kwa io imeandikwa baba akuchagulie mume..Kama huna ushauri tulia
Nionyeshe ni wapi iliandikwa baba anaweza kukutafutia mume..Tumieni vizur maandiko sio kupotosha watu
Wewe umekuja kuomba ushauri au kufanya criticism kwa hoja zinazotolewa, nimefuatilia replies zako tu nimegundua hata huyo jamaa anayetaka kukuoa pengine kaingia cha kike, una kaujeuri fulani pengine pia umerithi toka kwa wazazi, who knows
Mzee wako ana akili sana, pengine alishajua uko na huyo jamaa yako ambaye unadai mnapendana na mmebanduana wee kwa mwaka na nusu, lakini ni mtu ambaye siyo level ya familia yenu, hivyo kutamka hiyo mahari ni kumfukuza tu huyo mwenza wako wa mwaka na nusu ili asiongeze tegemezi kwenye familia yake kitu ambacho kwa upande mwingine ni sahihi,
Kila mtu aishi kulingana na level zake, kwann yeye anataka kumuongezea mzee wako mzigo maana hata wewe mwenyewe unakiri jamaa bado hajasimama, na pengine na familia yake na yenu haziendani, unahis hata akikuoa hatokua na inferiority complex dhidi ya familia yako na kuhisi anaonewa kwa kila jambo litakalokua linaenda against nayeye,
Ndoa siyo kuvaa shela na kupiga picha na marafiki, Acha mbwembwe dogo, huko kusoma kusikutie jeuri,
Vijana wenyewe siku hizi wanataka kuoa kwenye familia zisizo tegemezi(maisha tight), itakua huyo kuja kwenu ili mzee aanze kutoboka pesa za mtaji, kwan mzee yeye hana akili[emoji1]
kama hutojali ningependa kujua huyo ni mwanaume wako wa ngapi toka puberty, pengine tunashauri wageni wa League(mwanaume wako wa kwanza) au timu zinazokaribia kushuka daraja(age go)