Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.

Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.

Kama kawaida huyo kaka alikuja na mshenga wake pamoja na mjomba wake. Baba yangu alialika wenzake kama 6 hivi ili kujadiliana mahari. Kwa kweli ilikuwa tafrani, kwasababu baba yangu mzazi alishauriana na wenzake mahali iwe 10.5M kitu ambacho kilinishangaza sana.

Mjomba wake akasema hiyo hela hawana kwani hawanunui kiwanja. Baadae mjomba akasema wao wanaweza toa 2.5M baba akasema iongezeke japo 3M kwa shingo upande, kwamba hataki mahari ndogo akidai watakuja wengine.

Jioni yake akaniita mimi na mama akaanza kunifokea. Akaniambia mimi namdhalilisha kuleta mtu masikini na haeleweki kwa hiyo niachane naye, na nisipoachana naye mimi nitakuwa siyo mtoto wake na nikikubali kuolewa naye nisije kukanyaga kwake mpaka kaburi lake nisije kulisogelea.

Hakuishia hapo akaanza kunilinganisha na kabati ambalo anadai limenizidi, kwamba yeye alilinunua kwa bei kubwa kuliko mahali yangu. Nililia sana maana hata mama yangu alikuwa upande wa baba kwa hiyo sikuwa na support yoyote.

Aibu naipata mimi mtaani, naogopa hata kutoka kwenda sehemu kwa ajili ya wazazi wangu kunisambazia doa kubwa.

Naombeni ushauri katika huu wakati mgumu, kushauriwa kumuacha mtu uliyependana naye mkaendana siyo kitu rahisi. Japo huyo kaka hajaonesha dalili zozote za kuniacha, anawasiliana na mimi kama kawaida.

Ahsanteni sana. Napitia maoni yenu, wote nawakaribisha.

Tafuta another adult, au ndugu yeyote apokee mahari, nenda kaishi na mumeo.
 
Upagani ni mwingi sana kwenye harusi za kikristo. Dini ya kiislam ndo dini pekee ambayo suala la mahari limeachiwa kwa mwanamke kuamua anaolowa kwa mahari ya shilingi ngapi.

Ni hivi bi dada amua kwa moyo wako kwenda kwa jamaa muishi kama mume na mke ni imani yangu wazazi wako hawatakaa kukutafuta wewe ila wataamua kumtafuta jamaa apeleke hata debe la pombe ya kienyeji waongeee.

Mahari million 10 aseee unanunua kiwanja au?
 
Jamaa akubali kutoa hiyo 5, atanguize hiyo 2.5M alafu awaambie zingine zitakuja baadae mkijijenga kifamilia.

Mwoane mkazae mahari hulipwa pole pole na siyo biashara ya kuuza mtu. Ila kama vile baba yako amekuuza so be careful kwa wakwe watakuona umewasababishia umaskini kwa mahari ndefu ya kihistoria.

Be humble hili nalo litapita
 
Hapo sijui .

Kwa maana naushaidi upo baba yangu alimkataa mtu maskini dada yangu alikuwa na hela nyingi tu akamua waoane weeh si yule kaka akamua baba kishirikina ili asimkwaze nandoa yake.

Ndoa ya dada haikudumu yule kaka alishindwa kuendelea naye wakachana ila yule kaka alikuwa anatamaa na mali za dada akatuwekea ndumba ili tusipendwe na dada akawa ni yeye na familia yake.
Ndio wanapewa attention na zile pesa ilifikia mpaka walitaka kumuua ni maombi tu yalimrudisha katika hali yakawaida .

Yangu mama alikuwa hataki kila mwanaume niliyemleta home basi ikaws niko single wa leo so ndio hayo kuna kitu kimoja .

Ukiona baba hamtaki mtu sio mama ni baba achana naye .

Mimi ni hayo tu
 
Nenda kamuoe mchumbaako hyo ataendelea kuwa baba yako habadiliki...halafu anataka mtu tajiri je tajiri anakutaka ww? Ukimsikiza babako maisha yako yatakua magumu sana
Point unayomshauri wewe ni ipi hapo?

Umesema "aende akamuoe mchumba" wakati wa kuolewa ni yeye!
 
Mwanasulwa lady

Kumbuka si wazazi wako wanaenda kuishi na huyo mchumba? Wazazi wana mipaka yao na hawapaswi kuwakwaza watoto. Mungu pekee ni mwenye kubariki ndoa. Fanya maamuzi magumu na muamini Mungu atakuwa na wewe, mwanadamu leo wapo kesho hawapo.

Amtumainiaye Bwana ni kama mlima Sayuni, hatatikisika milele. 🙏
 
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.

Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.

Kama kawaida huyo kaka alikuja na mshenga wake pamoja na mjomba wake. Baba yangu alialika wenzake kama 6 hivi ili kujadiliana mahari. Kwa kweli ilikuwa tafrani, kwasababu baba yangu mzazi alishauriana na wenzake mahali iwe 10.5M kitu ambacho kilinishangaza sana.

