JACKLINE CELESTINE KITALE
Member
- Jul 29, 2021
- 81
- 158
Habari za wakati huu wan JF. Nimekuja na kitu kingine, sio kipya ila nilikiandika kwa sehemu tu na nikaona imepata mwitikio mkubwa sana, hivyo nikaona kuwa nina wajibu wa kuandika zaidi ili kudadavua uzi wangu.
Imekuwa ni kawaida kwa watu wanapooana kwa ndugu kuja kukaa na Wana ndoa hao hasa kama wana maisha mazuri kidogo. Huwa Jambo hili linachukuliwa kirahisi sana, lakini lina uzito wake na tena uzito mkubwa sana. Na Jambo hili huweza hata kuleta mfarakano na limeshaharibu ndoa nyingi.
Baada ya muda katika ndoa, mwanaume atamleta mama yake au ndugu zake katika nyumba ambapo wana ishi na mke wake. Sikatai kwamba mwanaume asimlete mama yake nyumbani la hasha. Ila Kuna sababu ambazo zitamfanya mzazi aje aishi nyumbani kwa mwanae. Mfano mama Ni mgonjwa Sana na hana mtu wa kumuhudumia huko alipo, maisha magumu sana, au nizee sana,hawezi kujihudumia na anahitaji msaada.
Lakini kama mzazi ana nguvu, anaweza kulima (kama ni mkulima ) au kufanya kazi zake za kawaida ni makosa makubwa kuja kuishi moja kwa moja kwenye nyumba ya mwanao ambaye ameoa.
Ninasema hivi kwasababu, mzazi kama mzazi anakuwa na mtazamo na fikra za tofauti kidogo ya jinsi mwanao wa kiume anavyotakiwa kuwa katika ndoa yake , kwakuwa yeye ni baba wa nyumba. Mfano, mzazi atategemea awe anapikiwa , anafanyiwa kila kitu na mkewe, hasa zile kazi za nyumbani. Sasa unaenda kuishi pale, unakuta labda kila siku za jumapili mwanao wa kiume anapika, anafua nguo na mingineyo. Au unakuta ana vaa mavazi kama suruali, taiti na vi hot pants. Au zaidi kabisa unakuta mke hajui kupika.
Wewe kama mzazi lazima uingilie, utaona kama unatatua tatizo lakini kumbe unaharibu kabisa mahusiano yao. Nyakati hizi ni tofauti, Kuna mabadiliko mengi kutokana na tekinolojia. Na pia kabla ya kuingilia jiulize kwani kabla sijaja kuishi hapa walikuwa wanaishije, ukishagundua hayo, utakuwa umepata jibu.
Na wanawake wengi huwa hwako tayari kwa mzazi wa mume aje kuishi nyumbani na siyo kwamba hampendi mama wa mumewe hapana, ila tu wanahofia na wanajaribu kukwepa ugomvi na mipishano inayoweza kutokea. Nilimuuliza mwanamke mmoja kuhusu hili na aliniambia kitu ambacho kilinishtua kidogo.
Aliniambia kuwa mama yake husema, “hapendi kwenda kwenye nyumba ya mwana mwanawe wa kike kwasababu anakuwa hana uhuru, ila ingekuwa mwanae Ni wa kiume, ndio angejisikia Uhuru kwasababu angekuwa na nguvu”.
Haya maneno yalinishtua sana kwasababu yana ukweli Sana. Na atakama huwa haya semwi, hujidhirisha kwa vitendo. Hebu fikiria wakati manaishi na mama nyumbani, alafu ugomvi utokee kati ya mama yako na mkeo, wewe utakuwa upande wa nani?
Jibu lipo wazi kabisa ya kuwa utakuwa upande wa mama, bila hata ya kujua chanzo utakuwa upande wake tu. Na ndiyo hiki ambacho wanachokihofia na ndio maana hawako tayari, hatakama huwa hawasemi. Na wanawake wengi huwa hawasemi kuwa hawako tayari kwa hili kwasababu wanaogopa kuonekana wana roho mbaya na hawapendi wa mume.
Lakini mzazi, kama mzazi anayejielewa kama hana sababu ya muhimu, hawezi kuja kukaa kwenye nyumba ya mwanae ambaye ana mke wake. Ni makosa, kitamaduni na hata kifikra.

Upvote
2