Wazanzibari ni raia daraja la kwanza katika JMT

Wazanzibari ni raia daraja la kwanza katika JMT

Watu wa Zanzibar wapo juu sana ktk kila kitu
 
Heshima kwenu,

Sasa ni wazi kabisa katika Muungano wetu Wazanzibar wana uraia pacha (uRaia wa Zanzibar na uRaia wa JMT).

Mosi Wazanzibar wana uRaia wa Zanzibar, kupitia sheria zao ambazo wamezipitisha katika BLW (Baraza la Wawakilishi) ambalo WaTanganyika hawaruhusiwi kutia mguu. Kupitia BLW WaZanzibar wamekuwa wakipitisha sheria mbali mbali ambazo kwa namna moja zimekuwa zikiwabagua WaTanganyika.

Kupitia BLW Raia wa Zanzibar wana haki za kumiliki ardhi, kuajiriwa katika serekali na mashirika ya umma kama Bandari, Bank, Bima. Ni marufuka kubwa kuajiri waTanganyika (Machogo).

Kupitia BLW Wazanzibar wamepitisha sheria ambayo wanaitambua Zanzibar kama nchi ambayo ina mipaka yake ya nchi na bahari. Katika ya JMT inaitambua Zanzibar kama sehemu ya Tanzania. Sasa sijui Majeshi yetu yana linda nini huku nchi ya Zanzibar.

Kupitia hilo BLW Wazanzibar wote wana uRaia wa TANZANIA sawa na waTanganyika! Kupitia katiba yetu ambayo haiheshimiwi WaZanzibar wana haki zote huku Tanganyika ikiwemo ya kumiliki ardhi, kugombea nafasi yoyote ya kisiasa, kuajiriwa mahali popote bila bugudha yoyote.
Kwa maana hiyo, hata sehemu za koloni hilo zikigawiwa kwa wajomba zetu, upande wetu ni sisi wazanzibar tunaofaidika. Hatuna uchungu wowote kugawa sehemu hiyo ya hilo eneo, kwa sababu huku kwetu Zanzibar ni neema tupu.

Nikuhakikishie, leo hii Mwalimu Nyerere angefufuka na kukuta hali hii iliyopo sasa atatusikitikia sana sisi waTanzania. Asingeweza hata kwa dakika moja aunde Muungano kama huu tulionao wakati huu.
 
hiyo ekari moja ataipata wapi? Aseme square mita 400 mpaka 500 basi ni shida.
Usipindishe, swali hapa siyo kuipata hiyo eka moja au sehemu ndogo ya ardhi hiyo, tatizo ni kuweka sheria kubagua watu wa nchi moja.
 
anzibar ardhi ni ndogo ndio maana wanaruhusiwa kuja kuishi bara. Ni kama vile Moshi ardhi ni ndogo ndio maana Wachaga wanaenda kuishi maeneo mengine ya Tanzania, kwa sababu Mtanzania ana uhuru wa kuishi popote ndani ya Tanzania.
Lakini sijawahi kusikia watu wa Moshi wakikataza wanaotaka kwenda kuishi huko wakikatazwa, pamoja na udogo wa ardhi ya huko, au wewe ulishasikia hilo?
Kwa hiyo Zanzibar ni ya kipekee sana.
 
Ushaambiwa zanzibar ni ndogo hakuna nafasi kwa mmbara kupata ardhi kule ila wazanzibar ruksa kupata ardhi bara tena waje kwa wingi. Tena unaambiwa visiwa hivyo ni tunu ya JMT vilindwe na vihifadhiwe ili visipoteze hadhi na asili yake. Ni kama hifadhi ya taifa
Kama suala ni udogo wa Zanzibar vipi kuhusu suala la uraia na kazi(ajira) kwa wa kuwa na uraia wa pande mbili? Bila shaka hoja ya udogo wa Zanzibar ni ya kujaribu kuhadaa watu wasihoji kuhusu muungano huo wa upande mmoja.