Mjomba wake akasema hiyo hela hawana kwani hawanunui kiwanja. Baadae mjomba akasema wao wanaweza toa 2.5M baba akasema iongezeke japo 3M kwa shingo upande, kwamba hataki mahari ndogo akidai watakuja wengine.

Jioni yake akaniita mimi na mama akaanza kunifokea. Akaniambia mimi namdhalilisha kuleta mtu masikini na haeleweki kwa hiyo niachane naye, na nisipoachana naye mimi nitakuwa siyo mtoto wake na nikikubali kuolewa naye nisije kukanyaga kwake mpaka kaburi lake nisije kulisogelea.

Hakuishia hapo akaanza kunilinganisha na kabati ambalo anadai limenizidi, kwamba yeye alilinunua kwa bei kubwa kuliko mahali yangu. Nililia sana maana hata mama yangu alikuwa upande wa baba kwa hiyo sikuwa na support yoyote.

Aibu naipata mimi mtaani, naogopa hata kutoka kwenda sehemu kwa ajili ya wazazi wangu kunisambazia doa kubwa.

Naombeni ushauri katika huu wakati mgumu, kushauriwa kumuacha mtu uliyependana naye mkaendana siyo kitu rahisi. Japo huyo kaka hajaonesha dalili zozote za kuniacha, anawasiliana na mimi kama kawaida.

Ahsanteni sana. Napitia maoni yenu, wote nawakaribisha.
Mzazi wako ni "pasua kichwa" na ni dhaifu.

Yawezekana hilo genge la washauri lilimpotosha ili asifanikiwe kufanya hilo tukio la heshima na kheri.

Ujue, jambo jema likiisha kuwekewa mabango lazima lipate dosari, hasa mambo yahusuyo ndoa shetwani kivuruge huwaga hachezi mbali.

Waweza kushangaa hata mtu wako wa karibu kuweza kutia ushauri potoshi ama kukuwekea pingamizi la fitina kabisa!

Yaani mzazi wako anashindwa kupokea mahari yenye tofauti ya hesabu ndogo namna hiyo kweli!

Mbona harusi nyingi karibu kona zote nchini kwa sasa millioni2, millioni3 ndiyo bei halisi?

Kwa kuwa wewe ni mtoto na yeye ni mzazi, weka msimamo usioweza ukawaletea bifu kati yako na yeye.

Piga mgomo baridi wa kimya kimya kwa jambo lolote usilolitaka.

Olewa na mchumba umpendaye na si wa kuchaguliwa na mtu yeyote, sababu wewe ndiye utakayeenda kuishi naye na si wao.

Huo ndiyo uwe msimamo wako.

Wakikuletea mtu hata kama ana ukwasi kiasi gani kama Musk, kama si chaguo lako mkatae.

Kiwango kilichobakia kutimiza hesabu, mshawishi mchumba wako akapambane atimize na kukileta, na umsubiri kwa kipindi chote hicho kutimiza ndoto yenu.

Ikishindikana mama, tulizana ili huyo mzee aendelee kukutunza, maana waswahili wanasema mtoto wa kike hakui nyumbani kwao.

Ninatumaini mwisho wa siku mzazi wako atabadili mawazo.

Matokeo ya kukomalia maamuzi yasiyokuwa na tija, mwisho wake huwa ni mbaya.
 
Duuh Ml 10 aisee sasa mzee amezidisha io ni tamaa tu,wazee wengine tamaa zitatupeleka wapi utafikiri kiwanja kinanunuliwa.
 
Wewe umekuja kuomba ushauri au kufanya criticism kwa hoja zinazotolewa, nimefuatilia replies zako tu nimegundua hata huyo jamaa anayetaka kukuoa pengine kaingia cha kike, una kaujeuri fulani pengine pia umerithi toka kwa wazazi, who knows

Mzee wako ana akili sana, pengine alishajua uko na huyo jamaa yako ambaye unadai mnapendana na mmebanduana wee kwa mwaka na nusu, lakini ni mtu ambaye siyo level ya familia yenu, hivyo kutamka hiyo mahari ni kumfukuza tu huyo mwenza wako wa mwaka na nusu ili asiongeze tegemezi kwenye familia yake kitu ambacho kwa upande mwingine ni sahihi,

Kila mtu aishi kulingana na level zake, kwann yeye anataka kumuongezea mzee wako mzigo maana hata wewe mwenyewe unakiri jamaa bado hajasimama, na pengine na familia yake na yenu haziendani, unahis hata akikuoa hatokua na inferiority complex dhidi ya familia yako na kuhisi anaonewa kwa kila jambo litakalokua linaenda against nayeye,

Ndoa siyo kuvaa shela na kupiga picha na marafiki, Acha mbwembwe dogo, huko kusoma kusikutie jeuri,

Vijana wenyewe siku hizi wanataka kuoa kwenye familia zisizo tegemezi(maisha tight), itakua huyo kuja kwenu ili mzee aanze kutoboka pesa za mtaji, kwan mzee yeye hana akili[emoji1]

kama hutojali ningependa kujua huyo ni mwanaume wako wa ngapi toka puberty, pengine tunashauri wageni wa League(mwanaume wako wa kwanza) au timu zinazokaribia kushuka daraja(age go)
Chief wewe ukikwama unaweza kwenda kulia shida ukweni?

Kama ni hapana basi hata huyo mwamba hawezi kuwa mzigo ukweni hata siku moja labda awe hajielewi yeye ni nani katika familia yake aliyoianzisha na majukumu yake kama mume.

Besides wangapi wanaolewa kwa mahari kidogo na wanaenda vizuri hadi uzeeni? Mfano mzuri ni wengi kati ya wazazi wetu.

Mtoa mada ana haki ya kuhoji au kutoa maoni katika mjadala huu unaomhusu na sio kukubali kwa kila ushauri.

Sijaona ujeuri wa mtoa mada ila nimeona uelewa, udadisi na kujiamini kitu ambacho sio dhambi.
 
Haya mambo,

KUSOMESHA KWA GHARAMA.
Ndio amesomesha kwa sababu ni mwanae alitaka nani amsomeshee?

KAKULEA KWA GHARAMA.
Again alitaka nani alee mwanae?

Na mengine mengi yote sio sawa. Kwa nini sijawahi sikia kuwa mzazi kamwambia mwanae wa kiume kuwa nimekulea na kukusomesha kwa gharama sasa huoi hadi unirudishie gharama zangu kwanza ndio ukaanzishe familia yako???
Hizi mahari ni utamaduni tu wa kuziunganisha zile familia mbili iwe ni moja kubwa zaidi. Haikupaswa kuwa kitega uchumi.

10 millions haina thamani kuliko utu na kwa kukumbushana tu ni hakuna ajuae kesho.
Wenda huyo kijana masikini leo akaja isaidia hiyo familia kesho.

Unless kuna yaliyo nyuma ya pazia basi mzee kazingua sana.
 
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.

Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.

Kama kawaida huyo kaka alikuja na mshenga wake pamoja na mjomba wake. Baba yangu alialika wenzake kama 6 hivi ili kujadiliana mahari. Kwa kweli ilikuwa tafrani, kwasababu baba yangu mzazi alishauriana na wenzake mahali iwe 10.5M kitu ambacho kilinishangaza sana.

Mjomba wake akasema hiyo hela hawana kwani hawanunui kiwanja. Baadae mjomba akasema wao wanaweza toa 2.5M baba akasema iongezeke japo 3M kwa shingo upande, kwamba hataki mahari ndogo akidai watakuja wengine.

Jioni yake akaniita mimi na mama akaanza kunifokea. Akaniambia mimi namdhalilisha kuleta mtu masikini na haeleweki kwa hiyo niachane naye, na nisipoachana naye mimi nitakuwa siyo mtoto wake na nikikubali kuolewa naye nisije kukanyaga kwake mpaka kaburi lake nisije kulisogelea.

Hakuishia hapo akaanza kunilinganisha na kabati ambalo anadai limenizidi, kwamba yeye alilinunua kwa bei kubwa kuliko mahali yangu. Nililia sana maana hata mama yangu alikuwa upande wa baba kwa hiyo sikuwa na support yoyote.

Aibu naipata mimi mtaani, naogopa hata kutoka kwenda sehemu kwa ajili ya wazazi wangu kunisambazia doa kubwa.

Naombeni ushauri katika huu wakati mgumu, kushauriwa kumuacha mtu uliyependana naye mkaendana siyo kitu rahisi. Japo huyo kaka hajaonesha dalili zozote za kuniacha, anawasiliana na mimi kama kawaida.

Ahsanteni sana. Napitia maoni yenu, wote nawakaribisha.
Peleka mimba nyumbani,watakuozesha hata bure
 
Unamwita kaka Kwa vile hamjafanya mpaka baada ya ndoa au?!
Na je wazazi wako wanajua hauna bikra ya kulipwa maharibuote hiyo!?
Na je unaelimu gani !?
 
Mie ushauri wangu stick na upande wa baba mzazi. Utachukuliwaje kwa bei ya kabati bwana🤣🤣🤣🤣

Halafu ngoja nikupe siri, masuperwoman hawaolewi. Wanaoolewa ni wanawake wenye njaa
Hahaha... bei ya kabati
 
Inategemea, je kama mdingi kasomesha mtoto wake ist? Acheni utani bwana mtoto anaondokaje nyumbani kwa bei ya kabati🤣🤣🤣🤣
Ungejua wenye pesa ndo hata hawanaga hayo mambo ya mahari za kukomoana..
 
Back
Top Bottom