Wazazi wakikulilia shida wasaidie

Wazazi wakikulilia shida wasaidie

Wengine hatuna hao wazazi wa kuwapa hela,
Saidieni wazazi wenu inapobidi inawapa confidence na kuwaongezea siku za kuishi.
Unajisikiaje anaposema anajembe lake.
 
Jamani please wazazi wakikulilia shida wasaidie hasa mama, siku nne zilizopita bimkubwa alifululiza kunipinga mizinga, juzi nikamkaushia, nikamwambia sina, ukweli nilikuwa nayo, nikaondoka zangu kwenda kwangu, kufika home nikasikia kunguru wanalia sana nyuma ya nyumba, kwenda kucheki kulikuwa na kenge.

Dah nikaokota jiwe kumpiga nalo, jiwe likaenda moja kwa moja kwenye kioo cha dirisha bwaaa kikavunjika, natoka kurudi kulikuwa na pipe ya maji sijui niliikanyaga, ikapasuka ikabidi nimuite fundi akala 15000, kioo 60000 zikanitoka, faster nikaenda kumtumia mother hela yaishe.
Tusaidie wazazi, baraka zao muhimu sana kwenye maisha ya watoto wao. Haijalishi unasaidia mara ngapi Kwa mzazi.
FB_IMG_16780461197599321.jpg
 
Mzazi inabidi uweke utaratibu wa kumpa kiasi fulani kila mwezi sio usubiri vinga,kama mambo madogo madogo hata laki au hamsini kila mwezi
 
Back
Top Bottom