Wazazi kama mna hii midoli, ichomeni moto

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,678
Reaction score
27,653
๐Ÿ˜ˆ๐Ÿงธ THE DEMON BEHIND THE SMILE: PAZUZU VS LABUBU

Your browser is not able to display this video.

Katika historia ya kale, watu wengi waliabudu miungu ya uongo kama Ashera, Bali, Zeus, Dagon, Hubal na mingineyo. Leo hii, roho zilezile zimerudi duniani, lakini zimevaa majina na sura mpya ili kuabudiwa na watu bila wao kujua.,

Huko nyuma nilionesha jinsi miungu kama Hubal anavyoabudiwa sasa, mungu baali pia ,n.k

Yesu aliwahi kumwambia Msamaria:

๐Ÿ“– โ€œNinyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa maana wokovu watoka kwa Wayahudi.โ€ (Yohana 4:22)

Maneno haya yanaonyesha kuwa watu wanaweza kabisa kuabudu bila kuelewa wanachokiabudu. Hali hiyo ndiyo tunayoshuhudia sasa: wengi wanamuabudu Shetani wakidhani wanamwabudu Mungu.

Mfano

Hubal amerudi na anaabudiwa leo kwa sura mpya.Na anapiganiwa kabisa

Baali amerudi kupitia tamaduni na ibada za kisasa.

Na sasa, Pazuzu amerudi lakini kwa njia ya midoli ya watoto.

Leo tutaangalia jinsi pepo huyu alivyorudi kupitia kinachoitwa Labubu dolls.

Tukio la Owasso

Katika siku za hivi karibuni, wakazi wa Owasso (Oklahoma, Marekani) wameshangazwa na mabango katika Cherry Street yanayoeleza kwamba Labubu dolls si midoli ya kawaida, bali ni pepo Pazuzu.

Mabango haya yaliwekwa na mama mmoja wa Lifechurch na yameambatana na ombi la kuchangisha $150,000 ili kununua na kuharibu kinachoitwa Labubu Alpha kinachoelezwa kuwa ni โ€œpepo mkuuโ€ kati ya vinyago hivyo.

Pazuzu ni pepo kutoka Mesopotamia ya kale, anayejulikana kama Mfalme wa Pepo wa Upepo Mbaya. Anaelezwa kuwa na๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mabawa na makucha,

Tabasamu la dhihaka lililoganda,

Macho makali yenye kutisha.

Ingawa aliogopwa, mara nyingine alitumika kama โ€œmlinziโ€ dhidi ya pepo wengine lakini kwa gharama ya kutafuta msaada kwa pepo. Hii ni sawa na kushinda giza kwa giza.

๐Ÿ“– โ€œMsishirikiane na matendo yasiyo na tunda ya giza, bali yaweeni mkikemea.โ€ (Waefeso 5:11)

Leo hii, mfano wa Pazuzu unajitokeza kupitia Labubu dolls, midoli midogo inayovuma kwenye mitandao ya kijamii, hasa TikTok.

Lakini tabasamu la Labubu lililoganda na macho yake matupu yanabeba alama za giza.

Pazuzu alionekana wazi kama pepo.

Labubu anajificha kama mdoli wakupendeza.

Wote wana tabasamu lililoganda

Hatari ya Michezo na Midoli Yenye Asili ya Kishetani

Wengi wanasema: โ€œNi midoli tu ya kuchezea.โ€ Lakini maandiko yanatufundisha kuwa na tahadhari kubwa:

๐Ÿ“– โ€œMsiwe na miungu mingine ila mimi.โ€ (Kutoka 20:3)
๐Ÿ“– โ€œWatoto wangu, jilindeni nafsi zenu na sanamu.โ€ (1 Yohana 5:21)

Hata vitu vinavyoonekana vidogo na visivyo na madhara vinapokuwa na mizizi ya giza vinaweza kufungua mlango wa roho chafu.

Kuna taarifa kutoka familia moja ya Tulsa kuwa mtoto wao wa kike (miaka 7) alianza kupata ndoto za kutisha mara baada ya kupewa doll ya Labubu kama zawadi ya kuzaliwa.

Usiku wa kwanza, mtoto alilia akisema mdoli unamuangalia na kutabasamu.

Baada ya wiki moja, alianza kuzungumza akiwa usingizini kana kwamba anazungumza na kitu kisichoonekana.

Hatimaye alisikia sauti ikimuita kutoka kwenye mdoli huyo

Wazazi walipompeleka mdoli kanisani ili achomwe moto, walieleza kulikuwa na kelele za ajabu kutoka ndani yake kana kwamba kuna kitu kinapinga.

๐Ÿ‘‰ Kisa hiki kimetajwa kwenye mijadala ya makanisa huko Oklahoma kama onyo la wazi juu ya hatari za Labubu dolls.

Mabango ya Owasso yameonya pia kuhusu tamaa ya mali kupitia midoli hii.

Yanawekwa sokoni kama โ€œlimited editionโ€ au โ€œrare piece.โ€

Yameundwa kuamsha tamaa ya kutaka zaidi na zaidi.

๐Ÿ“– โ€œKwa maana shina la mabaya yote ni kupenda fedha.โ€ (1 Timotheo 6:10)

๐Ÿ‘‰ Midoli kama Labubu si burudani tu bali somo la ulimbukeni, tamaa na ibada za uongo.

Watoto wana akili nyepesi na huathirika haraka na wanachoona. Kumzowesha mtoto na midoli yenye asili ya kishetani ni sawa na kumfundisha ibada ya uongo kwa vitendo.

๐Ÿ“– โ€œMlee mtoto katika njia impasayo naye hata akiisha kuwa mzee hataiacha.โ€ (Mithali 22:6)

๐Ÿ‘‰ Ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa kutokana na hila za giza.

Leo imefichuliwa wazi kupitia michezo, muziki, mitindo ya mavazi, mitandao ya kijamii na sasa midoli. Giza limefanywa kuwa jambo la kawaida.

Labubu na mfano wake ni sehemu ya programu ya kiutamaduni za giza.

๐Ÿ“– โ€œJihadharini, simameni imara katika imani, iwekeni nguvu zenu, iweni wakubwa wa moyo.โ€ (1 Wakorintho 16:13)

Pazuzu alikuwa pepo wa giza katika Babeli. Labubu ni mfano wake wa kisasa, anayevaa tabasamu la mdoll. Tabasamu lake limeganda, macho yake ni matupu, na ujumbe wake ni wa giza.

๐Ÿ“– โ€œAdui wenu ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ili apate kummeza.โ€ (1 Petro 5:8)

๐Ÿ‘‰ Ulimwengu hautakusadia kukuokoa bali kukuharibu.

Ni wajibu wetu wazazi kuwa macho, kuwalinda watoto na kusimama imara dhidi ya hila za giza.
 
Wamarekani wanamuonea wivu mchina

Wanamchukia Labubu sababu ni mdoli aliependwa kwenye soko ambae hajaanzishwa na mmarekani

Mbona mdoli Barbie hawamsemi vibaya?
Sio kweli kwamba Wamarekani wanamchukia Labubu kwa sababu ametoka China. Barbie naye anakosolewa mara nyingi, tofauti ni kwamba Labubu ameunganishwa na simulizi za ushirikina na hofu, ndiyo maana anazungumziwa vibaya. Hii si vita ya kitaifa, bali ni jinsi simulizi inavyopokewa na jamii.

Wamarekani hununua na kutumia bidhaa nyingi za China bila matatizo (electronics, nguo, vinyago, nk).

Kama ni wivu, bidhaa nyingi za Kichina zingepigwa vita, lakini hazifanyiwi hivyo.
 
Uongo
 
Asante mkuu kwa ujumbe huu, naomba uendelee kutuabarisha kila upatapo nafasi, ubarikiwe sana ๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Wamarekani wanamuonea wivu mchina

Wanamchukia Labubu sababu ni mdoli aliependwa kwenye soko ambae hajaanzishwa na mmarekani

Mbona mdoli Barbie hawamsemi vibaya?
wanataka watu wachome moto shetani aka midoli ๐Ÿ˜‚
 
wanataka watu wachome moto shetani aka midoli ๐Ÿ˜‚
Shetani anatumia vitu ,ndio maana hata manabii wa uongo wanasisitiza sana objects

Unaungamanishwa na roho chafu kupitia object

Huwezi kurogwa kamwe bila kufungua mlango Fulani kwenye maisha yako ,ndio maana itahitajika kitu chako ili urogwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