Mkuu,
Sema wewe hupati lolote alilofanya lakini sii wote kwa sababu huna kumbukumbu.na kibaya zaidi unataka kumhukumu mtu hoja zake ukiwa mtupu..
Ikiwa Zanzibar ilipigania Uhuru wake toka mwaka 1963 unajua Salim alikuwa wapi na akifanya nini!.. Unajua kwamba Salim ndiye alikuwa muasisi wa Zanzibar student Union na pia Secretary General wa chama cha waandishi Zanzibar wakati akiwa Chief editor..
Umezungumzia wakati akiwa na nafasi nono amewahi kufanya kipi! je, umesahau kwamba waakti wote akiwa PM, huyo Sharrif Hamad alikuwa Waziri kiongozi Zanzibar (1984 -1988). sijui huyu alileta mabadiliko gani kwani kazi unayodai haikuwa ya Salim peke yake.. Team kubwa ya Wazanzibar walishika madaraka ya juu kabisa ktk Uongozi wa serikali ya Jamhuri toka Makamu wa rais, PM, Waziri kiongozi huyo Seif Sharrif Hamad na kina Mwinyi akiwa Waziri wa mambo ya ndani.. Hawa walifanya nini?
Mkuu wakati Salim akiwa madarakani, ni wakati ambao Tanzania ilikuwa shwari kabisa hapakuwepo na migogoro kama ya leo hii pamoja na kwamba bara walitakiwa kubeba pass kuingia Visiwani.. hakuna aliyejali wala kufikiria utengano kwa vipimo kama mnavyotaka kutumia.Leo hii unaona CCM bara wameshika wizara zote kuendeleza libeneke la Ufisadi..I mean mkuu tazama wizara zetu leo hii wangapi wantoka Zanzibar na wameshika wizara gani?..
Mkuu ni lazima usome wakati na kuelewa kinatendeka kitu gani leo hii..Tanzania ya Nyerere pamoja na lawama zote zinazotolewa dhidi yake ilikuwa shwari kabisa kila upande uliridhika na mfumo wa uongozi..Ni pale tu tulipoanzisha vyama vingi ndipo tulipoharibu kila kitu, kwa sababu viongozi wengi wamejipanga kuchukua ruzuku na sii kutetea maslahi ya nchi.
Mtu kama Salim ni sumu ya mafisadi, hanunuliki na amechukiwa sana kila sehemu aloongoza kwa sababu hapendi mission town ktk ofisi zake. hapendi kuzembea na kupendelea ndugu ktk ajira...Hatoi wala hachukui rushwa kitu ambacho baada ya Azimio la Zanzibar kupitishwa alimwagwa.
Ni mtu ambaye kulingana na mazingira ya Kidanganyika naweza kusema ana roho mbaya! kwani sisi mtu anayejali sana maslahi ya Taifa ni mjinga, mchovu na atakufa maskini.He is the only person mimi ningempigia kura yangu bila hata kuuliza kama angepitia mwaka 2005 potelea mbali umri wake.
Hakika mtu yeyote anayetaka Wazanzibar waungane kwanza kuondoa tofauti zao ni mawazo makini sana kwa pande zote mbili... na siku Wazanzibar watakapo fanya hivyo, thubutu CCM kufanya tena walofanya Pemba mwaka 2000.. itakuwa kazi mpya..
Mkandara
Napenda kuzungumzia mambo makubwa 3 kutokana na habari yako nzuri uliyoitoa hapo juu!na kikubwa zaidi ni mada yenyewe hasa kuhusu kuimarika kwa Muungano wa znz miongoni mwao!
Kwanza sio kweli kama ulivyosema hapo juu kuwa Dr Salim alipokuwa kwenye madaraka ZNZ haikujikita kwenye migogoro kama hii ya leo.Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa ZNZ ilijitumbukiza kwenye mgogoro mkubwa wa kisiasa tena wa chama kimoja kipindi ambacho Dr Salim alikuwepo madarakani kuzidi hata sasa ambapo ni mfumo wa vyama vingi!tuanze na vifo vya Mzee Khasim Hanga na Dr Othman nambaye hadi leo miili yao haijulikani ilipo na kifo cha Rais Karume pale Kisiwandui,Dr Salim alikuwepo madarakani na machafuko yake yalikuwa makubwa sana na dalili za kwanza kujitenga kwa wana znz kutokana na vifo hivyo.
