Wazanzibari bado wanataka OIC, Watanganyika tubariki tuyaone maendeleo

Hivi unaitumia akili yako ipasavyo kweli 🤔 yani nchi ijiunge na huo upuuzi kisa watu wachache wasiokua na faida yoyote na nchi 🤔 vipi wewe
 
Na Watanzania wote. Kuwe na referrendum.
Kwa mujibu wa katiba yao, Zanzibar ni nchi, haihitaji ruhusa ya mtu yoyote kufanya jambo lolote lenye maslahi ya Zanzibar.

Hata Muungano, kwa vile wakati unaingiwa Wanzanzibari hawakuulizwa na kuridhia, ni Tanganyika tuu ndio tuliridhia, then Zanzibar are free to ask the Zanzibaris kama wanautaka Muungano au laa.
P
 
Wapi katiba yao imesema hivyo?
 
Anotaka kuja kutalii Zanzibar anitafute tuongee
Tour Nzuri zipo na utaenjoy sana tu

Karibuni
 
Fanyeni haraka kabla hajaja mkristo akatibua mipango 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Mzee noma sana huyu.
 
Katiba ya Zanzibar ni batili na inapaswa kufutwa, kinachoiweka mpaka sasa ni viongozi wa CCM kutokuheshimu katiba ya Jamuhuri ya Tanzania!
 
Hiv huyo aliongea yamekemewa popote? Na kama hajakemewa na yeyote na popote ina maana wamekubaliana na mawazo yake? Wanzazibar wote wapewe ajira mwinyi akishrikiana na Samia Kwa kua ni waisilamu ? Hizo ajira Samia atakazoshrikiana na mwinyi kuwapa hizo sehem za ajira zitausisha hao vijana wa kizanzibar kupata ajira zitausisha pia tz bara? Na hizo OIC Huwa wanatoka ajira zipi baada ya kujiunga? Mbona mm hizo ajira zinanituma ni makundi ya kigaidi kama zilivyo nchi nyingi zilivyo jiunga na OIC? Mzungumzaji hajatueleza OIC Huwa wanatoa wap ajira kuwapa vijana wa nchi zilizo jiunga nao,,na Kwa nn hawatoi hizo ajira Kwa waisilamu wa nchi ambazo Bado sio wanachama wao?
 
Wajiunge ni haki yao sababu ni nchi yao, muungano uvunjwe haraka
Kujiunga hatutajiunga kamwe ,na Muungano hautavunjika,hao wanao sema Zanzibar tujiunge OIC ni wahuni sana,sisi Wazanzibar tunafaid meng sana kutoka tz bara,kulko wao wanavyofaid kutoka tz visiwan, kulko tutoke Bora tutawaliwe na tz bara.HATUKO TAYARI KUJIUNGA NA OIC!!!
 
Umenichekesha sn, umesema kweli tupu
 
Ndiyo wanachokitaka
 
Wapewe kura ya maoni kuwauliza kama wanautaka Muungano au hawautaki.

Huo ndio mzizi wa fitina hizi nyingine ni mazungumzo baada ya habari tu.
Wakati Warioba akikusanya maoni kuhusu katiba mpya walitaka serikali tatu kwa hiyo tusijifanye hatukusikia au hatujui!
 
Huyu ni kiongozi wa Chadema Zanzibar! Mrema ambaye ni mwenezi wa Chadema amejitenga na kauli ya huyu kiongozi kuwa ni kauli yake binafsi na si maoni ya Chadema!
 
Wazanzibar wanaweza kunufaika zaidi na OIC katika maendeleo yao kupitia njia kadhaa:

1. Ushirikiano wa Kiuchumi: OIC inaweza kusaidia Zanzibar kuimarisha biashara na uwekezaji kutoka nchi za wanachama. Hii inaweza kuleta miradi ya maendeleo, ajira, na rasilimali za kifedha.

2. Msaada wa Kijamii: OIC ina mipango mbalimbali ya kusaidia jamii, kama vile elimu, afya, na maendeleo ya jamii. Wazanzibar wanaweza kupata msaada katika sekta hizi, kuboresha maisha yao.

3. Kujifunza na Kubadilishana Maarifa: OIC inatoa fursa kwa nchi wanachama kubadilishana uzoefu na maarifa katika sekta mbalimbali, kama vile kilimo, teknolojia, na utawala bora. Hii inaweza kuboresha mbinu za maendeleo katika Zanzibar.

4. Ushirikiano wa Kisiasa: Kujiunga na OIC kunaweza kuongeza sauti ya Zanzibar katika masuala ya kimataifa na kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine za Kiislamu.

5. Mikakati ya Maendeleo Endelevu: OIC ina mipango ya maendeleo endelevu ambayo inaweza kusaidia Zanzibar kuzingatia malengo ya maendeleo yanayohusiana na mazingira, afya, na ustawi wa jamii.

6. Msaada wa Kiufundi: OIC inaweza kutoa msaada wa kiufundi katika miradi maalum, kama vile ujenzi wa miundombinu na teknolojia ya habari.

Kwa ujumla, ushirikiano na OIC unaweza kusaidia Zanzibar kufikia malengo yake ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wake.
 
Wakati Warioba akikusanya maoni kuhusu katiba mpya walitaka serikali tatu kwa hiyo tusijifanye hatukusikia au hatujui!
Inawezekana walisema wanataka serikali tatu kwa sababu wametishwa kisheria kwamba kuvunja muungano ni uhaini, na tume ya Warioba haikuuliza kuuvunja Muungano, iliuliza muundo wa Muungano.

Tuwape uhuru watoe maoni kama wanautaka muungano au wanataka kuuvunja.

Wanapiga kelele sana, ni haki yao kuamua.
 
Tatizo si Wazanzibari kujiunga na OIC.

Tatizo ni udini na na Uzanzibari aliousema Mzee. Kwamba Samia Muislam, Mwinyi Muislam, Kombo Muislam, Masauni Muislam, wote Wazanzibari, wajiunge na OIC haraka, asije rais Mkristo akaharibu mambo.

Hii ni kauli ya kubagua Watanzania kidini, kinyume na katiba za Tanzania, Zanzibar na CHADEMA.
 
Kasema hawataki kuletewa pundamilia...

kumbe Tanganyika wanagawa mpaka maliasili kwa Zanzibar...

Hakuna watu mazuzu duniani kama Watanganyika

Julius Nyerere, Baba wa Taifa la mazezeta, vizazi vya mbele vinavyosoma shule binafsi, na vyenye access ya tehama ya kuwafumbua upeo kama watu wengine duniani, watakuja kusema alivyokuwa na uelewa wa Chifu Mangungo
 
Labda kama hukuwepo wakati ule, watu walikuwa wanatoa maoni kwa uhuru kabisa na wala hakukuwa na questionnaire ya kujaza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…