Wazazi wakataa sadaka ya kuchinja iliyotolewa na Waarabu, wakidai watoto wao watatolewa kafara

Wazazi wakataa sadaka ya kuchinja iliyotolewa na Waarabu, wakidai watoto wao watatolewa kafara

Wajinga tu

Pigine wali nyama nyie ujinga uwatoke

Huko makwenu mnawalisha wanennu ugali maharage ndio maana wana akili duni
 
Wajinga tu

Pigine wali nyama nyie ujinga uwatoke

Huko makwenu mnawalisha wanennu ugali maharage ndio maana wana akili duni
Wameombwa msaada wajenge ukuta wa shule, nyama kila mtu atakula kwake.
Ila africa Kuna mijitu mijinga sana, Yani unatoa msaada wa nyama? Ukila unaenda chooni kuitoa? Kwa nini wasijenge ukuta au madarasa yatayodumu miaka mingi?
 
Wazazi katika shule ya msingi Baraa iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha,wamekataa sadaka ya kuchinja ,Mbuzi , Kondoo na Ng'ombe zipatazo 135 zilizotolewa msaada Kwa ajili ya kitoweo cha nyama Kwa wanafunzi wa shule hiyo ,wakidai msaada huo unalenga kuwatoa kafara watoto wao.

Msaada huo ambao ulikuwa utolewe tangu ijumaa ya wiki iliyopita na taasisi ya dini ya kiislamu ya Khair Elkhaleej company LTD ya nchini Misri,ulizua taharuki Katika shule hiyo baada ya wazazi hao kushuhudia Lori lililokuwa limebeba Mbuzi ,Kondoo,Ng'ombe na magunia ya mchele Kwa ajili ya kuwapikia chakula wanafunzi hao .

Wakiongea katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda ,katika shule hiyo baadhi ya wazazi hao,Monica Meja , Ibrahim Mollel na Godface Godwin walimweleza mkuu huyo wa wilaya ya kwamba hawahitaji msaada huo kwani wamekuwa na hofu juu ya msaada huo kuwa watoto wao kudhulika .

"Sisi wazazi tumekuwa na wasiwasi baada ya kuambiwa kuwa kuna mifugo inakuja kuchinjwa hapa shuleni Kwa ajili ya kitoweo kwa wanafunzi ,jambo hili tulipaswa tujulishwe mapema maana hatuna uhakika wa afya za watoto wetu "alisema Monica Meja.

Naye Mzazi mwingine, Godface Godwin alisema suala la kiimani linahitahi ufafanuzi mkubwa Kwa sababu wanaotoa msaada wanaimani yao na sisi hapa tunaimani yetu ndio maana tunahofu na msaada wao ukizingatia kwamba wanyama watakaochinjwa watahitaji kuombewa.

Naye Ibrahim Mollel ambaye ni Mzazi na mwananchi wa kata ya Baraa aliitaka.taasisi hiyo kuubadilisha msaada huo badala.ya kutoa sadaka ya nyama badala yake wajenge ukuta kuzunguka shule hiyo.

"Mheshimiwa mkuu wa wilaya sisi kama wazazi tumekuwa na hofu juu ya msaada huo wa nyama Kwa watoto wetu unaotokewa na wahisani ,tunawaomba wakabadilisha hii sadaka watujengee uzio katika shule yetu,wauze hiyo mifugo Kwa sababu watoto wetu wakija kula wakazulika itakuwa shida sana''alisema

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Said Mtanda aliwatoa hofu wananchi hao Kwa kuwaeleza kwamba wasiwe na wasiwasi Kwa sababu amejiridhisha pasipo shaka kwamba msaada huo ni salama na hauna hofu na maisha ya watu.

Mtanda aliwasihi wananchi hao kupokea msaada huo hao shuleni kwa ajili ya chakula Cha watoto wao kwani ameelekeza mifugo hiyo ichinjwe katika machinjio ya halmashauri na serikali ndio itagawa hizo nyama katika shule zilizoelekezwa za jiji la Arusha.

"Kwa sababu mmekuwa na mashala na msaada huu, mimi sijaja hapa kuwalazimisha mpokee Ila kama hamtaki basi, utaelekezwa Kwa wengine wenye uhitaji Ila suala la kuchangia chakula shuleni ni lazima "alisema Mtanda.

Aidha aliongeza Kwa kutoa maelekezo Kwa wazazi wasiotaka kuchangia wakamatwe na kufikishwa kituo Cha polisi.

Mwakilishi wa Taasisi ya Khair Elkhaleej company LTD hapa nchini ,Jamar Waziri alisema taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa msaada katika nchi mbalimbali kupitia mashule.

Alisema taratibu zao ni kununua mifugo na kuitoka sadaka ya nyama kwenye shule mbalimbali na katika shule za jiji la Arusha walipanga kuchinja mbuzi na Kondoo zipatazo135 ,Ng'ombe,mchele kilo 400,mafuta na Kuni Kwa wanafunzi zaidi ya 2000 katika shule ya Baraa

"Wananchi wamekuwa na hofu wakifikiria watoto wao wanakuja kutolewa kafara na baadhi ya wazazi wakajikuta wakizuia watoto wao wasije shuleni "alisema

Alifafanua kwamba taasisi yao makao yake makuu yapi Egpty nchini Misri na imekuwa ikijohusisha kutoa misaada katika matawi yake ikiwemo Nchi ya Tanzania na Malawi.

Naye Diwani wa kata ya Baraa,Jacob Mollel alisema kuwa msaada huo ulifika katika Kata yake ijumaa iliyopita lakini aliamuru kusitishwa baada ya wazazi kuibuka mashala na msaada huo.


Akiongea katika kikao hicho Leo alisema baadhi ya wazazi wameelimishwa na kukubali kupokea msaada huo laikini baadhi yao bado wanamashaka jambo ambalo aliwasihi wazazi hao kuondoa shaka juu ya wahisani hao kwani wamekubali pia kusaidia katika nyanja mbalimbali za maendeleo katika shule hiyo.

Ends.....

Wangepeleka kwenye shule za kiislamu au taaisi za dini ya kiislamu zenye uhitaji ili kuondoa utata

Otherwise ni wazo zuri kubadilisha hao mifugo kuwa pesa na wajenge ukuta au wanunue vifaa va kuwafundishia watoto
 
Changieni chakula cha wanafunzi sasa.
Kwani siku zote watoto wameishije? Wapo sahihi. Bora wangesema misaada ila unapewa sadaka. Unajua wamenenea nini? Hata mimi ninhekataza wanangu kila hiyo. Sadaka huwa inaendana na madhabahu. Unataka unganisha watu na majini ya kiarabu alafu unalazimisha. Kama wana nia ya dhati wangetoa pesa watoto wanunuliwe chakula sio kondoo, mbuzi na ngamia. Niliona Morogoro hiyo, watu wameshtuka hawataki ungamanishwa na mapepo.
 
Hiki kitu hata Mimi sijakielewa, ni msaada au ni sadaka?

Kama ni msaada lazima ulenge mahitaji ya wahusika, je nyama ndio hitaji Lao hapo shuleni? Hawana changamoto zinazowakabili?

Kama ni sadaka huwa imebeba maagano fulani ya kiroho, hao wanaopelekewa sadaka wameshirikishwa kikamilifu kwenye hayo maagano ya iyo sadaka?
 
Safi sana wazazi endeleeni kukataa misaada ya hawa makabachori..leo hii wanajifanya na huruma na sisi wakati waliua na kutesa babu na bibi zetu...tangu lini mwarabu akampenda mwafrika kama sio kuna kitu wanatafuta kwa maslahi yao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom