Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Maige
alishambulia Bunge
Wakati
wabunge wa CCM wakiwashambulia wenzao wa kambi rasmi ya upinzani
waliosusia muswada huo, Mbunge wa Msalala, Ezekil Maige (CCM),
amelishambulia Bunge, hususan kiti cha Spika kwa kushindwa kutumia
busara kuepusha vurugu bungeni.
Katika taarifa yake aliyoitoa kupitia mtandao wa Kijamii wa Wanabidii,
Maige ambaye amepata kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema
kuwa alitazama kwa mshangao na kutoamini kuhusu kilichojiri bungeni
juzi.
Alisema kwa bahati mbaya hakuwepo Dodoma siku hiyo kwani alikuwa mjini
Arusha kikazi, lakini hakuona sababu kabisa ya kufikia hapo kwani hali
hiyo ingeweza kuepushwa na kiti cha
Spika.
Ingewezekana
kabisa kuahirisha muswada na kutoa nafasi kwa Kamati ya Katiba na
Sheria kwenda Zanzibar kupata maoni ya wenzetu wa
huko.
Najua
kuna maelezo mazuri ya kushirikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Lakini kikanuni, Baada ya Muswada kusomwa mara ya kwanza, unakuwa
mikononi mwa Bunge na kamati ndiyo inayokusanya maoni si serikali,
alisema Maige.
Maige ambaye anakuwa mbunge wa kwanza wa CCM kukosoa kiti cha Spika,
alisema kwa kuwa hakuna ushahidi wa public hearing kufanyika Zanzibar
na kuwasikia Wazanzibari wa kawaida (nje ya serikali), basi kulikuwa na
hoja kabisa ya kurekebisha kasoro hiyo kwa kutoa nafasi kwa kamati
kwenda Zanzibar.
Suala
la Katiba ni kubwa hivyo ni vema zikafanyika jitihada za kutosha
kuhakikisha tunakwenda pamoja (na wenzetu hasa wenye mtazamo tofauti na
sisi) badala ya kutumia wingi wetu kwani mwisho wa safari tukienda hivi
wapo watakaodai Katiba Mpya si yao, hivyo kuikosesha social
legitimacy, alisema.
Kwa mujibu wa Maige, hatua ya Ndugai kutomsikiliza Kiongozi Mkuu wa
Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, nako kulitibua mambo bila
sababu.
Mbowe
angepewa nafasi ya kusikilizwa, hata kama hoja yake isipokubaliwa
ingekuwa nafuu sana na shari na aibu ya jana
ingeepukika.
Tumesameheana,
lakini tujifunze na tujitahidi sana kwenda kwa maelewano, alisema
Maige katika taarifa hiyo.
CC
chama
hana lolote maige. anaonesha hasira za kuvuliwa Urais. fisadi mkubwa huyu