Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Wazazi wamkataa mchumba wangu kisa mahari ni ndogo

Mwambie jamaa akutoroshe akupangie sehemu ubebe mimba yake na ugome kabisa kurudi kwenu ikwezekana ubadilishe na namba zako za simu.

Baada ya muda wazazi wako watapata uchungu wa uzazi watakuja kukuomba msamaha na kurudisha mahusiano na wewe.
Wala haina haja ya kumtorosha kama ni mtu mzima anasepa tu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] baba yako anatafta pensheni kwenye mgongo wako na akiendelea ww kitie kitumbua mchanga mkose wote. M10 labda kama nina mashamba uje kulima hela irudi.

Bbaa yako ni mshamba kawaida familia zikitaka kuungana hakuna haja ya kutangaza dau kubwa kama ndio mnataka kuponea hapo kuna maisha after ndoa.
Nina ndugu yangu alipewa mke bureeeee zaidi alitoa blanket la babu na mbuzi wa sherehe basi hakutajiwa dau wala idadi ya wanyama
 
Nina rafiki yangu alikwenda kuoa wakataka 2mil,jamaa akajivuta mpaka 1.5 lakini wakakataa kabisa wao wanataka 2m.

Jamaa yangu alichofanya akalipa 1.5ml,harafu 500k akawaeleza siku ya kufunga ndoa asubuhi watamalizia,akijua kwamba ikifika siku hiyo wale wazee atawaambia hana hela hivyo na kufanya ndoa ifungwe kwa ile 1.5ml.

Ilipofika siku ya harusi ila kitu kimeandaliwa wale wazee cha kwanza wakata pesa,ndio ndoa ifungwe kama haina ndoa haifungwi,ikabidi watu wachangishane fedha ilipwe ili ndoa ifungwe.

Baada ya tukio la ndoa kuisha,yule jamaa aliwanyoosha wale wazazi hata wakiomba buku jamaa anawajibu nalipa deni la kai tano [emoji1] [emoji1787] [emoji23] maana alikopa kwa riba.

Wazazi kama hao baada ya siku kadhaa wanaomba hela za kulimia,Shenzi kabisa
 
Daah wazee walizinguaa sanaa...[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hao mnaowaoa kwa mahari ya milioni 10 tunawala bure.
mzee ameweka shida zake kwenye mahari yako.
 
Nina rafiki yangu alikwenda kuoa wakataka 2mil,jamaa akajivuta mpaka 1.5 lakini wakakataa kabisa wao wanataka 2m.

Jamaa yangu alichofanya akalipa 1.5ml,harafu 500k akawaeleza siku ya kufunga ndoa asubuhi watamalizia,akijua kwamba ikifika siku hiyo wale wazee atawaambia hana hela hivyo na kufanya ndoa ifungwe kwa ile 1.5ml.

Ilipofika siku ya harusi ila kitu kimeandaliwa wale wazee cha kwanza wakata pesa,ndio ndoa ifungwe kama haina ndoa haifungwi,ikabidi watu wachangishane fedha ilipwe ili ndoa ifungwe.

Baada ya tukio la ndoa kuisha,yule jamaa aliwanyoosha wale wazazi hata wakiomba buku jamaa anawajibu nalipa deni la kai tano [emoji1] [emoji1787] [emoji23] maana alikopa kwa riba.

Wazazi kama hao baada ya siku kadhaa wanaomba hela za kulimia,Shenzi kabisa

Heee hao wazazi walikua wapi kutafta pesa
 
Mchawi ni mshenga ningekua ni mimi ningekubari mapema hiyo ml 10 Ila kuitoa ingekuwa kipengele wakati huo nipo na mtoto wao naendelea kula maisha

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Sioi mwanamke kwa mahari zaidi ya 400K never labda huko baadae niwe n mihela mingi ila mahari kizidi 400K nasema sina uwezonayo wakizingua namchana manzi kula njia yako nile njia yangu
 
Habari zenu wana JF,

Bila kuwachosha naenda moja kwa moja kwenye point. Nilikuwa na mchumba wangu tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa. Kwa hiyo mwaka huu huyo kaka nilimwambia aje home kujitambulisha, akasema haina shida.

Niliwataarifu wazazi wangu tarehe ambayo aliniambia anakuja wakasema aje kwetu.

Kama kawaida huyo kaka alikuja na mshenga wake pamoja na mjomba wake. Baba yangu alialika wenzake kama 6 hivi ili kujadiliana mahari. Kwa kweli ilikuwa tafrani, kwasababu baba yangu mzazi alishauriana na wenzake mahali iwe 10.5M kitu ambacho kilinishangaza sana.

Mjomba wake akasema hiyo hela hawana kwani hawanunui kiwanja. Baadae mjomba akasema wao wanaweza toa 2.5M baba akasema iongezeke japo 3M kwa shingo upande, kwamba hataki mahari ndogo akidai watakuja wengine.

Jioni yake akaniita mimi na mama akaanza kunifokea. Akaniambia mimi namdhalilisha kuleta mtu masikini na haeleweki kwa hiyo niachane naye, na nisipoachana naye mimi nitakuwa siyo mtoto wake na nikikubali kuolewa naye nisije kukanyaga kwake mpaka kaburi lake nisije kulisogelea.

Hakuishia hapo akaanza kunilinganisha na kabati ambalo anadai limenizidi, kwamba yeye alilinunua kwa bei kubwa kuliko mahali yangu. Nililia sana maana hata mama yangu alikuwa upande wa baba kwa hiyo sikuwa na support yoyote.

Aibu naipata mimi mtaani, naogopa hata kutoka kwenda sehemu kwa ajili ya wazazi wangu kunisambazia doa kubwa.

Naombeni ushauri katika huu wakati mgumu, kushauriwa kumuacha mtu uliyependana naye mkaendana siyo kitu rahisi. Japo huyo kaka hajaonesha dalili zozote za kuniacha, anawasiliana na mimi kama kawaida.

Ahsanteni sana. Napitia maoni yenu, wote nawakaribisha.
Pole sana kwa yote yaliyokusibu.
 
Back
Top Bottom