Wazazi wakataa sadaka ya kuchinja iliyotolewa na Waarabu, wakidai watoto wao watatolewa kafara

Wazazi katika shule ya msingi Baraa iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha, wamekataa sadaka ya kuchinja, Mbuzi, Kondoo na Ng'ombe zipatazo 135 zilizotolewa msaada Kwa ajili ya kitoweo cha nyama Kwa wanafunzi wa shule hiyo, wakidai msaada huo unalenga kuwatoa kafara watoto wao.

Msaada huo ambao ulikuwa utolewe tangu Ijumaa ya wiki iliyopita na taasisi ya dini ya kiislamu ya Khair Elkhaleej company LTD ya nchini Misri,ulizua taharuki Katika shule hiyo baada ya wazazi hao kushuhudia Lori lililokuwa limebeba Mbuzi ,Kondoo,Ng'ombe na magunia ya mchele Kwa ajili ya kuwapikia chakula wanafunzi hao .

Wakiongea katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda ,katika shule hiyo baadhi ya wazazi hao,Monica Meja , Ibrahim Mollel na Godface Godwin walimweleza mkuu huyo wa wilaya ya kwamba hawahitaji msaada huo kwani wamekuwa na hofu juu ya msaada huo kuwa watoto wao kudhulika .

"Sisi wazazi tumekuwa na wasiwasi baada ya kuambiwa kuwa kuna mifugo inakuja kuchinjwa hapa shuleni Kwa ajili ya kitoweo kwa wanafunzi ,jambo hili tulipaswa tujulishwe mapema maana hatuna uhakika wa afya za watoto wetu "alisema Monica Meja.

Naye Mzazi mwingine, Godface Godwin alisema suala la kiimani linahitahi ufafanuzi mkubwa Kwa sababu wanaotoa msaada wanaimani yao na sisi hapa tunaimani yetu ndio maana tunahofu na msaada wao ukizingatia kwamba wanyama watakaochinjwa watahitaji kuombewa.

Naye Ibrahim Mollel ambaye ni Mzazi na mwananchi wa kata ya Baraa aliitaka.taasisi hiyo kuubadilisha msaada huo badala.ya kutoa sadaka ya nyama badala yake wajenge ukuta kuzunguka shule hiyo.

"Mheshimiwa mkuu wa wilaya sisi kama wazazi tumekuwa na hofu juu ya msaada huo wa nyama Kwa watoto wetu unaotokewa na wahisani ,tunawaomba wakabadilisha hii sadaka watujengee uzio katika shule yetu,wauze hiyo mifugo Kwa sababu watoto wetu wakija kula wakazulika itakuwa shida sana''alisema

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Said Mtanda aliwatoa hofu wananchi hao Kwa kuwaeleza kwamba wasiwe na wasiwasi Kwa sababu amejiridhisha pasipo shaka kwamba msaada huo ni salama na hauna hofu na maisha ya watu.

Mtanda aliwasihi wananchi hao kupokea msaada huo hao shuleni kwa ajili ya chakula Cha watoto wao kwani ameelekeza mifugo hiyo ichinjwe katika machinjio ya halmashauri na serikali ndio itagawa hizo nyama katika shule zilizoelekezwa za jiji la Arusha.

"Kwa sababu mmekuwa na mashala na msaada huu, mimi sijaja hapa kuwalazimisha mpokee Ila kama hamtaki basi, utaelekezwa Kwa wengine wenye uhitaji Ila suala la kuchangia chakula shuleni ni lazima "alisema Mtanda.

Aidha aliongeza Kwa kutoa maelekezo Kwa wazazi wasiotaka kuchangia wakamatwe na kufikishwa kituo Cha polisi.

Mwakilishi wa Taasisi ya Khair Elkhaleej company LTD hapa nchini ,Jamar Waziri alisema taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa msaada katika nchi mbalimbali kupitia mashule.

Alisema taratibu zao ni kununua mifugo na kuitoka sadaka ya nyama kwenye shule mbalimbali na katika shule za jiji la Arusha walipanga kuchinja mbuzi na Kondoo zipatazo135 ,Ng'ombe,mchele kilo 400,mafuta na Kuni Kwa wanafunzi zaidi ya 2000 katika shule ya Baraa

"Wananchi wamekuwa na hofu wakifikiria watoto wao wanakuja kutolewa kafara na baadhi ya wazazi wakajikuta wakizuia watoto wao wasije shuleni "alisema

Alifafanua kwamba taasisi yao makao yake makuu yapi Egpty nchini Misri na imekuwa ikijohusisha kutoa misaada katika matawi yake ikiwemo Nchi ya Tanzania na Malawi.

