Wazazi wakikulilia shida wasaidie

Wazazi wakikulilia shida wasaidie

kwenda21

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Posts
3,423
Reaction score
3,414
Jamani please wazazi wakikulilia shida wasaidie hasa mama, siku nne zilizopita bimkubwa alifululiza kunipinga mizinga, juzi nikamkaushia, nikamwambia sina, ukweli nilikuwa nayo, nikaondoka zangu kwenda kwangu, kufika home nikasikia kunguru wanalia sana nyuma ya nyumba, kwenda kucheki kulikuwa na kenge.

Dah nikaokota jiwe kumpiga nalo, jiwe likaenda moja kwa moja kwenye kioo cha dirisha bwaaa kikavunjika, natoka kurudi kulikuwa na pipe ya maji sijui niliikanyaga, ikapasuka ikabidi nimuite fundi akala 15000, kioo 60000 zikanitoka, faster nikaenda kumtumia mother hela yaishe.
 
Ni ajabu mtu unakuwa mgumu kutoa hadi kwa wazazi wako na uwezo unao. Kuna muda natamani nifanye kitu zaidi kwa wazazi wangu ila uwezo.

Uzuri wa wazazi hata ukitoa kidogo ulichojaaliwa wanapokea kwa moyo wa upendo na kuzidi kukuombea.

Kutoa ni moyo sio utajiri.
 
Ni ajabu mtu unakua mgumu kutoa hadi kwa wazazi wako na uwezo unao. Kuna mda natamani nifanye kitu zaidi kwa wazazi wangu ila uwezo.
Uzuri wa wazazi hata ukitoa kidogo ulichojaaliwa wanapokea kwa moyo wa upendo na kuzidi kukuombea.

Kutoa ni moyo sio utajiri.
Si unajua shetani huwa anaingiaga, huwa natoa mkuu
 
Saidia ila sio kwa kupitiliza

Kuna wazazi unampa hela nae huko aliko anakuwa boss anaanza kutoa kwa ndugu zake tena wasio hata na shukurani,wakipata shida wanamkimbilia nae anakuomba wewe
 
Kutokumtumia mzazi hela na hayo yaliyotokea havihusiani, ni coincidence tu.

By the way saidia wazazi wanapokuwa na uhitaji na ukiwa na uwezo wa kufanya hivyo bila wewe mwenyewe kuathirika.
Vinahusiano mkubwa sana,nitakuambia kitu kwanini we misiba inatokeaga mingi sana lakini ile hali ya kulia haikujii,lakini ukitokea around ndugu zako au wazazi unaumia sana, ni ile nguvu iliyopo
 
Ni ajabu mtu unakuwa mgumu kutoa hadi kwa wazazi wako na uwezo unao. Kuna muda natamani nifanye kitu zaidi kwa wazazi wangu ila uwezo.

Uzuri wa wazazi hata ukitoa kidogo ulichojaaliwa wanapokea kwa moyo wa upendo na kuzidi kukuombea.

Kutoa ni moyo sio utajiri.

Michepuko inakupiga Hela, na Wala haikuombdi , Tena wanakuuliza, unataka nije huko sijaenda Saluni?

Tuwapende sana Wazazi wetu.
 
Yaani Mama/Mzazi kuhitaji kitu kwako unaita Mzinga!?
 
Duh, unaanzaje kuona ubahili kumpa mama yako pesa?

Mzazi hapaswi hata kukuomba inapaswa umfikirie kabla na kama wewe unacho hapaswi kukosa kabisa
 
Jamani please wazazi wakikulilia shida wasaidie hasa mama, siku nne zilizopita bimkubwa alifululiza kunipinga mizinga, juzi nikamkaushia, nikamwambia sina, ukweli nilikuwa nayo, nikaondoka zangu kwenda kwangu, kufika home nikasikia kunguru wanalia sana nyuma ya nyumba, kwenda kucheki kulikuwa na kenge.

Dah nikaokota jiwe kumpiga nalo, jiwe likaenda moja kwa moja kwenye kioo cha dirisha bwaaa kikavunjika, natoka kurudi kulikuwa na pipe ya maji sijui niliikanyaga, ikapasuka ikabidi nimuite fundi akala 15000, kioo 60000 zikanitoka, faster nikaenda kumtumia mother hela yaishe.
Usisubiri mpaka uliliwe shida. Jua mahitaji yao na wawe na akiba kidogo.
 
Back
Top Bottom