Habari wanajamvi,
Kwa muda sasa kuna jambo limekua linaniumiza na nimekosa pa kuliongelea kwa uhuru ila naamini humu nitapata hekima na busara zangu.
Kama ilivyo ndoto ya kila mzazi anaesomesha mtoto ni ili mtoto ajisimamie na awe msaada kwa wazazi na nduguze baadae. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu nimesomeshwa vizuri na nimepata kazi nzuri ambau=yo imeniwezesha kufanya makubwa kwetu ikiwemo kumaliza ujenzi wa nyumba ya wazazi , kuwakatia bima na kuhakikisha wanapata matumizi yao ya kila mwezi kwa kifupi wanaishi maisha comfortable.
Wakati huo pia na mimi kama binti najiendeleza kimaisha maana tayari nina familia japo mwezangu palitokea mgogoro tukatengena.
Shida ipo hivi: Tangu nimeachana na mwenzangu ( kiukweli hakuna aneingia kwenye ndoa achane japo matatizo mengine hayavumiliki) ni kama wazazi wangu ni kitu walichokua wanakitaka maana wana access na mimi na wana nicontrol kama wanavyotaka jambo ambalo kwangu halijakaa sawa kuwaambia siwezi ila mimi pia kama mtu mwenye mji wangu kuna mambo ambayo naamini nimeyavuka nje ya control ya wazazi.
Kwa mfano bi mkubwa akija kwangu bila kuuliza ataingia kabatini na kuvaa nguo zangu magauni, kanga etc sioni kama limekaa sawa japo sisemi. Akija pia nakua sina uhuru na kwangu atapanga kila kitu tuleje, tuishije etc na sio mara moja nimesharudi toka kazini nikakuta sijawekewa chakula nyumbni kwangu mwenyewe mama akiwepo!!
Ikiwa nimepata la deal kazini na bi mkubwa akajua ataniambia nisipeleke pesa kwenye ujenzi bali niwape wao waweke kwenye biashara au watatue issue fulani( ikumbukwe hapo mimi huwapa pesa kila mwezi atleast 200k ama zaidi wakati mwingine mbali na kununua mahitaji, umeme etc) .Ikumbuke issue nyingine za kifamilia misiba, shuhuli etc nimebeba mie japo pia ninao ndugu wengine ila mimi ndio 70% wengine hizo zilizo baki.
Kiuhalisia mbali na kuwahudumia na mimi lazima maisha yaendelee tayari nina mji wangu, kuna wakati alininunia alipojua nimepata hela sijamuambia nikapeleka site. Bi mkubwa ameenda mbali zaidi akija hapa nyumbani hujenga mazoea na watu kiasi kwamba muda wote unakuta nyumba ina watu wengine hata siwafahamu na sio ndugu kitu ambacho sio sawa kwa usalama na privacy. ( Mfano wauza mboga, mara fundi cherehani mara watu wasaluni yani wote atataka awazoeeee kupitiliza)
Najitahidi sana wakija wazazi friji ipendeze na jikoni pawe vizuri wale wanachopenda ila atakula kisha atasema kabisa sijaridhika ikumbukwe yeye ndo ameamua kipikwe nini!! Hapo nitamuuliza nipike nini tena angalau afurahie.....daaaaah naumia kuna wakati mzee alikuja napika chakula saa ingine hagusi au anakula kidogo kisha anamwambia bi mkubwa sijala hapo ntapigiwa simu nisemweeee. Yani wakati mwingine najifungia ndani nalia tu.
Najua kwa baadhi sitaeleweka ila kuna pattern niiliisoma nikaumia kwamba kwa namna fulani huenda shida katika nyumba yangu ilisababishwa na wao kwasabau kwa bahati mbaya yule mwenzangu hakua vizuri sana kwa hiyo ni kama waliona hawanifaidi vya kutosha kwa hivyo kwa namna fulani hivi nilivyo kwao ni fursa.
Najua wengi mnaweza kunisema ila pia ni kitu nimekaa nacho zaidi ya miaka mili kinanisumbua. Naomba mnisaidie naishije ama nafanyaje?
Naomba mnisamehe kwa nitakao wakwaza au kuwaumiza na kuona sina shukrani kwa wazi ila kwa kwli najitahidi sana ila kuna namna fulani naumizwa pia.