Wazazi na Walezi Mtwara wajitolea kuchimba Msingi kwa Ujenzi wa uzio Shule ya Sekondari Chuno

Wazazi na Walezi Mtwara wajitolea kuchimba Msingi kwa Ujenzi wa uzio Shule ya Sekondari Chuno

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Wazazi na walezi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara wamehamasika kujitolea kuchimba msingi katika ujenzi wa uzio shule ya sekondari chuno ili kudhibiti wanafunzi kuingia na kutoka shuleni kiholela.

Kukamilika kwa uzio katika shule hiyo ya Sekondari Chuno kutasaidia wanafunzi kuhudhulia vipindi vyote vya masomo.

Baadhi ya wananchi hao akiwemo Shakira Mustafa amesema baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakitoroka na kwenda katika maeneo yasiyofaa huku baadhi yao wakijiingiza katika vitendo vya kihalifu.

1741183882185.png
Ameongeza kuwa kukamilika kwa uzio huo utasaidia kuondoa changamoto hiyo na kufanya wanafunzi kuhudhulia vipindi vyote vya masomo na hatimaye kuongeza ufauru .

Diwani wa kata ya Chuno Fanikio Chijinga amesema ujenzi huo ni azimio la kikao ambacho waliazimia kila mzazi kuchangia elfu 32000 ili waweze kukamilisha ujenzi wa uzio huo.

Katika kuunga mkono juhudi za wananchi hao Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Hassan Nyange ameahidi kugharamia malipo kwa mafundi ambao watajenga uzio huo na kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Hassan Mtenga ameahidi kutoa tofali 1,000

Mkuu wa shule ya sekondari Chuno Mwalimu Hamisi Kaoneka amesema pamoja na mambo mengine ujenzi huo unakwenda kuondoa adha ya watu kukatiza eneo la shule bila utaratibu maalumu,wanafunzi kufika shuleni kwa wakati pamoja na kulinda miundombinu ya shule.

Snapinst.app_482739958_18389594299111588_5117039898141352651_n_1080.jpg
1741183999903.png
 
Back
Top Bottom