Mambo makubwa zaidi 2 yaliyosabisha na kuwafanya wanzn watengane ni haya;
@Mapinduzi haramu ya kumtoa madarakani Rais wa 2 wa znz ambaye alichaguliwa kikatiba Mzee Jumbe mwaka 1984 kwa kila walichokiita akina Nyerere na wenzake"kuharibika kwa hali ya hewa znz".Mkandara kipindi hicho Dr Salim yupo tz na ana madaraka makubwa sana,Nyerere alitutangazia habari hii akiwa Dar na pembeni yake alikuwepo Dr Salim.
@Kufukuzwa kwa uanachama wan CCM 1988 wenye msimamo mkali hasa wenye asili ya Pemba kwa kile kilichojulikana kama"saficha CCM",kipindi hicho bado Dr Salim alikuwa na nguvu sana kwenye siasa za tz.
@Kubadilishwa katiba ya tz na kumfanya Rais wa znz awe kama mkuu wa mkoa kimuungano,kumbuka kuwa Rais na Makamu wake wakiwa nje ya tz PM anachukua madaraka,ili hali kachaguliwa na watu wa jimbo la Mpanda tu!jambo hili liliwagawa sana waznz hasa waliopo madarakani na wasio na kitu.Dr Salim hadi leo hajalikemea jambo hili linalowafanya waznz wapigane vijembe!
Serikali kuu ilizidisha utengano kwa wanzn ili hali waznz waliopo madarakani kama akina Mwinyi,Salim na wengineo wakiwa tu wametulia tuli.Tulishuhudia wana harakati waliojaribu kutetea U-znz wao bila kujali itikadi za kisiasa wakiishia kituo cha Polisi cha Madema na baadae gereza lenye balaa la Kiinua-Miguu!
Nahitimisha kuwa kutengana kwa wanzn sio suala la jana au leo,lina mizizi yake toka miaka mingi sana na hawa akina Dr Salim hawawezi kukwepa lawama hizi toka akiwa balozi wetu Misri,Waziri wa kigeni,Waziri wa Ulinzi,PM,nfasi kubwa kubwa za kimataifa na nyinginezo.Salim hakukemea wala kueleza hisia zake pale ambapo wanzn walipotengwa ndani ya katiba,pale mbapo kundi moja la wana znz lilipodhulumiwa haki zake wala pale ambapo kundi la mzee Jumbe lilipodhihakiwa adharani.
Ni nani waliopindisha uchaguzi wa CCM wa kumpata atakayerithi Urais wa ZNZ kutoka kwa mzee Mwinyi kati ya Abdul Wakil na Maalim Seif mwaka 84?Mzee Wakil alishinda kihalali?Wanzn si ndiyo walianza kujitenga hapo kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba hata machafuko ya mwaka 2000 yalikuwa ni hitimisho tu la kutengana kwa wanzn?
Baadhi ya wanzn wanaotoka upande mmoja wa nchi wanadhulumiwa haki zao waziwazi,wanafukuzwa kazi na kuvunjiwa makazi yao,na haya yanatendeka hawa akina Dr Salim wanayaona!Yaliyomkuta wakili Mbwelezeni,Yusufu Hariri aliyekuwa mwakilishi wa Konde, na watu wengine mashuhuri,kutengwa zaidi kwa Dr Ghalib hata aliposhinda kura za maoni mwaka 2000 kunafanya zaidi kuwa kitu kimoja kwa waznz kuwa kama wimbo tu!
Mkandara,msome vizuri mzee huyu na utakuja kukubaliana na mimi kuwa nae ni mmoja kati ya waliochangia kuwafanya waznz wajitenge!