Rasimu ya katiba ya jaji Warioba ilipendekeza kuwepo kwa serikali tatu ili muungano uonekane ni muungano kweli na sio porojo za ccm.
 
Mtikila alikuwa sahihi Tanganyika wageni ndio wanaoifaidi raisi mzenji makamo ni rund, makamu mwenyekiti CCM msomali.

Mawaziri kibao ni wasome, wanyarwanda, wamalawi na waarabu kama zung
Mzanzibati Kaja huku bara
1. kauza bandari zote
2.kauza mbuga zote,
3.kauza misitu Ile deal ya carbon credit
Watanganyika wapo wamelala upumbavu huu
 
Lakini sijawahi kusikia watu wa Moshi wakikataza wanaotaka kwenda kuishi huko wakikatazwa, pamoja na udogo wa ardhi ya huko, au wewe ulishasikia hilo?
Kwa hiyo Zanzibar ni ya kipekee sana.
wanasema zanzibar ni ndogo wabara wakihamia huko itapoteza uasilia wake. Kwa hiyo inatunzwa ibaki hivyohivyo ila wao wanaruhusiwa kwenda bara ni pakubwa
 
Usipindishe, swali hapa siyo kuipata hiyo eka moja au sehemu ndogo ya ardhi hiyo, tatizo ni kuweka sheria kubagua watu wa nchi moja.
hapana cha kupindisha hapo, hebu ulizeni hao wanaoishi zanzibar ni kweli hawapati ardhi ya kununua? Nyinyi munajisemea tu humu kwenye mitandao lakini wale wenye nia hasa huwa wanapata ardhi.
 
hapana cha kupindisha hapo, hebu ulizeni hao wanaoishi zanzibar ni kweli hawapati ardhi ya kununua? Nyinyi munajisemea tu humu kwenye mitandao lakini wale wenye nia hasa huwa wanapata ardhi.

Hawa watu dawa yao ni huu uvamizi uvunjike haya maneno maneno yaishe tuwawache na Raisi wao Mchaga
 
Zanzibar ardhi ni ndogo ndio maana wanaruhusiwa kuja kuishi bara. Ni kama vile Moshi ardhi ni ndogo ndio maana Wachaga wanaenda kuishi maeneo mengine ya Tanzania, kwa sababu Mtanzania ana uhuru wa kuishi popote ndani ya Tanzania.

Sasa umewahi kusikia kwamba kwa kuwa Moshi ardhi ni ndogo basi makabila mengine hawaruhusiwi kununua ardhi ya Wachaga huko Moshi? Na kuna mtu amekuambia huko Zanzibar hakuna soko la ardhi kwa sababu ni ndogo? Au umesikia popote kwamba watu wa bara wakinunua Zanzibar watalazimisha wauziwe ili wabanane na watu wa Zanzibar?

Mtu ambaye anatoa sababu za watu wa bara wasinunue ardhi Zanzibar kwa sababu ya udogo wa ardhi si mjinga, bali ni mpumbavu na hana akili, hata kama yuko kwenye Baraza la Wawakilishi au ni kiongozi wa Zanzibar au serikali ya Muungano
Ni ubaguzi tu hakuna kingine.Nimewahi kwenda Zazibar nikaona plot inauzwa, nilimuuliza mwenyeji wangu kama naweza kununua hiyo plot. Jibu lake lilikuwa ni vigumu sana. Sasa swali ni kwamba, kama plot inauzwa na sisi wote ni watanzania, iwapo muuzaji amekubaliana na bei ninayotaka kununua, kuna shida gani mimi kununua kama sio ubaguzi tu?
 