Naye Diwani wa kata ya Baraa,Jacob Mollel alisema kuwa msaada huo ulifika katika Kata yake ijumaa iliyopita lakini aliamuru kusitishwa baada ya wazazi kuibuka mashala na msaada huo.

Akiongea katika kikao hicho Leo alisema baadhi ya wazazi wameelimishwa na kukubali kupokea msaada huo laikini baadhi yao bado wanamashaka jambo ambalo aliwasihi wazazi hao kuondoa shaka juu ya wahisani hao kwani wamekubali pia kusaidia katika nyanja mbalimbali za maendeleo katika shule hiyo.

Ends.....

Kwanini msaada uje na makando kando ya dini?kwa nini waseme sadaka ya kuchinjwa!!!? Huu msaada ungetolewa Mtwara,Lindi,au Zenj,Wala hakuna shida jamii za huko ambazo ni waislam wengi,Wala zisingetaharuki,maana kwa imani ya dini zao ibada za kuchinja zipo.
Arusha ni mji wa kikristo zaidi,Hawa wa misri Wana ajenda ya Siri.
 
Hii habari Ina upotoshaji mkubwa sana. Mwandishi alizingatia kupotosha uma, na hakueleza ukweli.
Itoshe kusema baadhi ya waandishi habari wa Arusha wanaendekeza njaa ndogo ndogo, wanapaswa kujirekebisha.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Alisema taratibu zao ni kununua mifugo na kuitoka sadaka ya nyama kwenye shule mbalimbali
Nadhani tatizo lipo hapa " sadaka ya nyama". Imekaa ki-kafara kafara kwa sisi wenye imani zetu
 
Wazazi katika shule ya msingi Baraa iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha, wamekataa sadaka ya kuchinja, Mbuzi, Kondoo na Ng'ombe zipatazo 135 zilizotolewa msaada Kwa ajili ya kitoweo cha nyama Kwa wanafunzi wa shule hiyo, wakidai msaada huo unalenga kuwatoa kafara watoto wao.

Msaada huo ambao ulikuwa utolewe tangu Ijumaa ya wiki iliyopita na taasisi ya dini ya kiislamu ya Khair Elkhaleej company LTD ya nchini Misri,ulizua taharuki Katika shule hiyo baada ya wazazi hao kushuhudia Lori lililokuwa limebeba Mbuzi ,Kondoo,Ng'ombe na magunia ya mchele Kwa ajili ya kuwapikia chakula wanafunzi hao .

Wakiongea katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda ,katika shule hiyo baadhi ya wazazi hao,Monica Meja , Ibrahim Mollel na Godface Godwin walimweleza mkuu huyo wa wilaya ya kwamba hawahitaji msaada huo kwani wamekuwa na hofu juu ya msaada huo kuwa watoto wao kudhulika .

"Sisi wazazi tumekuwa na wasiwasi baada ya kuambiwa kuwa kuna mifugo inakuja kuchinjwa hapa shuleni Kwa ajili ya kitoweo kwa wanafunzi ,jambo hili tulipaswa tujulishwe mapema maana hatuna uhakika wa afya za watoto wetu "alisema Monica Meja.

Naye Mzazi mwingine, Godface Godwin alisema suala la kiimani linahitahi ufafanuzi mkubwa Kwa sababu wanaotoa msaada wanaimani yao na sisi hapa tunaimani yetu ndio maana tunahofu na msaada wao ukizingatia kwamba wanyama watakaochinjwa watahitaji kuombewa.

Naye Ibrahim Mollel ambaye ni Mzazi na mwananchi wa kata ya Baraa aliitaka.taasisi hiyo kuubadilisha msaada huo badala.ya kutoa sadaka ya nyama badala yake wajenge ukuta kuzunguka shule hiyo.

