Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"Badirika" ndio nini? Mbona huko kwingine umeandika vizuri?Ndio maana ulivunja ndoa yako ya kwanza. Una gubu,umimi. Badirika
Pia kila jambo litazame in positive way. Ata kama limekuchefua kiasi gani
Umeshafanya homework yako? Kesho shule....na ukajifunze kuandika.Kwa nafasi uliyo nayo n ngumu kufanya au kupata huo uhuru na control yko binafsi kwa sbb moja ty huna mwanaume ambae watu wakiwa wnkuja kwko wnjua kbx pale Kuna mwanaume.
Kwaio kitu Cha kfnya ulshkosea toka mwanzo inwezekana ulkua na kbur kwa jmaa kw sbb una mzd kipato au hkumpa uongoz mty wako pia mybe ulkua unwapa economic status ya mmeo wzaz wako wakaon n foolish kwko.
Kwaio xx Ili hiyo istokee tena tafta men olewa au hta kma kmrdia yule up to u alafu mpe uongozi km mwanaume hamia kwake hata kma umejenga uanze upya n ngumu mwanamk kusimama pkeake hata angemiliki millions of dollars[emoji120][emoji120]
Pole sana Dada yangu. Ikumbukwe hawa ni binadamu na wana tabia nzuri na mbaya. Sio kwa sababu ni wakubwa basi tabia mbaya waliacha.La hasha ziko pale pale.Najitahidi sana wakija wazazi friji ipendeze na jikoni pawe vizuri wale wanachopenda ila atakula kisha atasema kabisa sijaridhika ikumbukwe yeye ndo ameamua kipikwe nini!! Hapo nitamuuliza nipike nini tena angalau afurahie.....daaaaah naumia kuna wakati mzee alikuja napika chakula saa ingine hagusi au anakula kidogo kisha anamwambia bi mkubwa sijala hapo ntapigiwa simu nisemweeee. Yani wakati mwingine najifungia ndani nalia tu.
Hii hulka ( tabia ) imenimaliza sana kiasi kwamba hivi sasa natafuta Chuo cha Kufundisha Uchoyo, Roho Mbaya na Ukatili ili nikasome.Pole sana dada.
........Tatizo lako ni kuwa una huruma sana, una roho nzuri na unajali sana.
Kichwa chako kibovu sana.Ndio maana ulivunja ndoa yako ya kwanza. Una gubu,umimi. Badirika
Pia kila jambo litazame in positive way. Ata kama limekuchefua kiasi gani
1. Baadhi ya wamama wa kimeruMi nilimwambia mama nimefukuzwa kazi
Nikapunguza baadhi ya karaha, sijui Kwa nini baadhi ya wamama hufanya hivi hasa Kwa watoto wa kike
Hizi case nimekutana nazo nyingi, yupo tayari akusemee mbovu Kwa mwenzio kama anaona hana maslahi nae ili tu mfarakane ale pesa zako mwenyewe.[emoji20]
Maza ni Mmarangu au Mrombo?Nawashukuru sana wotee ambao mmechukua muda wenu kusoma na kunishauri , nawashukuru mno na hekima na busara zenu zimenipa mwanga kwa namna fulani. Toka jana moyo wangu umekua mzito mno kuna wakati najifungia ndani nalia ili nipate relief maana naogopa hata kusema kwa ndugu zangu.
Kuna wakati ndugu yangu alimtambulisha mchumba wake wakawa wanawasiliana matokeo yale mama siku nyingine akawa anaomba hela kwa huyu mchumba hilo jambo lilituumiza sana ila ndugu yangu alipata ujasiri wa kumwambia kua hapendi hiyo tabia.
Kwa wale mliosema mimi naonekana nina gubu ama jeuri kwa wanaume...naomba kuwaambia sipo hivyo nipo tofauti kabisa. Ni aina ya mwanamke ambae naweza kumpa mwanaume kadi yangu ya benki ili tu asijione mnyonge endapo mambo yake hayajakaa sawa, naweza kununua au kufanya kitu kwa hela yangu ila nikiulizwa nitasema mume ndio amefanya.... ni mtu wa kumfichia aibu mwenzangu( nisingependa kumuongelea sana kwasabau sio jambo la msingi kwa mada yangu hii)
Hayo niliyoeleza ni mambo machache kati ya mengi ambayo napitia .
Kuna wakati ilifika nikadhamiria kuacha kazi kwasababu kazi nzuri niliyoipata nikategemea itakua baraka kwangu na kwa familia yangu imegeuka huzuni. Sijawahi ku disclos nalipwa kiasi gani ila sijui ni kwa namna gani walifahamu kwa hiyo kuna wakati wanapoomba wanataka uwape walichotaja sio ulichonacho wewe. Anyways ni mambo mengi lakini nashukuru nimepata nguvu ya kushare haya machache na nyinyi na mkaweza kunishauri, nimepokea kwa mikono miwili na Mungu awabariki.
Kwa mlionifuata PM pia asanteni kwa kuguswa na jambo langu na kunishauri na shukuru pia kwa mnaoniombea. Mwisho wa yote nawatakia baraka, furaha na amani katika maisha yenu.