Ukanunue ardhi Zanzibar ili iweje? Hata mpira huwezi kucheza ukipiga shuti linaangukia baharini
 
Ni ubaguzi tu hakuna kingine.Nimewahi kwenda Zazibar nikaona plot inauzwa, nilimuuliza mwenyeji wangu kama naweza kununua hiyo plot. Jibu lake lilikuwa ni vigumu sana. Sasa swali ni kwamba, kama plot inauzwa na sisi wote ni watanzania, iwapo muuzaji amekubaliana na bei ninayotaka kununua, kuna shida gani mimi kununua kama sio ubaguzi tu?

Ndiyo bora huu uvamizi uvunjike mbaki na Raisi wenu Mbowe
 
Ni ubaguzi tu hakuna kingine.Nimewahi kwenda Zazibar nikaona plot inauzwa, nilimuuliza mwenyeji wangu kama naweza kununua hiyo plot. Jibu lake lilikuwa ni vigumu sana. Sasa swali ni kwamba, kama plot inauzwa na sisi wote ni watanzania, iwapo muuzaji amekubaliana na bei ninayotaka kununua, kuna shida gani mimi kununua kama sio ubaguzi tu?

Wale uamsho walipoyasema haya walikamatwa na kufungwa miaka zaidi ya 9 wakabambikiwa kesi Za kigaidi , Tutaona jee hawa waliotamka haya watafanywa kitu gani ??
 
Mzanzibati Kaja huku bara
1. kauza bandari zote
2.kauza mbuga zote,
3.kauza misitu Ile deal ya carbon credit
Watanganyika wapo wamelala upumbavu huu
Kauza na KIA kwa wajomba zake wa Oman.
 
Heshima kwenu,

Sasa ni wazi kabisa katika Muungano wetu Wazanzibar wana uraia pacha (uRaia wa Zanzibar na uRaia wa JMT).

Mosi Wazanzibar wana uRaia wa Zanzibar, kupitia sheria zao ambazo wamezipitisha katika BLW (Baraza la Wawakilishi) ambalo WaTanganyika hawaruhusiwi kutia mguu. Kupitia BLW WaZanzibar wamekuwa wakipitisha sheria mbali mbali ambazo kwa namna moja zimekuwa zikiwabagua WaTanganyika.

Kupitia BLW Raia wa Zanzibar wana haki za kumiliki ardhi, kuajiriwa katika serekali na mashirika ya umma kama Bandari, Bank, Bima. Ni marufuka kubwa kuajiri waTanganyika (Machogo).

Kupitia BLW Wazanzibar wamepitisha sheria ambayo wanaitambua Zanzibar kama nchi ambayo ina mipaka yake ya nchi na bahari. Katika ya JMT inaitambua Zanzibar kama sehemu ya Tanzania. Sasa sijui Majeshi yetu yana linda nini huku nchi ya Zanzibar.

Kupitia hilo BLW Wazanzibar wote wana uRaia wa TANZANIA sawa na waTanganyika! Kupitia katiba yetu ambayo haiheshimiwi WaZanzibar wana haki zote huku Tanganyika ikiwemo ya kumiliki ardhi, kugombea nafasi yoyote ya kisiasa, kuajiriwa mahali popote bila bugudha yoyote.

Maelezo ya Mbowe ni kuikandamiza zaidi Zanzibar. Kwani hoja zake Rais asitoke Zanzibar ( sehemu ndogo kuiongoza kubwa) .
Hoja ya pili ni idadi ya Wabunge kulingana na idadi ya watu.
Hoja zote sio za haki ya nchi mbili zilizoungana, ni hoja za mmoja kummeza mwengine na kuwa moja.
Kwa nini asiseme Sudan ya Kusini yenye mil 10 kuwa na uwakilishi sawa wa wabunge na Tanzania mil 65 katika bunge la afrika mashariki.
 
Hawa watu dawa yao ni huu uvamizi uvunjike haya maneno maneno yaishe tuwawache na Raisi wao Mchaga
nimeamini kweli watz bara wanapenda ugomvi, maana sasa mumekomaa na zanzibar na huku akina mama wao wamekomaa na wakenya.
 
Back
Top Bottom