Ni zaidi ya miezi sita sasa tangu Mheshimiwa Hussein Bashe, Mbunge wa Nzega Mjini, atoe ahadi ya kugharamia chakula kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Mwanzoli, hasa wale wa bweni waliopata ufaulu wa juu. Hadi leo, utekelezaji wa ahadi hiyo haujafanyika.
Ahadi hiyo ilipokewa kwa matumaini makubwa. Wazazi waliamini changamoto ya chakula kwa watoto wao imetatuliwa. Walimu walihamasika. Wanafunzi waliona dira mpya ya matumaini. Lakini mpaka sasa, ahadi hiyo imebaki hewani.
Kesho shule zinafunguliwa. Leo wazazi wamepeleka watoto wao shuleni na wanadaiwa michango ya chakula. Wengi wao wameingia katika hali ya sintofahamu, wakidhani kwamba Mheshimiwa Bashe alishachukua jukumu hilo kama alivyoahidi.
Wengine walijikakamua kutafuta nauli na mahitaji mengine wakiamini gharama ya chakula imeshughulikiwa. Lakini sasa, wanakutana na ukweli mgumu na maswali mengi yasiyo na majibu.
Je, ahadi hii ilikuwa ya kweli au ya kisiasa? Je, kuna maelezo yoyote rasmi kwa nini haijatekelezwa? Je, wanafunzi wa Mwanzoli hawana tena thamani katika macho ya waliowaahidi?
Ni muhimu kwa Mheshimiwa Bashe kutoa kauli ya wazi kwa wananchi wa Mwanzoli na Nzega kwa ujumla. Hii si hoja ya kisiasa tu, bali ni ya kijamii na kiutu.
Tunatoa wito: Toa tamko rasmi kuhusu hatma ya ahadi yako kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Mwanzoli. Watoto, wazazi na jamii nzima wanahitaji majibu.
Ahadi ni deni. Na deni kwa watoto ni deni kwa vizazi vijavyo.