Wazazi wa sasa na kizazi chao

Wazazi wa sasa na kizazi chao

papag

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,352
Reaction score
2,036
Habari wazazi wa kipindi hichi cha zama za tekelinalokujia. Siku hizi mtoto si wa jumuia kama enzi zetu. Popote utakapo kutwa na mzazi yeyote waweza tumwa au kuadhibiwa. Ila kizazi hichi thubutu uone rangi za wazazi.

Sasa hivi ukimfungia mtoto ndani kwenye mageti ni SHIDA na pia ukimuacha huko nje pia ni SHIDA.
KWA SABABU KILA MZAZI ANAANGALIA KIZAZI CHAKE TU NA KUTAFUTA MALI .HATA FAMILIA HAZITEMBELEANI MPAKA MKUTANE KWENYE HARUSI AU MISIBA.

"LA MWISHO NA MUHIMU NI KWAMBA MMEACHA MILA NA DESTURI ZA BABU ZENU"
angalia vizuri mtaani kwenu utapata jibu.
Tchao
 
Kila mtu ana parenting style yake. Ukiona mtoto anafanya madudu mtaani, wewe pita hivi, mind your own business kulinda amani yako!
 
Kuna walimu watafikishwa mahakamani si muda mrefu baada ya kumchapa bakora mwanafunzi wao mpaka akafa.Ishi kama hauoni kitu na wala haukereki.
 
Sijajua umelelewa wapi ila hata zamani yangu jirani alikua hawezi kumuadhibu mtoto si wake, tena kua makini na wala sio sifa, mtoto ambaye si wako hujui changamoto zake, unamuadhibu anakauka unaenda kufia jela,

Kila mtu alinde kizazi chake mbona ni rahisi sana.
 
Km wewe ni kizazi cha 90s ni sawa kuwa na mawazo kama hayo yako. Na ninaya heshimu. Ila kwa sisi wa 70s na 80s mambo yalikuwa tofauti kabisa. Unauliza nimekuulia wapi. Jibu nimekulia na kuzaliwa Daresalamaa
 
Kila mtu ana parenting style yake. Ukiona mtoto anafanya madudu mtaani, wewe pita hivi, mind your own business kulinda amani yako!
Sikatai kabisa. Ila zamani haikuwa hivi mkuu. Now ukiwafungia ni shida ukiwaachia pia ni shida
 
Back
Top Bottom