Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wazazi wawili Yohana Josephat (40) na Lucia Michael (30) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu baada ya kuwajeruhi watoto wao kwa kuwachoma na moto sehemu mbalimbali za mwilini baada ya kuwatuhumu kuiba mahindi debe moja.
Watuhumiwa ni Wakazi wa Kijiji cha Yitwimilaa, Kata ya Kiloleli, Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wanadaiwa kutenda kosa hilo Julai 29, 2022.
Watoto ambao wanatuhumiwa kuiba mahindi hayo nyumbani kwa bibi yao wana umri wa miaka 14 na 13 walipata msaada kutoka kwa raia wema ambao waliwapelekea Kituo cha Afya cha Nassa wnakopatiwa matibabu mpaka sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda amesema watuhumiwa watafikishwa Mahakamani muda wowote upelelezi ukikamilika.
Ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kuzuia matukio ya ukatili dhidi ya Watoto, na kuwa hatua zitachukuliwa.