"Mheshimiwa mkuu wa wilaya sisi kama wazazi tumekuwa na hofu juu ya msaada huo wa nyama Kwa watoto wetu unaotokewa na wahisani ,tunawaomba wakabadilisha hii sadaka watujengee uzio katika shule yetu,wauze hiyo mifugo Kwa sababu watoto wetu wakija kula wakazulika itakuwa shida sana''alisema

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Said Mtanda aliwatoa hofu wananchi hao Kwa kuwaeleza kwamba wasiwe na wasiwasi Kwa sababu amejiridhisha pasipo shaka kwamba msaada huo ni salama na hauna hofu na maisha ya watu.

Mtanda aliwasihi wananchi hao kupokea msaada huo hao shuleni kwa ajili ya chakula Cha watoto wao kwani ameelekeza mifugo hiyo ichinjwe katika machinjio ya halmashauri na serikali ndio itagawa hizo nyama katika shule zilizoelekezwa za jiji la Arusha.

"Kwa sababu mmekuwa na mashala na msaada huu, mimi sijaja hapa kuwalazimisha mpokee Ila kama hamtaki basi, utaelekezwa Kwa wengine wenye uhitaji Ila suala la kuchangia chakula shuleni ni lazima "alisema Mtanda.

Aidha aliongeza Kwa kutoa maelekezo Kwa wazazi wasiotaka kuchangia wakamatwe na kufikishwa kituo Cha polisi.

Mwakilishi wa Taasisi ya Khair Elkhaleej company LTD hapa nchini ,Jamar Waziri alisema taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa msaada katika nchi mbalimbali kupitia mashule.

Alisema taratibu zao ni kununua mifugo na kuitoka sadaka ya nyama kwenye shule mbalimbali na katika shule za jiji la Arusha walipanga kuchinja mbuzi na Kondoo zipatazo135 ,Ng'ombe,mchele kilo 400,mafuta na Kuni Kwa wanafunzi zaidi ya 2000 katika shule ya Baraa

"Wananchi wamekuwa na hofu wakifikiria watoto wao wanakuja kutolewa kafara na baadhi ya wazazi wakajikuta wakizuia watoto wao wasije shuleni "alisema

Alifafanua kwamba taasisi yao makao yake makuu yapi Egpty nchini Misri na imekuwa ikijohusisha kutoa misaada katika matawi yake ikiwemo Nchi ya Tanzania na Malawi.

Naye Diwani wa kata ya Baraa,Jacob Mollel alisema kuwa msaada huo ulifika katika Kata yake ijumaa iliyopita lakini aliamuru kusitishwa baada ya wazazi kuibuka mashala na msaada huo.

Akiongea katika kikao hicho Leo alisema baadhi ya wazazi wameelimishwa na kukubali kupokea msaada huo laikini baadhi yao bado wanamashaka jambo ambalo aliwasihi wazazi hao kuondoa shaka juu ya wahisani hao kwani wamekubali pia kusaidia katika nyanja mbalimbali za maendeleo katika shule hiyo.

Ends.....

Mwelekezeni alete Dodoma huku yaani utachotaje maji kisimani ukaweke Baharini? Halafu utegemee bahari ikushukuru!!!
 
Nyie mnadhani waarabu/waisilamu ni kama ninyi mnaotoana makafara kisa utajiri ee,,, baba anamtoa kafara mwanae kisa utajiri kwa maagizo ya mganga akili iyo!!!!, huo ni ujinga na ulimbukeni. Waarabu wanaakili bwana, na uisilamu ndiyo umewafikisha hapo, hivyo wanajuwa wanachokifanya. Nyie endeleeni kuuwana, bila kumsahau mchungaji wenu aliewauza huko moshi kawaachia mafuta ya upako muuwane wenyewe kwa wenyewe jamaa akasepa mammae.

وَلَنْ تَرْضَىٰ عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ
Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.
Acha jazba ndugu yangu, relax.

Ukipelekwa vitani front line unaweza kuuza nchi kwa kusababisha friendly attack.
Jipe muda kidogo usome vizuri nilicho andika.

Mimi mwenyewe nakiri moyoni na kutamka kwa ulimi kwamba

"Laaa ilaaha il la (A)llah, Muhammadan Rasuulullah" halafu unanipeleka kwa Mwamposa.
Au ndio wale "maostadh" (feki) wanaowabashiria wenzao Moto?
 
