Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Kuna mama yangu mlezi yupo sehemu ana watoto sita wa kike wameolewa wote na hajawahi kupokea mahari ya mwanaume hata buku na kawapa baraka zote wanae na wako top kimafankio ktk ndoa zao.

Huyo mzee wako mwambie kabla hajafa, hajaumbika na asilete Umungu mtu na inaonekana hata mlango wa kanisa/msikiti haujui na km ana mali basi hata kwenu wawili Mungu wa kweli atawabariki mzipate.
 
Baba yako anakosea sana kwenye hilo.
Kama alitaka wewe upate mume tajiri angekujengea mazingira ya wewe kuolewa na tajiri.

I mean angekusomesha shule za mataji na pia asinge kuweka katika mazingira ya kukutana na sie masikini.
Yaan ungekua unakupereka kwenye safari zake za kukutana na majiri wenzake na kwenye shughuli za matajiri wenzake.

Kwani uko ndo ungekutana na matajiri anaowataka.

But kama wewe ni wakujichanganya na kila mtu akubaliane na matoke ya wewe kuolewa na yeyote.
 
Wazazi wa mama ako wangeamua kama baba ako alivyoamua hapo wewe usingekuwepo, baba ako hana utajiri halafu unataka utajiri kupitia mahari 🤮
 
Wanaosema kupokea mahali ndogo ni ushamba wabaki hivyohivyo,

Mahali ndogo huchukui Binti yangu kwanza ni kipimo Utaweza kumlisha huko unapompeleka?

Ni IPO hivyo hata kwetu wazee wangu na shangazi zangu hawataki mba mba mba kama huna Hela kajipange tu.
So nilete bei gani ili nikutwae mkuu...???
 
Uyo Mzee wako anaonekana ni mtu wakutafuta show off kwa wenzake ,na jamii Nina mzazi wangu mmoja anavitabia vya namna iyo...,nani aliyesema mzazi hakosei ,mzazi anakosea Sana Tena Sana nasanyingine kuvuka mipaka ...
 
Kaoe kulingana na level zako,unaenda kuoa kwa watu wenye uwezo na wews huna unategemea nini?

Hata mimi sitokubali niletewe maskini na nimeona familia nyingi zinawakataa watu wa hivyo na kuwaponda..

Mwisho wa siku mwanaume anatakiwa kuwa msaada sio mzigo.
Mwanaume anatakiwa kua msaada kwa nani? Na sio mzigo kwa nani?
 
Nenda kamuoe mchumbaako hyo ataendelea kuwa baba yako habadiliki...halafu anataka mtu tajiri je tajiri anakutaka ww? Ukimsikiza babako maisha yako yatakua magumu sana
Mkuu dada atueleze je wazazi wake ni wana utajiri wa kiwango gani ?
 
Inategemea, je kama mdingi kasomesha mtoto wake ist? Acheni utani bwana mtoto anaondokaje nyumbani kwa bei ya kabati[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwaiyo mkuu inaonekana mzee anataka binti yake aondoke kwa bei ya Jeep na siyo kwa bei ya kabati [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mzee wetu wa ukoo(mchaga)...alifukuza vijana kama wa 4 waliokuja na vi mahari vyao vya uchwara...
Binti yake alimsomesha Russia akahitimu udaktari bingwa wa kichwa(ubongo)
Mzee wa ukoo alikua anataka mahari si chini ya mil 12 na zaidi.
Mmoja wapo akajifanya mwamba akampa ujauzito ili iwe nyepesi[emoji23]...mzee presha na sukari ikapanda
Baada ya kujifungua yule mtoto akaitwa jina la babu yake..kuanzia jina la mwanzo lakati na la mwisho yotee upande wetu...
Mwamba akaenda kufungua kesi...kesi (ikaendaa)..sijui ikwaje mzee akashinda[emoji2]
Sasahizi binti yupo(wanaishi) denmkark na alishaolewa na mwanaume mwengine ambae ni (mshozi) ila dogo yupo(kabaki) kwa babu yake""
("Mzee alikua anasema alitumia pesa nyingi sana kumsomesha uko nje so hataki mahari ya ajabu ajabu"

""DADA kama unajiona una iyo thaman ya mil 10 basi tulia...watakuja tuu wenye uwo uwezo""
Kweli watakuja tu sasa hivi nchi imefunguliwa vijana wenye milioni kumi hawa kosekanai
 
Kwaiyo mkuu inaonekana mzee anataka binti yake aondoke kwa bei ya Jeep na siyo kwa bei ya kabati [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ata mie sikubali mtoto wangu aondoke kwa bei ya kabati.
 
huyo babaako aache akili za kivuta bangi, mwanaume utaishi nae wewe sasa yeye anatia kauzibe ya nini? mahari 10m kwamba anakuuza au? wazazi kama hao ndio hua wanafanya wanaume wanakua na hasira hadi wanaua wake zao kwa kosa dogo tuu... mwambie ameniudhi sana.
Binti yake atakuwa bikira
 
Milioni 10 ananunua ng'ombe Kwamba ataenda kukamua maziwa 😂
 
Back
Top Bottom