Wanaotaka serikali mbili ni MACCM na hao ndio wanaofaidika na hizo serikali mbili ,mwananchi wa kawaida wala hawezi kuwa na mshiko wa aina yeyote ile.
Wananchi wa ZANZIBAR walio wengi wanahitaji au wanataka serikali tatu na kaama haiwezekani basi Muungano na ufilie mbali.
Hao WAZANZIBARI Wachache waishio Tanganyika hawawezi kuzuia hilo kwani ,wahenga walisema mdharau kwao atakuwa amepotoka ,ni kitu gani kiliwapeleka huko ? Na kitu gani kinaweza kuwarudisha kwao ? Je ni serikali moja ,mbili au tatu ,kwa maoni yangu hakuna hata moja katika hayo ,nilionalo ni hali ya maisha ya mtu mmoja mmoja ,ni wapi ameona atapata afadhali ,kuna wabara au tuseme watanganyika kibao wapo Zanzibar na vitega uchumi vyao ikiwemo maguesthouse ,mabaa ,hoteli wakiwemo waajiriwa katika sekta binafsi hata za ulinzi wa nyumba ,maduka na sehemu zinazoegeshwa magari nyakati za usiku ,mbali ya hao kuna wakulima ambao wanamashamba yao binafsi na wanamiliki mashamba hayo japo ni ya kulima karanga na viazi vitamu ,wote hao ni watanganyika na wapo pia waTanganyika waliokimbia kodi huko kwao bara na hujishugulisha na kuuza bidhaa mbalimbali manjiani ikiwemo njugu na vinyago.
Kitu gani kiliwakimbiza Tanganyika na kurukia Zanzibar ilihali madai yenu kuwa huko ni bora kuliko Zanzibar ? Jawabu langu kwa upande wangu ni lilelile la hali ya maisha anavyoimudu mtu mmoja mmoja na ilivyo ndani ya akili yake ni wapi anaweza kumudu na kujiendeleza.
Kauli za Zanzibar ambazo niliwahi kuzisikia katika mikutano hasa ya CUF mwanzoni mwa harakati za kukisimamisha chama ni kuwa hata Muungano ukivunjika basi hatafukuzwa mtu ,awe polisi jeshi ,wa serikalini au mwananchi wa kawaida hilo halipo ndani ya agenda ,ni yeye na uamuzi wake kama ataamua kurudi Tanganyika au atabakia Zanzibar kwani lengo la kuanzisha au kudai serikali tatu si kuwafukuza watu ni kutaka kuboresha hali ya Zanzibar kimaisha ,haiaminiki ya kwamba wageni kutoka Tanganyika ndio sababu ya kudumaa uchumi wa Zanzibar ,madai ni serikali ya Tanzania inainyonya na kuibamiza serikali ya Zanzibar na faida kubwa humezwa na viongozi waliomo ndani ya serikali hiyo na Zanzibar hakuna maendeleo yanayoonekana ,sasa ndani ya muundo wa serikali mbili mmoja hapati maendeleo nchi yake haiendi mbele,misaada nayo pia haifiki Zanzibar ,sasa ikiwa itakuwa serikali moja ,si ndio kabisa kutakufa na kuwa kama kisiwa cha wavuvi ? :biggrin1:
Ubora ni serikali tatu au mbili ya Tanganyika na Zanzibar ,bila ya kufukuzwa mtu ,wahuku arudi kwao na wa huku aludi kwao hilo halipo na kama litakuwepo waathirika hawatakuwa WaZanzibari peke yao hata WaTanganyika litawagusa.
Na zaidi mmesahau kama kuna mchakato wa DUAL CITIZEN ambao unakaribia kukubalika ,hivyo hakuna atakaerudi kwao ,
MaCCM mpoo :biggrin1: