Wazanzibari waliumbua Bunge! Taasisi 7 zilinyimwa fursa kutoa maoni katika rasimu ya katiba!

Wazanzibari waliumbua Bunge! Taasisi 7 zilinyimwa fursa kutoa maoni katika rasimu ya katiba!

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
  • Taasisi ambazo zimeshiriki mkutano huo ni pamoja na TAMWA, Zanzibar Youth Forum, Zanzibar Law Society, Baraza la Katiba, Pemba Press Club, Jumuiya ya Waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar na ZAFELA.

Taasisi za kiraia Zanzibar zimesema hazijawahi kushirikishwa katika kuiboresha Muswada wa sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya Tanzania.

Taasisi hizo saba ambazo zinaongozwa na Baraza la Katiba Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Pr. Abdul Sharif zilisema Bunge halijawatendea haki kwa kunyimwa fursa ya kutoa maoni katika sheria hiyo. Waliyasema hayo huko Bwawani Zanzibar walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jana.

Katibu wa Zanzibar Youth Forum Alimasi Mohammed Ali alisema kushirikishwa Serikali ya Mapinduzi haina maana kwamba na wananchi wameshirikishwa.

“Muswada ule ulipokuja mwanzo, viongozi wa serikali waliitwa Bwawani na sisi raia wa kawaida tuliitwa katika skuli ya Haile Salasi kutoa maoni yetu” alisema Ali.

Alisema haoni sababu kwa muswada huu wa sheria hiyo kupewa fursa serikali peke yake na wao kama raia wakaonekana kama hawana maana.

“Walijua fika kwamba Wazanzibar hawawezi kukubali kuwa wachache katika Bunge la Katiba na bara kuwa wengi” alisema Ali.

Alifananisha na tume ya mabadiliko ya katiba kwamba ilikwenda kwa wananchi mara mbili tofauti. Kwa nini kamati ya Katiba na Sheria ishindwe. “Hatukubaliani hata siku moja kwa Bara wawe na 64% na Zanzibar kubakia na 36% wakati ni nchi mbili sawa katika Muungano” alieleza Ali.

Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar Pr Abdul Sharif alisema kwa mujibu wa sheria ingalikuwa vyema Muswada huo ukaonekana katika magazeti ili wananchi watoe maoni yao.

“Mimi mwenyewe nilikuwa na mapendekezo yangu lakini hawakunipatia fursa ya kutoa mawazo yangu” alisema Pr. Sharif.

Alisema wameutoa mswada huo katika kabati na kuupeleka Bungeni tu, halafu wanajidai wananchi wamepata fursa si kweli. Aliendeleaa.

Taasisi ambazo zimeshiriki mkutano huo ni pamoja na TAMWA, Zanzibar Youth Forum, Zanzibar Law Society, Baraza la Katiba, Pemba Press Club, Jumuiya ya Waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar na ZAFELA.

CHANZO: Nipashe
 
Patamu hapo njia ya mwongo ni fupi, kama Pinda alishaongopa ndani ya bunge utarajie wenzake wasimfuate?
 
Hiyo ndio CCM na Serikali yake Sikivu kwa Kubaka Haki za Kiraia...
 
Maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 yanadaiwa kuwa yalibadilishwa dakika za mwisho na kwamba suala hilo ndicho kiini cha vurugu zilizotokea bungeni mjini Dodoma juzi.

Gazeti hili limefanikiwa kuona nakala inayodaiwa kuwa ni maoni ya awali ya kamati hiyo ambayo yalikuwa na mapendekezo yanayotaka kuwapo kwa marekebisho kadhaa kwenye muswada huo, tofauti na yale yaliyowasilishwa bungeni juzi na Mwenyekiti wa Kamati, Pindi Chana.

Jumatano na Alhamisi wiki hii kulikuwa na mvutano mkubwa bungeni kiasi cha wabunge wa upinzani kutoka vyama vitatu vya NCCR -Mageuzi, Chadema na CUF kuungana na kususia mjadala kuhusu muswada huo.

Imedokezwa kuwa mvutano mkali kuhusu muswada huo ulianza ndani ya kamati hiyo wakati wajumbe wake ambao ni wabunge wa CCM walipotumia wingi wao kubadili maoni ya awali na kuweka maoni mapya, hatua ambayo inadaiwa kuwa ilikuwa na msukumo wa Serikali nyuma yake.

Ndani ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, wabunge wa upinzani ambao kwa idadi yao ni wachache walishindwa kuzuia mabadiliko hayo ya "lala salama" yanayodaiwa kuwa yaliwekwa Septemba 2, mwaka huu, hivyo waliazimia kuhamasisha wabunge wote wa upinzani kupinga marekebisho hayo kutokana na sababu kuu mbili.

Sababu hizo ni kutofanyika kwa mikutano ya wazi kwa umma (public hearing) upande wa Zanzibar na hatua ya kuwapo kwa mapendekezo ya Rais kurundikiwa madaraka makubwa ya uteuzi wa wabunge kutoka asasi za kijamii watakaoingia katika Bunge la Katiba.

Habari zinasema wakati fulani Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alitembelea kamati hiyo wakati ikiedelea na vikao vyake na kukuta mvutano mkali kuhusu suala la marekebisho ya sheria ya sheria hiyo na alishauri kwamba pale ambapo hawataweza kuelewana basi wasubiri uamuzi ndani ya Bunge.

Jana gazeti hili lilimtafuta Chana kupitia simu yake ya mkononi na baada ya kumweleza kuhusu madai hayo alisema: "Tafadhali sana kwa sasa niko kwenye kikao, kwanza simu yako nimeipokea kwa heshima tu, tutafutane wakati mwingine".

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alikiri kwamba kulikuwa na mapendekezo ya kuongeza idadi ya wabunge na namna ya kuwapata, lakini Serikali iliyakataa katika hatua ya majadiliano kabla ya suala hilo kufikishwa bungeni.

Tofauti ya maoni

Nakala ya taarifa ya awali ilipendekezwa kuwa katika kuteua wajumbe 166 wa Bunge la Katiba, Rais azingatie kikamilifu mtiririko wa mapendekezo ya kila kundi lililoainishwa katika kifungu cha (1) (c).

"Na endapo Rais hatazingatia mapendekezo ya kundi mojawapo, Rais afanye mrejesho kwa taarifa kwa kundi husika juu ya sababu za kutozingatia mtiririko wa mapendekezo yaliyowasilishwa kwake," inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa kamati hiyo ilikuwa na maoni kwamba makundi mengine ya kijamii yaongezwe katika kifungu cha 22(1) (c) cha sheria mama, ili kupanua wigo wa uwakilishi mpana katika Bunge la Katiba, hivyo kuongeza idadi ya wabunge hao kutoka idadi ya awali 166 hadi kufikia 201.

"Kamati inashauri kuwa idadi ya wajumbe iwe 201 badala ya idadi ya wajumbe 166 iliyotajwa katika sheria mama, ili kupata idadi ya wajumbe watakaounda Bunge Maalumu la Katiba," inasomeka taarifa hiyo.

Hata hivyo, maoni hayo yanatofautiana na yale yaliyowasilishwa bungeni juzi na jana, kwani yanaonyesha kwamba kulikuwa na majadiliano na mashauriano baina ya kamati na Serikali, hivyo ilikubaliana kuwa "Rais apewe mamlaka ya kufanya uteuzi wa wajumbe Bunge la Katiba" huku idadi ya wabunge wa kuteuliwa wakibaki 166.

Kifungu hicho kiliondoa haki ya kila taasisi kuteua jina la mjumbe wake katika Bunge hilo na badala yake, ikapendekezwa kuwa Rais atapelekewa matatu ili ateue moja kati ya hayo.

Hata hivyo, jana wakati Bunge lilipoketi kama kamati kwa ajili ya kupitia vifungu vya marekebisho ya muswada huo, Serikali iliwasilisha marekebisho ya nyongeza ambayo yanazitaka asasi za kiraia ziteue majina tisa na kati ya hayo Rais anaweza kuteua jina moja na kama asiporidhika anaweza kuteua mtu kutoka nje ya orodha hiyo.

Kuhusu suala hilo Chikawe alisema: "Tangu awali ilikuwa inaonyesha wajumbe ni 166. Ni kweli Kamati ilipendekeza wajumbe hao waongezeke hadi 201 lakini pendekezo hilo halikukubaliwa, ikabakia wajumbe watakuwa 166."

Ushiriki wa Zanzibar

Itakumbukwa kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilipewa wiki nne za kuendesha vikao vyake kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 12 wa Bunge uliomalizika jana, tofauti na kamati nyingine ambazo zilipewa wiki mbili.

Baadhi ya wabunge (hasa wa upinzani) wanasema madhumuni ya kupewa muda huo ni kama hayakutimia kwani hawakuweza kupokea maoni kutoka kwa makundi muhimu hasa ya upande wa Zanzibar kama ilivyokusudiwa.

Hata hivyo, jana Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idd, alilihakikishia Bunge kuwa upande wa Zanzibar ulishirikishwa katika kutoa maoni ya muswada huo.

Hatua ya Balozi Idd kutoa ufafanuzi ilitokana na mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba(CCM) aliyeomba kwa vile Balozi Seif yuko ndani ya Bunge basi apewe fursa kufafanua utata huo.

Kauli ya Balozi Idd inapingana na ile iliyotolewa juzi jioni na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ambaye alisema ni kosa kubwa kamati kutochukua maoni ya Wazanzibar.


Lissu alisema kulikuwa na njama tangu mwanzo za kuhakikisha kuwa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala haichukui maoni ya Wazanzibari na hilo linathibitishwa na ratiba zilizokuwa zimeandaliwa na kamati.

"Katika orodha ya wadau wote 22 waliokuwa wameorodheshwa katika kutoa maoni yao juu ya muswada huu hakukuwa na Mzanzibari hata mmoja…tulipoipitia tukasema hapana Wazanzibari wako wapi," alisema.

Lissu alisema yeye, Mwenyekiti wa Kamati, Chana na Makamu Mwenyekiti, William Ngeleja walikwenda kumwona Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah na kumweleza azma yao ya kwenda kuzungumza na wadau wa Zanzibar.

"Katibu akatwambia kwamba yeye ana fedha za kutuwezesha kukaa Zanzibar hata wiki moja, kwa hiyo tukarudi kwenye kamati tukatengeneza ratiba mpya na tukaongeza wadau sita wa Tanganyika na Wazanzibari wanane," alisema Lissu.

Aliwataja wadau hao kuwa ni Chuo cha Taifa Zanzibar, Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chama cha Mawakili Zanzibar, Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar, Chama cha Walemavu Zanzibar na Profesa Abdul Shariff.

Wadau wengine walikuwa ni Shirikisho la Vyama visivyo vya Kiserikali Zanzibar (Angoza) na Jumuiya ya Misikiti Zanzibar na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, lakini hatukuwahi kukutana nao na kupokea maoni yao.

"Tukakubaliana kuwa tutakaa Zanzibar kwa siku tatu kuanzia Julai 14 hadi Julai 16 mpaka leo hatujawahi kuambiwa kwa nini tulizuiwa kwenda Zanzibar, lakini maneno yaliyokuwa yakisikika eti kwa sababu za kiusalama," alisema.

Lissu alisema wakati kamati yao ikiambiwa haiwezi kwenda Zanzibar kwa sababu za kiusalama, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge hilo ilikuwa Pemba ikiendelea na ziara zake.

 
Haya sasa, Watanzania mnaodanganywa na kina Lukuvu, Werema,Pindi Chana wakilindwa na Ndugai ma polisi, waulizeni walikutana wapi na hao Wazanzibari? Hapa nni nani muongo? ni Lissu au Ccm? Mtakubali kudanganywa hadi lini? Miaka 50 bado haiwatoshi? Acheni kuishabikia Ccm, jaina mia njema na Tanzania
 
Kila Mtanzania anayo haki ya kutoa maoni, hi ni haki kwa wote.
 
Maige alishambulia Bunge
Wakati wabunge wa CCM wakiwashambulia wenzao wa kambi rasmi ya upinzani waliosusia muswada huo, Mbunge wa Msalala, Ezekil Maige (CCM), amelishambulia Bunge, hususan kiti cha Spika kwa kushindwa kutumia busara kuepusha vurugu bungeni.

Katika taarifa yake aliyoitoa kupitia mtandao wa Kijamii wa Wanabidii, Maige ambaye amepata kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kuwa alitazama kwa mshangao na kutoamini kuhusu kilichojiri bungeni juzi.


Alisema kwa bahati mbaya hakuwepo Dodoma siku hiyo kwani alikuwa mjini Arusha kikazi, lakini hakuona sababu kabisa ya kufikia hapo kwani hali hiyo ingeweza kuepushwa na kiti cha Spika.

"Ingewezekana kabisa kuahirisha muswada na kutoa nafasi kwa Kamati ya Katiba na Sheria kwenda Zanzibar kupata maoni ya wenzetu wa huko.
"Najua kuna maelezo mazuri ya kushirikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Lakini kikanuni, Baada ya Muswada kusomwa mara ya kwanza, unakuwa mikononi mwa Bunge na kamati ndiyo inayokusanya maoni si serikali," alisema Maige.

Maige ambaye anakuwa mbunge wa kwanza wa CCM kukosoa kiti cha Spika, alisema kwa kuwa hakuna ushahidi wa ‘public hearing' kufanyika Zanzibar na kuwasikia Wazanzibari wa kawaida (nje ya serikali), basi kulikuwa na hoja kabisa ya kurekebisha kasoro hiyo kwa kutoa nafasi kwa kamati kwenda Zanzibar.

"Suala la Katiba ni kubwa hivyo ni vema zikafanyika jitihada za kutosha kuhakikisha tunakwenda pamoja (na wenzetu hasa wenye mtazamo tofauti na sisi) badala ya kutumia wingi wetu kwani mwisho wa safari tukienda hivi wapo watakaodai Katiba Mpya si yao, hivyo kuikosesha ‘social legitimacy'," alisema.

Kwa mujibu wa Maige, hatua ya Ndugai kutomsikiliza Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, nako kulitibua mambo bila sababu.

"Mbowe angepewa nafasi ya kusikilizwa, hata kama hoja yake isipokubaliwa ingekuwa nafuu sana na shari na aibu ya jana ingeepukika.
"Tumesameheana, lakini tujifunze na tujitahidi sana kwenda kwa maelewano," alisema Maige katika taarifa hiyo.

CC
chama
 
Patamu hapo njia ya mwongo ni fupi, kama Pinda alishaongopa ndani ya bunge utarajie wenzake wasimfuate?

Hakuna waziri mkuu mzigo aliyewahi kutokea Tanzania/Tanganyika kama Pinda!! Huyu jamaa ni muongo,mnafiki ana kila sifa za kishenzi!
 
Wapi Lukuvi? Ipo siku shimo litakuja kuchimbika pale kati.
 
Patamu hapo
njia ya mwongo ni fupi, kama Pinda alishaongopa ndani ya bunge utarajie
wenzake wasimfuate?

maadam wamekiri kuwa serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar imeshirikishwa, tunaamini kuwa zanzibar imeshirikishwa. jukumu la kutunga sheria ni la Bunge na wengine hushirikishwa pale inapoona inafaa hususan wadau muhimu
 
Pindi Chana .....anasema wameshirikishwa JAHAZI ASILI....kwa niaba ya wa zanzibar ....na eti moani ya CUF yapo kwenye serekali kwa maana serekali ni ya mseto .....duuuuuuu
 
Haya sasa, Watanzania mnaodanganywa na kina Lukuvu, Werema,Pindi Chana wakilindwa na Ndugai ma polisi, waulizeni walikutana wapi na hao Wazanzibari? Hapa nni nani muongo? ni Lissu au Ccm? Mtakubali kudanganywa hadi lini? Miaka 50 bado haiwatoshi? Acheni kuishabikia Ccm, jaina mia njema na Tanzania

R.i.p CCM!
 
kumbe sikutupa kura yangu bure kuichagua chadema.
CHADEMA YATOSHA!
 
Haya sasa, Watanzania
mnaodanganywa na kina Lukuvu, Werema,Pindi Chana wakilindwa na Ndugai ma
polisi, waulizeni walikutana wapi na hao Wazanzibari? Hapa nni nani
muongo? ni Lissu au Ccm? Mtakubali kudanganywa hadi lini? Miaka 50 bado
haiwatoshi? Acheni kuishabikia Ccm, jaina mia njema na Tanzania

tunasikiliza maoni na kauli za viongozi wetu. hatusikilizi maneno ya mitaani na ya watu wenye njaa
 
Hapo patamu cdm hawakurupuki ccm kwa kuwadanganya 2 wananchi hamjambo lissu ni sawa na lukuvi+chana+pinda 200
 
Back
Top Bottom