Wazazi hawakuelewana Mahari, Binti anataka atoroke Nyumbani aje kwangu

  • Kama hayupo tayari kuwatii wazazi wake ambao wamemlea tangu azaliwe; jiandae zamu yako ikifika
  • Kama anatishia kujiua haujamuoa; uwezekano mkubwa mkipata changamoto atajiua akiamini ndio suluhisho pekee

Maoni yangu: hakuna mwanamke hapo, endelea kutafuta.
Sio kweli Kuna time wazazi huwa wanawachalewesha mabinti Kwa tamaa zao za kiboya tu mwishoe wanaharibikiwa na Maisha so Binti anajua anataka Nini kwenye maisha na kafanya maamuzi
 
safi sana mkuu!Ushauri mzuri lakini nini matokeo ya binti baada ya kutoroka?
 
Wakuu
Mimi ni kijana wa umri wa kuoa (miaka kati ya 23-30),mwezi wa nane mwaka jana nilienda kuchumbua katika kijiji jirani,

Nilienda na mwenyeji wangu,NA zoezi la kuchumbia lilikamilika na kishika uchumba tuliacha Tsh.10,000(kwa wale wasukuma watakubaliana na mimi kuhusu mchakato wa kuchumbia),

Badae wazazi wangu na wa mchumba wangu wakakutana kupanga mahari,lakini kiukweli hawakuelewana,wazazi wa binti walisema ng'ombe 12 lakini wazazi wangu walisema ni milioni mbili na laki mbili tu,hivyo hawakuelewana na wakapotezeana.

Lakini binti akazisaka namba zangu mpaka akazipata, tukawa tunawasiliana,anasema ananipenda na anataka tuoane tu licha ya wazazi kutoelewana,anataka kutoroka nyumbani kwao aje kwetu kuolewa,licha ya kumchenga chenga kuwa asubili lakini imefikia hatua binti analia anasema anakuja.
Na nikikataa atajinyonga

Mwishowe nikashawishika, akaniambia nimtumie hela ya kuja kwetu,ndo juzi nimemtumia elfu kumi atoroke aje kwetu

Wajuvi wa mambo mnanishauri/mnanisaidia vipi katika hili?

Karibuni.
Tafuta jukwaa la watoto umekosea njia
 
Pata baraka ya wazazi ni muhimu sana, ana hamu ya kupika na kupakua bila baraka za wazazi wake, huyo ni binadamu lolote laweza kutokea
 
Wazazi wake ndiyo wanamtoa kijanja hivyo wala siyo utashi wa binti,amepangwa tu baada ya kuona mmeenda kimoja.

2.2M mbona mahari standard kabisa hivyo usukumani.

NB:Kumpokea ni kutengeneza mahusiano mabovu na wakwe zako watarajiwa maana huwa kuna faini juu kwa kutorosha binti wa watu mbali na mahari.
 
"Kauli ya kwamba sikuachi mpaka kifo ni kama sifa..
 Inasemwa na wengi ila wachache wana maanisha..
wale wapambe na mashahidi wa kujivika au keki na mauwa ambayo mwisho hupukutika"

Dizasta vina: Ndoano
 
Inamaana mzeebaba hadi unaenda kuchumbia ulikuwa huna namba ya huyo mchumba! Au hana simu!
 
wazazi wa binti waliona mbali kama nauli tu unatuma 10k utaweza majukumu ya kutunza mke?
 
Shida ilianzia hapo kwenye elfu 10, ndio maana wakahitaji idadi ya ng'ombe wengi ili uachane na binti yao. Chakula ulichokula tu siku hiyo inazidi elf 10.
 
Back
Top Bottom