi. Watajuta na kusaga meno.
 
Wamezoea kuwa kupe enh!! tumeghairi habari ya serikali mbili NO' kama wanataka iwe serikali moja
la basi ziwe serikali tatu.huu mchezo wa kuwa wanataka wao wawe serikali kamili halafu bado wawe kwenye
muungano na nchi isiyokuwepo hatutaki' Tanganyika kwanza'
 
Unaposema wazanzibari unamaanisha nini? Yaani maoni ya mtu mmoja unayaunganisha kwa watu wote. Umepita shule kweli wewe? Au ndiye walewale waliyoifanya serikali iunde tume kuchunguza matokeo?

.....namaanisha waliberali kama una swali lingine uliza.
 
Wazanzibar wamehoji na kumshangaa warioba wadai ameyatoa wapi maoni ya serikali tatu mpaka awe na ujasiri wa kuyaweka kwenye rasimu ya katiba?

source RFA gazeti Mtanzania.

DUUUH wazanzibar sasa hamna shukrani..

Acha uwongo Zanzibar wanataka serikali tatu.
 
Wazanzibar wamehoji na kumshangaa warioba wadai ameyatoa wapi maoni ya serikali tatu mpaka awe na ujasiri wa kuyaweka kwenye rasimu ya katiba?

source RFA gazeti Mtanzania.

DUUUH wazanzibar sasa hamna shukrani..
Labda wanataka seriikali moja ya Zanzibaar tu, na Tanganyika iwe mkoa Siku zote wamekuwa wanalalama wanaonewa kumbe walikuwa wana neep? Pokeeni sasa mmepigiwa
 
Wazanzibar wamehoji na kumshangaa warioba wadai ameyatoa wapi maoni ya serikali tatu mpaka awe na ujasiri wa kuyaweka kwenye rasimu ya katiba?

source RFA gazeti Mtanzania.

DUUUH wazanzibar sasa hamna shukrani..

hayo ni mawazo yako na huyo mwandishi wa gazeti lako itabidi tuwaulize na nyie hii kauli mmeitoa wapi.
 
wazanzibari wengi sana wamehoji wapi au kauri ya sefu ndiyo unataka kuifanya ya wazanzibar?,mawazo kama haya mimi huyaita ya kupotosha na uchochezi.
 
Zanzibr kwanza,porojo pelekeni butiama.
 
Back
Top Bottom