Ukiona manyoya, .............Sawa.
Kwann umeanzisha huu uzi leo mpenzi, nini kimekusibu?!
Kuna jamaa alimpiga mwalimu na kichwa kwenye paji la uso na kupelekea yule mwalimu kupasukaMaana mtetezi wa mtoto ni mtu mzkma kwakuwa mtoto hawezi kujitetea mwenyewe bali anakuwa inferiority pale anapokutana na adhabu za walimu wasiojua maadili yao ama wasiofuata utaratibu wa kisheria wa adhabu.
Shida walimu wengi ni failure sasa hawajui maana ya muongozo/waraka wa elimu juu ya adhabu. Pia hata codes of ethics za ualimu hawazijui.
Siku nikikuta mwalimu anatoa adhabu kinyjme na utaratibu ni moja kwa moja na deal nae kisheria kukomesha uonevu kwa watoto wasio na hatia.
Safi sana mkuu. Kuna kisa kimetokea Nigeria amepost Mercy Johnson kimeniuma ndo nikapata muda wa kuandika hii kitu. Yani mashuleni watt wanafanyiwa ndivyo sivyo na huyo mtoto amekufa kwa maumivu makubwaa alipigwa na wenzie kisa amekataa kujiunga na kikundi chao. You know what? Walimu wameficha hiyo kitu wanasema ameumia wakati anacheza mpira. Wakati huo huo baadhi ya wazazi wa watoto washukiwa waliofanya hivyo wamehamishwa shule fasta wamepelekwa nje ya nchi.Umeongea point kubwa na muhimu sana hakika wewe ni mzazi bora. Hiyo ndiyo njia niifanyayo mimi pia. Hapa wengine watapita kimya kimya kwasababu hawana muda wa kuwafuatilia watoto wao hata wakirudi wamepigwa na walimu wakavimba uso mzazi ndo wa kwanza kumwambia mtoto "wewe ni mtundu ndo maana umepigwa"
Sasa kama mzazi anakuwa mkatili kwa maanae unadhani mtoto hata akifanyiwa jambo baya atamweleza mzazi? Lahasha.
Niliwahi kuwakuta walimu kama watatu wanawaadhibu wanafunzi pasipo utaratibu nikaenda kwa mwalkmu mkuu kumweleza kama anajua watoto wanaadhibiwa hovyo akashangaa akaniuliza wapi. Nikamwambia twende pale nje akawakuta walimu wanawadhibu watoto akawaita ofisini akawaandikisha barua za maelezo hadi leo nikipita mle hakuna ujinga huo na huwa nawauliza wanafunzi mara kwa mara.
Kwakuwa kitaaluma mimi ni mwanasheria nipo tayari kumshitaki mwalimu yeyote asiyefuata mwongozo/waraka wa adhabu kwa wanafunzi ambapo anayepaswa kumwadhibu mwanafunzi ni mkuu wa shule tu ama ampe idhini ya maandishi mwalimu mwingine kutoa adhabu hiyo tena kwa idadi ya viboko visivyozidi vitatu kwa kosa kubwa.
For sure. Ila hapa ni malezi sasa ya pande zote wazazi tufanye jitihada kulea wtt wetu vzr nyumbani na walimu pia watusaidie huko shuleKuna jamaa alimpiga mwalimu na kichwa kwenye paji la uso na kupelekea yule mwalimu kupasuka
Mwalimu hakukubari akampeleka yule mwanafunzi police akaona haitoshi hasira akaziamishia kwa wanafunzi woote
Jamaa alianza kutafuta visababu vya kijinga mara nata notes za vipindi vyote kama huna anakularua kama anaua Nyoka ili kupoza machungu
Yule jamaa aliempeleka police naye alifukuzwa Shule yaani haya Maisha usione mtu kakosa Elimu unamlaumu watu wanapitia masahibu mengi
Pole sana mkuuMe nilifanyiwa ukatili mkubwa Sana baada ya kuanza halakati za kudai haki Elimu, kitendo kilichopelekea Headmistress kunihisi ni watu wa usalama na kuanza kuniona Adui mkubwa,
Me nimtu wakupuuzia vitu hasa kama sijatenda Mimi sasa kukaa kwangu kimya Kumbe wenzangu wananiwinda ili kunifukuzisha Shule ili nyoyo zao zifurahi, mbaya zaidi Kuna baba mmoja alienda kwa Afsa Elimu kumueleza madhaifu ya Mwalimu mkuu basi walimu wakajua moja kwa moja ni Mimi
Mambo yakawa moto walimu woote wakawa hawataki hata kuniona Darasa nililokuwepo wakalisusa ikawa tunakaa Hadi week bila kusoma kisa Mimi kuwa mnoko jamani wakati sijui chochote wala sihusiki na Chochote
Niliishi maisha Magumu Sana pale shule Soo hayo ndiyo yalinikuta nikiwa shule ingawa yapo mengi ila nimejaribu kusamulize.
Kabisa kabisa mkuu.Hili ni tatizo sana kiukweli, hizi shule kwa sasa zimekuwa biashara sana kuliko kuangalia na kutunza hawa watoto tunaowapelekea....
Mishahara kwa walimu ni midogo na hailipwi kwa wakati pamoja na wazazi kulipa ada kubwa.
Wafanyakazi wengine kama wafanya usafi, madereva nk hawalipwi vizuri na wanamaisha magumu mpaka inasikitisha..
Hayo yote yanashusha hali ya ufanyajikazi na matokeo yake uangalizi wa watoto unakuwa mdogo shuleni na maeneo yanayozunguka shule.
Mfumo wa kuajili wafanyakazi kwenye hizi shule unapaswa kuwekewa utaratibu mzuri ili kulinda watoto kwenye hizi shule..
Serikali inapaswa kufanya controlling kwenye hizi shule kwa kuwa na watu maalum wanaofanya ziara za mara kwa mara kujua mienendo ya kila siku....kama itatokea ukiukwaji wowote wa maadili na nidhamu mbovu kwenye shule hizi adhabu yake iwe kuubwa sana na mtoto yoyote aliyefanyiwa udhalilishaji shule husika ilipe fidia kubwa sana...