KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Wazazi wakiafrika ni kama mmezubaa sana, mfumo wa uchumi ni zaidi ya kumsomesha mtoto na angojee ajira!.
Kuna jitihada fulani lazima zifanyike pia ndani ya familia kuhusu watoto wako na maswala ya uchumi.
kutokupata elimu ya uchumi walau kwa uchache inapelekea vijana waingie kwenye vitu vya hovyo ama pia kuchelewa kufikia malengo yake!. unakuta mtu bado ni limbukeni wa pesa mtu anafanikiwa kupata pesa leo kesho yote kwisha huku haijafanya kitu chochote!, Nafasi ya kumfundisha mtoto kuhusu uchumi ianzie ngazi ya familia tuache mchezo.
Mtu anajipata akianza kuingiza mshahara tu hata wa laki tano basi anajiona amemaliza!, pombe, shisha na starehe za kila namna huyu atakuja kufika nafasi yake ya mafanikio lini..?
starehe sio tabu, tabu starehe inatakiwa unaitumia pesa ambayo hata ikitoka haileti tafrani!.
Baba kafanikiwa kwa baishara akifa leo familia inayumba kwasababu hakuna hata mtu mmoja anaejua mzee alikuwa anapita njia zipi kufanikisha biashara yake iwe kwenye mafanikio!. Ndio maana kwenye jamii yetu zinaibuka nadharia za hovyo mara uchawi watu wanahisi wameshikiliwa nyota zao kumbe ni elimu tu ya uchumi kidogo ndo haipo!.
Mtu hata kujinyima mwezi mmoja ili afanikishe jambo fulani anashindwa!, unakuta mtoto anakuja kujufunza haya tayari ameshaingia kwenye mfumo na amejitengenezea majukumu ambayo hawezi kuyaruka na kipato chake bado kichanga!.
Kuna uhusiano mkubwa sana hapa pesa anazoanza kuzalisha mtoto wako na vitu atakavyoanza kutumia!.
Vilevile kuhusu mahusiano sio swala la kukurupukia!, tunajua ni ugumu kiasi gani kupambana na mihemko ya kihisia pale mtu anapopevuka lakini hilo sio sababu yakukosa elimu ya ujinsia!.
Mahusiano yanachanganya sana vijana, inaathiri mpaka maswala yao ya uchumi!.. waambieni ukweli ukifanya hivi kitatokea hichi maswala yakuoneana aibu yaishe maisha yanataka umakini, Ukute mzazi hujawahi hata kukaa na mwanao kumfundisha kuhusu me na ke unategemea aje ajifunze kwenye jamii ambayo nayo haijafunza watoto wao!!.
Siwezi kuwafundisha muwafundishe vipi kila mtu ananjia zake na welevu wake lakini zingatieni Mahusiano na Uchumi ni vitu basics mwanao kuvijua.