Wazanzibar Wamshangaa Warioba kwa kupendekeza serikali tatu!

Wazanzibar Wamshangaa Warioba kwa kupendekeza serikali tatu!

Kwanza haya ni maoni ya Waryoba au ya wa wananchi kama yalivyochambuliwa na Kamati. Kama ni ya Waryoba na mimi nina hofu kubwa na kama inatokana na uchambuzi wa maoni yetu uliofanywa na Kamati mimi sina hofu kabisa maana mimi ni nani kupinga ya wengi Tanzania yote?
Tulikuwa na serikali mbili nia ikiwa kuelekea serikali moja. Kweli naheshimu maoni ya wengi ya serikali tatu. Maoni yangu binafsi niliyotoa ni kutoka serikali mbili ni serikali moja au muungano kuvunjika na hiki ndicho nilidhani wazanzibari wanataka na hasa wanapofikia kutamka muungano wa mkataba - Si bahati, kamati ilizuiwa kufanya zaidi katika hadidu rejea. Tatizo ni serikali haikutoa uhuru Kamati iseme kile wananchi wanataka kuhusu muungano.
 
kweli kabisa tusipoteze muda kulumbana!tunataka zanzibar huru na tanganyika huru; hapo tutaheshimiana tu!
 
hawa wazanzibar kweli waajabu sana yaani wawe na nchi kamili sisi tusiwe na nchi still wawe ndani ya muungano?
 
wazanzbar waacheni waende they need thier oman ruler back wanakosa misaada chini ya oic, wanataka kuhalalisha uliberali.
 
kama hawataki afadhali waondoke coz wanayunyonya tu bure serikali moja au tatu wachague moja.
 
kwani tunavutana kwa nini si kila nchi ijitambue na ijiendeshe yenyewe? kwanini tulaumiane? utawala wa kulazimishana haujengi taifa.
 
tunataka serikali tatu hata sisi wabongo tumechoka kusikia na kuona kilasiku waliokwenye serikali hawabadiliki, kama sababu chama kushika hatamu sasa tubadilikeni tuache kudanganywa kwa umasikini wakati bara tuko matajiri kwani twaogopa nini? kila mmoja awe na dola yake.
 
Vyovyote iwavyo, suala la Zanzibar kuweza kujiamulia mambo yake yenyewe ndilo linalotakikana kwa sasa. Uite Muungano wa Serikali tatu, mbili au mkataba. After all what is in a name?
 
Back
Top Bottom