Nisamehe sana ustadhi wangu Makwega,,,nimekusoma. Allah akujaze kheri
 
Kwanini msaada uje na makando kando ya dini?kwa nini waseme sadaka ya kuchinjwa!!!? Huu msaada ungetolewa Mtwara,Lindi,au Zenj,Wala hakuna shida jamii za huko ambazo ni waislam wengi,Wala zisingetaharuki,maana kwa imani ya dini zao ibada za kuchinja zipo.
Arusha ni mji wa kikristo zaidi,Hawa wa misri Wana ajenda ya Siri.

Mnachekesha na kujiaibisha 😁 ungelijuwa Tanzania ina waislamu wengi kuliko wakristo wala usingeongea haya. Pwani yote waislamu ni wengi kuliko wakristo, kwanzia dar, tanga na pwani yote kwa ujumla waislamu ni wengi. Kanda ya ziwa, Shinyanga, bukoba na Mwanza pia kuna waislamu wengi, labda vijijini huko bado bado wako kwenye sehemu ya ujinga kwa maana still hawakuuona ukweli.

Ukija kanda ya magharibi, Tabora, kigoma ina waislamu wengi sana

Ukija Singida ni balaa, waislamu ni wengi sana

Huko machame nackia waislamu ni wengi mno, ndugu yangu katika imani ata2pa ukweli maana ni mtu wa huko machame kimsboy

Znz ndiyo ucseme asilimia zaidi ya 90% ni waislamu

Kwa hesabu ya haraka, waislamu ni zaidi ya asilimia 70%, wakifuatiwa na wakristu, kisha wapagani.

Hapo tatizo ni Waarabu tu. Parception ya watanzania wengi kwa waarabu ni negative.

Kweli kabisa, hapo tatizo ni waarabu,,,wangelikuwa wale makafiri wenzao wa ulaya wasingelalamika na kutokwa povu kiac hicho. Mungu awabariki sana waarabu, tuko nyuma yao kwa lolote dhidi ya hao wanaoupiga vita uislamu.
 
Hawa watu weupe bwana, wao wanaendeleza sadaka za kuchinja lakini sisi tukifanya matambiko yetu kwa kuchinja wanaita ni ushirikina.

Kumbuka ibada zote za kiislam na kikristu zilikuwa ni matambiko ya kijadi ya mababu zao na hata ukisoma hadidhi ya abraham kumtoa sadaka mwanaye kwenye vitabu vyote biblia na quran utaliona hilo.

Wao wameua matambiko yetu hasa watu wa kanisa na waislamu lakini ya kwao bado wanaendeleza

Usile nyama ya tambiko kama wewe sii muusika wa lile tambiko utabeba malaana na mabalaa yawatu. Yanahama kwao nyanahamia kwako
 
Ni mawazo na mitazamo Yao kuhusu hofu ya kuitumia sadaka wasioshiriki kuiandaa kuwa ni chakula kwa watoto wao. Ilipaswa kutolewa ufafanuzi mzuri kwa wanafunzi na wazazi wakaridhika, kwani mtu ni utu!
 
Ikumbukwe kuwa Wazungu wa Marekani pia wameshatoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya lishe mashuleni......

Hapo napo watazuka watu wa kudai hao ni Freemasons, wengine watasema hivyo vyakula vinaharibu akili za watoto!

Wakiambiwa kuchanga watoto wao wale wanasema eti, 'walimu watakula' hatuwezi kuchanga!

Watoto wanakaa na njaa kutwa mzima. Wakifeli walimu hawafanyi kazi!

Afrika is shit hole!
Chakula cha siku moja kitawafanya wafaulu?
 
Hawa watu weupe bwana, wao wanaendeleza sadaka za kuchinja lakini sisi tukifanya matambiko yetu kwa kuchinja wanaita ni ushirikina.

Kumbuka ibada zote za kiislam na kikristu zilikuwa ni matambiko ya kijadi ya mababu zao na hata ukisoma hadidhi ya abraham kumtoa sadaka mwanaye kwenye vitabu vyote biblia na quran utaliona hilo.

Wao wameua matambiko yetu hasa watu wa kanisa na waislamu lakini ya kwao bado wanaendeleza

Usile nyama ya tambiko kama wewe sii muusika wa lile tambiko utabeba malaana na mabalaa yawatu. Yanahama kwao nyanahamia kwako

Muisilamu gani mjinga ale minyamafu!!!! Hata wakristo wengi tu hawali nyamafu, mpaka achinje muisilamu ndiyo wanakulla.
 
Back
Top Bottom