Wazazi tunapitia magumu mno katika malezi, watoto wana mbinu ovu

Wazazi tunapitia magumu mno katika malezi, watoto wana mbinu ovu

Kama serikali ilivyoweka sheria kali kwa wabakaji wa watoto na kufungwa miaka 30. Watoto wa kiume wawekewe sheria kali zaidi ya miaka 30.
Kwanini watoto wa kiume ndiò waadhibiwe?

wanafunzi wa kike kwa tamaa zao wanaanzisha mahusiano na watu wazima, wanabeba mimba na bado wanarudi kusoma
ila wakiume ndio anaonekana muharifu anapelekwa jela

Inferiority complex bado inasumbua jamii yetu
 
Sheria inatambua kuwa mtu yoyote mwenye umri chini ya 18yrs hawezi kufanya maamuzi mwenyewe as bado hajawa mtu mzima. Hivyo tunaamini kuwa yoyote atakayefanya mapenzi na huyo mtu amemrubuni, amemlaghai na/au kumbaka. Hivyo yeye hana kosa bali yule aliyemrubuni.
 
1. Miziki pendwa mfn ya zuchu
2. Tamaa ya kumiliki vitu asivyoweza kupewa na wazazi wake
3. Vyakula pendwa vinavyosisimua mwilini
4. Kuporomoka kwa maadili
5. Media zote pendwa saizi vipindi vyake ni kujadili mpira, mziki wa kizazi kipya(zuchu) na mapenzi
6. Malezi ya mzazi mmoja
7. Simu

Hizi ni baadhi ya changamoto zinazomzunguka mtoto kipindi hiki, si kwamba ni nyingi sana la hasha ila zina uzito na msukumo mkubwa sana kwenye kubadili tabia ya mtoto na kupelekea kuharibika kitabia
 
Hali ni mbaya sana wakati huu, mtoto akishalamba asali kuja kuacha ni ngumu hata aelezwe vp labda impact ikishatokea ndio atajua madhara ya asali.
 
Mungu atasaidia.kikubwa mpe elimu ya kujitambua.
Imagine mtoto ana smartphone anaweza kujiweka porno mda wote anaangalia,juzijuzi wamefukuzwa shule Fulani wanajipiga picha za uchi na kusambaza.malezi magumu.
Niliona hiyo habari, kwa sasa kulingana na mabadiliko ya teknolojia na uhuru uliopo ni kuwaweka wazi tu wajue ila kizazi cha sasa ni korofi mno.
Mwezi wa 6 kuna binti wa darasa la 7 alimshikia kisu mama yake kwa sababu alimfokea kwa kuchelewa kurudi nyumbani. Mtoto alirudi saa 5 usiku kaletwa na boda, inasikitisha sana.
 
Hahaha pole Kwa huyo mama...hili ni balaa
 
Back
Top Bottom