Wazanzibar Wamshangaa Warioba kwa kupendekeza serikali tatu!

Wazanzibar Wamshangaa Warioba kwa kupendekeza serikali tatu!

warioba alipokuwa anahojiwa na itv dk 45 alisema wanzanzibari wengi walioongea nao wakati wa ukusanyaji maoni ya katiba waliutaka muungano ila walitaka mambo fulani yarekebishwe, ila watanzania bara wengi waliukataa muungano, hii ikaonesha kuwa wabara hawautaki kuungano na wanzanzibari wanautaka mungano, sijui warioba alimaanisha alichokuwa anaongea au aliongea kwa makusudi fulani.

Inawezekana Warioba alikosea. Tunachojua sie ni kwamba Wazanzibari weeeeengi sana hawautaki muungano. Na sababu ni moja tu: Muungano hauna faida kwao. Sisi watu wa bara tulio wengi tunachagua kukubaliana na wanzanzibari: Muungano hauna faida kwa Wazanzibari. Watoke!
 
hayo ni mawazo yako na huyo mwandishi wa gazeti lako itabidi tuwaulize na nyie hii kauli mmeitoa wapi.

.....mtajua Wenyewe c mlituoana watanganyika maboya sasa kimenuka.
 
Mimi najiuliza mustahabali wa wazanzibari waliojazana Tanganyika endapo muungano utavunjika, hivi hata wasipoondoka Tanganyika hakutatokea XENOPHOBIA kweli? Hatutaanza kuwashambulia kweli hawa ndugu zetu? Mungu alipitishie mbali hili, lakini naona kwa Rasimu hii bado Wazenji watakuwa favoured sana sijui tuwasaidie vipi tena maana rasimu inasema uraia ni suala la muungano ambapo ni advantage sana kwao!
 
Unaposema wazanzibari unamaanisha nini? Yaani maoni ya mtu mmoja unayaunganisha kwa watu wote. Umepita shule kweli wewe? Au ndiye walewale waliyoifanya serikali iunde tume kuchunguza matokeo?

Wazanzibari wapewe haki yao ili Tanganyika yetu irudi. Usitokwe povu...
 
Hata hivyo wanzazibar wasiwe wafinyu wa uweledi, kwani hayo maoni yalichukuliwa zanzibar pekee? je wanafikiri wanzazibar wangeweza pendekeza tanganyika irudi wakati hawana maslahi nayo?
 
Hivi ni kweli Muungano unawanyonya wazanzibar? Maana naona ni wao ndio wanataka Zanzibar huru, lakini waTanganyika wao wapo kimya kuhusu Tanganyika yao, je wao hawahitaji nchi yao ambayo imefunikwa katika vitabu vya historia tu? Hapa naona kama kuna umuhimu wa kuwa na serikali ya muungano basi kuwe na serikali tatu ili na Tanganyika nayo iweze kurudi katika ramani...Nawasilisha.
 
Wa upande wa pili wa muungano mnataka nini, mbona mnaongelea ZNZ tu? Tanganyika au Tanzania Bara?

Ha ha ha!
 
Mimi najiuliza mustahabali wa wazanzibari waliojazana Tanganyika endapo muungano utavunjika, hivi hata wasipoondoka Tanganyika hakutatokea XENOPHOBIA kweli? Hatutaanza kuwashambulia kweli hawa ndugu zetu? Mungu alipitishie mbali hili, lakini naona kwa Rasimu hii bado Wazenji watakuwa favoured sana sijui tuwasaidie vipi tena maana rasimu inasema uraia ni suala la muungano ambapo ni advantage sana kwao!

Wazanzibari wameshawaoa sana watanganyika. Usihofu hakuna unyanyapaa utakaotokea.

We uliona wapi mtu akampiga shemeji yake wakati dada yake amewekwa ndani na anatunzwa vizuri?
 
Unaposema wazanzibari unamaanisha nini? Yaani maoni ya mtu mmoja unayaunganisha kwa watu wote. Umepita shule kweli wewe? Au ndiye walewale waliyoifanya serikali iunde tume kuchunguza matokeo?

ni mtu mmoja kivipi? angekuwa hapati watu wanaomuunga mkono kwenye mikutano yake, hapo ungesema ni mtu mmoja.