Suzieq
Mimi nacheka [emoji1787][emoji1787][emoji1787]tyu utadhani YEYE ndyo alikuwa mumeDah mkuu sioni sababu ya wewe kumkasirikia bidada namna hiyo?
Kwanza kabisa pole sana, binafsi nimekuelewa sana sana, ninachokiona chanzo kikubwa cha kuachana na mume wako kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na wazazi wako. Hujasema kisa cha kuachana ila inaonyesha wazazi wako wamechangia kwa asilimia kubwa, ukitaka kuelewa hili mrudiane na mume wako utaona hilo vizuri.Habari wanajamvi,
Kwa muda sasa kuna jambo limekua linaniumiza na nimekosa pa kuliongelea kwa uhuru ila naamini humu nitapata hekima na busara zangu.
Kama ilivyo ndoto ya kila mzazi anaesomesha mtoto ni ili mtoto ajisimamie na awe msaada kwa wazazi na nduguze baadae. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu nimesomeshwa vizuri na nimepata kazi nzuri ambau=yo imeniwezesha kufanya makubwa kwetu ikiwemo kumaliza ujenzi wa nyumba ya wazazi , kuwakatia bima na kuhakikisha wanapata matumizi yao ya kila mwezi kwa kifupi wanaishi maisha comfortable.
Wakati huo pia na mimi kama binti najiendeleza kimaisha maana tayari nina familia japo mwezangu palitokea mgogoro tukatengena.
Shida ipo hivi: Tangu nimeachana na mwenzangu ( kiukweli hakuna aneingia kwenye ndoa achane japo matatizo mengine hayavumiliki) ni kama wazazi wangu ni kitu walichokua wanakitaka maana wana access na mimi na wana nicontrol kama wanavyotaka jambo ambalo kwangu halijakaa sawa kuwaambia siwezi ila mimi pia kama mtu mwenye mji wangu kuna mambo ambayo naamini nimeyavuka nje ya control ya wazazi.
Kwa mfano bi mkubwa akija kwangu bila kuuliza ataingia kabatini na kuvaa nguo zangu magauni, kanga etc sioni kama limekaa sawa japo sisemi. Akija pia nakua sina uhuru na kwangu atapanga kila kitu tuleje, tuishije etc na sio mara moja nimesharudi toka kazini nikakuta sijawekewa chakula nyumbni kwangu mwenyewe mama akiwepo!!
Ikiwa nimepata la deal kazini na bi mkubwa akajua ataniambia nisipeleke pesa kwenye ujenzi bali niwape wao waweke kwenye biashara au watatue issue fulani( ikumbukwe hapo mimi huwapa pesa kila mwezi atleast 200k ama zaidi wakati mwingine mbali na kununua mahitaji, umeme etc) .Ikumbuke issue nyingine za kifamilia misiba, shuhuli etc nimebeba mie japo pia ninao ndugu wengine ila mimi ndio 70% wengine hizo zilizo baki.
Kiuhalisia mbali na kuwahudumia na mimi lazima maisha yaendelee tayari nina mji wangu, kuna wakati alininunia alipojua nimepata hela sijamuambia nikapeleka site. Bi mkubwa ameenda mbali zaidi akija hapa nyumbani hujenga mazoea na watu kiasi kwamba muda wote unakuta nyumba ina watu wengine hata siwafahamu na sio ndugu kitu ambacho sio sawa kwa usalama na privacy. ( Mfano wauza mboga, mara fundi cherehani mara watu wasaluni yani wote atataka awazoeeee kupitiliza)
Najitahidi sana wakija wazazi friji ipendeze na jikoni pawe vizuri wale wanachopenda ila atakula kisha atasema kabisa sijaridhika ikumbukwe yeye ndo ameamua kipikwe nini!! Hapo nitamuuliza nipike nini tena angalau afurahie.....daaaaah naumia kuna wakati mzee alikuja napika chakula saa ingine hagusi au anakula kidogo kisha anamwambia bi mkubwa sijala hapo ntapigiwa simu nisemweeee. Yani wakati mwingine najifungia ndani nalia tu.
Najua kwa baadhi sitaeleweka ila kuna pattern niiliisoma nikaumia kwamba kwa namna fulani huenda shida katika nyumba yangu ilisababishwa na wao kwasabau kwa bahati mbaya yule mwenzangu hakua vizuri sana kwa hiyo ni kama waliona hawanifaidi vya kutosha kwa hivyo kwa namna fulani hivi nilivyo kwao ni fursa.
Najua wengi mnaweza kunisema ila pia ni kitu nimekaa nacho zaidi ya miaka mili kinanisumbua. Naomba mnisaidie naishije ama nafanyaje?
Naomba mnisamehe kwa nitakao wakwaza au kuwaumiza na kuona sina shukrani kwa wazi ila kwa kwli najitahidi sana ila kuna namna fulani naumizwa pia.
Hakika
Ameharibu hapo alipoandika sasa eti (xx) yani sipendii. Japo ana pointUnaonekana ni high IQ ila hujui kuandika. I like the content tho.