BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Umri wa wale ambao wamezaliwa kuanzia miaka ya 90 kurudi nyuma, kufika hadi miaka ya 80 na kuendelea huko nyuma, matukio ya mzazi kumpiga mtoto kama vile anapiga mwizi anaekamatwa mtaani ilikuwa ni kawaida.
Yaani ilikuwa mzazi akikukamata kukupa kichapo ilikuwa ni kichapo hevi kinomanoma, hiyo iliwaambukiza Walimu shuleni. Ilikuwa kawaida kuoana mwalimu akitoa kipigo cha nguvu na wanafunzi wakazoea.
Miaka ya nyuma ilikuwa ni kawaida kusikia zile stori za mwanafunzi anaenda ofisini kwa walimu anakula stiki kwa walimu zaidi ya 10, na akitoka hapo fresh tu, sijui ndio tulikuwa wametujengea usugu!
Zama zimebadilika, sasa hivi wazazi wengi wanalea watoto kama mayai kama vile likianguka tu linapasuka, ndivyo ilivyo kwa watoto wa kipindi hiki.
Hali hiyo ndiyo ipo kwa walimu, nao wanalazimika kuishi na wanafunzi vilevile dunia inavyotaka.
Sisemi kama ila ya zamani ndio ilikuwa sawa au ya sasa ndio sawa, lakini niwape angalizo tu wale wenzangu na mimi ambao bado tunaamini ili mtoto akuelewe, lazima umpige kama ngoma.
Zama zimebadilika watoto wenyewe hawa mayaimayai, inabidi kama ni adhabu ya kumchapa iwe ya wastani, tuache tabia ya kupiga mtoto.