Kamati ya Maridhiano Six: MKUTANO WA MAMLAKA KAMILI DAY; 01/06/2013; Part 1 - YouTube

Kamati ya Maridhiano Six: MKUTANO WA MAMLAKA KAMILI DAY; 01/06/2013; Part 4 - YouTube

Kamati ya Maridhiano Six: MKUTANO WA MAMLAKA KAMILI DAY; 01/06/2013; Part 2 - YouTube
 
Mie ni Mtanganyika wa kuzaliwa na mtanzania Bara wa kulazimishwa!
 
Kuna wazanzibari na wazanzibara [ni wale vibaraka kutoka Dodoma] wanaona kana kwamba tonge sasa washanyang'anywa, sasa wamefadhaika hawajuwi watapata wapi ulaji,
 
Somethings simply dont make sense . whats the point of shirikisho la Tanzania ndani ya shirikisho la EA? (huko ndipo tunapo kwenda).NONSENSE kabisa.
 
Tanzania tutaifkia kama tulivyowafukia waliyoileta, Tukishapata Tanganyika yetu tunaelekea kuzima na kufukia Mwenge kama tulivofukia waliouleta! Tanganyika kwanza mengine baadae. Tunataka Ilala na buguruni yetu

Umesahau Msasani na Tandika!!!
 
Duh! Fikra zako zinakupeleka pabaya. Kwani ulizani sisi tuombe ndio mutukadirie cha kutupa, sivyo hivyo tunachotaka ndio tupewe na sio mutuchagulie. 66% tulitaka mkataba na sio serikali 3. Izo tatu tulishaachana nazo toka 2005. Zishapitwa na wakati.
Wazanzibar wamehoji na kumshangaa warioba wadai ameyatoa wapi maoni ya serikali tatu mpaka awe na ujasiri wa kuyaweka kwenye rasimu ya katiba?

source: gazeti RAIA mwema.

DUUUH wazanzibar sasa hamna shukrani..
 
Wewe ndio naona hujenda shule, maana 66.3% kusema ni maoni ya mtu mmoja sijui nani hajenda shule kati yako na huyo ulomjibu. NB. Saa nyengine uwe makini usirejee kosa.
 
Tusipoteze muda kulumbana! Tanganyika irejeshe serikali yake ili kila moja ijitenge kwa muda wa miaka 10-15. Kisha tuone kama kuna haja tena ya muungano!
 
Wewe ndio naona hujenda shule, maana 66.3% kusema ni maoni ya mtu mmoja sijui nani hajenda shule kati yako na huyo ulomjibu. NB. Saa nyengine uwe makini usirejee kosa.

hao 66.3% umepimaje, au unachukua data zilizopikwa na wengine. Nenda Zanzibar kaulize, hapo ndio utajua ukweli.
Kosa unalifanya wewe kuamini data zilizopikwa. Majority ya wazanzibar wanataka serikali yao yenye mamlaka kamili na hii hawakuanza kuidai leo wala jana. Inaelekea wewe either ni teenager hujashuhudia vuta nikute ya muungano au umekuwa brain washed au umeamua kujitoa akili kwa sababu kuna watu wanakulipa kuja humu mtandaoni.
 
Kuna wazanzibari na wazanzibara [ni wale vibaraka kutoka Dodoma] wanaona kana kwamba tonge sasa washanyang'anywa, sasa wamefadhaika hawajuwi watapata wapi ulaji,

Na hao ndio wapo kwenye bunge la jamhuri ya muungano, na hao ndio wanaounga mkono muungano na kuufanya muungano uendelee kuwepo kwa sababu wao wanaangalia matonge yao zaidi kuliko mtazamo wa watu wengi wa zanzibar. Na kwa vile bunge la jamhuri limekuwa na maamuzi ya mwisho, ndio maana muungano una survive mpaka leo.
 
Back
Top Bottom