Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Usafi ni moja ya nyenzo bora za mtu kuwa na afya njema. Ili mtu awe na afya bora, hana budi kuzingatia usafi wa mwili, mazingira anayoishi na anavyokula.
Usafi wa Ngozi: Pamoja na kazi nyingi, ngozi hufanya kazi ya kulinda mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa. Tunashauriwa kuzitunza ngozi za watoto wetu kwa kuwaogesha kila siku kwa maji safi ya vuguvugu na sabuni ili kuondoa vimelea vya magonjwa juu ya ngozi.
Usafi wa Kinywa: Ni vema kutunza meno ya watoto wetu kwa kuwapigisha mswaki kila siku asubuhi na ikiwezekana kila baada ya kula. Mfundishe mtoto namna ya kuswaki vizuri ili kuondoa mabaki ya chakula katikati ya meno ili kuzia meno yasioze na magonjwa ya fizi kwa watoto.
Usafi wa mikono: Wazazi tuwanawishe watoto wetu mikono kwa maji safi ya vuguvugu yanayotiririka na sabuni kila wanapotoka kucheza, kabla ya kula, baada ya kula na baada ya kutoka chooni. Ni muhimu kuwanawisha mikono yao watoto wadogo mara kwa mara.
Usafi wa matunda: Matunda yanayonunuliwa sokoni mara nyingi huwa yametoka mashambani ambapo yalikwisha pigwa madawa na pia kukusanya uchafu. Mzazi unashauriwa kusafisha matunda kwa maji safi yanayotiririka kabla ya kuyamenya na kumpa mtoto.
Usafi wa Mazingira: Mazingira safi hufaya mtoto awe na afya bora. Ili kutunza afya za watoto kwa kuwaepusha na magonjwa ya ngozi kama vile upele na mba, mzazi unashauriwa kufanya usafi wa mazingira wa mahali ambapo mtoto hupendelela kucheza na mahali anapolala.