Mohammed wa 5
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,215
- 3,035
Mtu mmoja aliniuliza kitu gani miongoni mwa vitu ambavyo najutia maishani..nilimjibu kitu fulani lakini leo napenda kujibu hapa kushare na wengine labda inaweza kusaidia kubadili mitazamo yetu kuhusu maisha.
Binafsi najutia tabia yangu fulani ya utotoni...tabia yangu na ya baadhi ya rafiki zangu wakati huo...sawa ilikuwa ni utoto lakini haikuwa sawa na kwa sasa kila nikifikiria kuna matone ya machozi huwa yananitoka, tabia ya kuwadharau na kuwacheka wanafunzi waliokuwa dhaifu kimavazi na kihali darasani.
Kila wakati moyo wangu unawaomba samahani ingawa ni miaka mingi imepita na sijawaona tena. Mwalimu angeweza kusema "Wewe mbona mchafu? Mbona haujafua?"...wote tunacheka huku mimi nikiwa kiongozi wa wachekaji.
Kumbe kosa sio la mwenzetu. Kumbe labda Baba yake hakuwa na uwezo hata wa kununua sabuni anachapwa, analia na wote tunamkejeli. Rafiki yangu mwingine analala muda mwingi darasani kumbe njaa inamsumbua kwa sababu kwao hajala.
Hawana chakula. Mwalimu anaingia anamkuta kalala katika dawati anamchapa na sisi tunashangilia. Haikuwa sawa. Mwenzetu mwingine anachapwa pia kwa kulala kumbe amechoka kwa sababu nyumbani anafanya kazi ngumu ambazo kwetu alikuwa anafanya Houseboy. Haikuwa sawa. Kila ninapokumbuka kwa sasa nafsi yangu huwa inaumia.
Kwa sasa nimejikita katika kuwaelimisha wanangu kuwa watoto wema kwa wenzao. Kuheshimu utu, kuamini katika kazi ya Mungu na kusambaza upendo bila ya kiburi na majivuno. Nikiwanunulia watoto wangu biskuti na Ice Cream nawasisitizia pia kuwagawia watoto wa majirani ambao Baba zao hawana uwezo wa kununua.
Mwanangu akiwa anaendesha Baiskeli namwambia ampe mtoto wa jirani pia aiendeshe. Hakuna tunachopoteza. Mungu ndiye anayetugawia riziki na anatugawia sio kwa ajili ya kuwadharau ambao hajawapatia.
Maisha ni fumbo.