Wazazi wakanyeni watoto wenu,mtawazika kwa kujihusisha na ujambazi

Wazazi wakanyeni watoto wenu,mtawazika kwa kujihusisha na ujambazi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Jana nilipitia taarifa ya Jeshi la Polisi Dar kuhusu ujambazi na kukamatwa kwa majambazi. Lakini leo nimeambiwa kuna vijana wanashiba bangi wanajipanga hadharani kwenda kuiba huku mchana kutwa wakiwa kwenye bar na vijiwe vya bangi wakibugia vilevi. Niwaomba wazazi, msiwalazimishe Polisi wakawasaidia kulea maana wakiamua kuwalea watoto tutawazika wengi.

Polisi ya Leo si Polisi ya miaka ya nyuma, watu wanakuchoma kwa RPC kupitia namba zilizotolewa hivi karibuni. Mzazi unayemtakia mema mwanao mkanye. Jirani unayecheka naye ndiye mlinzi wa amani wa serikali tusiendelee kuamini kwamba maisha yatasonga tu kwa kupiga tukio na kujificha. Simu za camera zinatumika sana kufichua waalifu, mkanye mwanao.

Nayasema haya kwa sababu nafahamu kijana kabetuliwa kwenye tukio juzi kati kanda ya ziwa baada yakutunishiana misuli na dola. Pls walindeni ndugu zenu kwa kuwachoma kwenye vyombo vya dola lakini pia kuwakanya
 
Kuna vibaka/wadokozi/wakabaji na Majambazi yenye mashine. Wewe unazungumzia kundi lipi?
 
Ila umesahau kua polisi pia ni jambazi mwenye kibali..Week iloyopita nimerushiwa risasi mbili na polisi wa kitanzania wapo kwenye gari la private, pona yangu ni God never allowed me to touched with f*kn bullet na pia kupata akili ya kusimama kwenye kijiji chenye pilika pilika muda ule, cha ajabu hawakusimama niliwatambua kua ni polisi kwenye next barrier na bado mikwara mingi wakanipga..OF course nilikua na change ya cash ka million 6, nilitoka kununua mashamba njia ya kigamboni 80km from ferry. Bado suala lipo kituoni. ILA NJAA ZA MAAFISA POLISI ZINATUMALIZA PIA.
 
Kama hao watoto wapo kama ulivyowaelezea hapa, ni kazi bure kwa wazazi kufanya chochote juu yao!
 
Tumechoka majambazi uchwara...police piga kanyaga twende.....mkiwaounguza kama 100 hivi tutatulia mtaani
 
Kuwe na jukwaa la mapolice humu tuwe tunawatonya tonya kila saa.
 
Back
Top Bottom