Watoto wana haki ya kudeka na kufaidi matunda ya wazazi lakini ni muhimu pia wao wajifunze kuwajenga uwezo wa kujisimamia bila backup ya mzazi.
Kwa maisha ya kiuhalisia ya hapa bongo lolote laweza tokea ila angalau mtu ajue kujifulia nguo, kuweza kutumia usafiri wa umma, kuweza kula vyakula kama ugali, kuweza kujitetea anapoonewa, kuweza kumingle na watu wa matabaka mbali mbali, kuweza kufanya kazi za nyumbani bila msaada wa house girl, n.k.
Inashangaza kuona kuna watoto:

- Hawajui kujifulia, Ni mpaka house girl au mashine
- Hawawezi kufika sehemu ya mbali hadi wafikishwe,
- Hawawezi kula ugali, Haya nimeshuhudia kwa macho yangu
- Wakionewa hawawezi kujitetea hadi mzazi aje
- Ngumu kumingle na watu wa matabaka ya kawaida
- House girl asipokuwepo wanaweza kulala njaa, n.k.