Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uzi ufungweKwa nafasi uliyo nayo n ngumu kufanya au kupata huo uhuru na control yko binafsi kwa sbb moja ty huna mwanaume ambae watu wakiwa wnkuja kwko wnjua kbx pale Kuna mwanaume.
Kwaio kitu Cha kfnya ulshkosea toka mwanzo inwezekana ulkua na kbur kwa jmaa kw sbb una mzd kipato au hkumpa uongoz mty wako pia mybe ulkua unwapa economic status ya mmeo wzaz wako wakaon n foolish kwko.
Kwaio xx Ili hiyo istokee tena tafta men olewa au hta kma kmrdia yule up to u alafu mpe uongozi km mwanaume hamia kwake hata kma umejenga uanze upya n ngumu mwanamk kusimama pkeake hata angemiliki millions of dollars[emoji120][emoji120]
Unawajua waha wewe?labda ahamie mbinguniSijui kwa nini nimekuonea huruma sana niliposoma andiko hili. Inaonekana wazazi wako ni aina ya wazazi ambao ni controlling sana, they like and enjoy to take charge na ku control maisha ya watoto wao. Inawezekana pia wao wamechangia kwa kiasi fulani ndoa yako kupata matatizo na kuvunjika. Inawezekana pia ndio sababu hata ndugu zako uliozaliwa nao wamejiweka mbali nao kwa sababu wanajua kuwa wazazi wao ni watu wa aina gani, hivyo wamechagua kuwaweka mbali wabaki tu kama wazazi, kuwahudumia hapa na pale na kuwatembelea hapa na pale na kuwapigia simu, na sio kuwaweka karibu kiundani kama unavyofanya wewe.
Inaonekana wewe either umechelewa kugundua hilo, au unalijua ila una huruma sana hivyo unashindwa kufanya lolote, na wao wanajua kabisa hiyo weakness yako na wanatembea nayo hiyo hiyo (ndio tabia ya watu ambao ni controlling).
Ushauri:
Je, unaweza kuhama huo mkoa uliopo sasa ambao pia wazazi wako wapo? Kama ni wajiriwa, unaweza kuomba uhamisho kazini kwako ukahamia mkoa mwingine? Kama ndio, fanya hivyo, anza process za uhamisho uhame mkoa kwa kisingizio chochote kile, na ukikamilisha uwaage uwaambia umepata uhamisho inabidi uhame, itakua ni hatua muhimu sana kwako katika safari ya kuondoa hiyo control. Kama ofisi yenu suala la kuhama mkoa haliwezekani, basi pia angalia uwezekano wa kutafuta kazi ofisi nyingine ambayo itakua nje ya mkoa ulioko sasa na wazazi wako.
Tafuta kidume wewe alafu hamia kwa kidume. Hawawezi kukusumbua tenaHabari wanajamvi,
Kwa muda sasa kuna jambo limekua linaniumiza na nimekosa pa kuliongelea kwa uhuru ila naamini humu nitapata hekima na busara zangu.
Kama ilivyo ndoto ya kila mzazi anaesomesha mtoto ni ili mtoto ajisimamie na awe msaada kwa wazazi na nduguze baadae. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu nimesomeshwa vizuri na nimepata kazi nzuri ambau=yo imeniwezesha kufanya makubwa kwetu ikiwemo kumaliza ujenzi wa nyumba ya wazazi , kuwakatia bima na kuhakikisha wanapata matumizi yao ya kila mwezi kwa kifupi wanaishi maisha comfortable.
Wakati huo pia na mimi kama binti najiendeleza kimaisha maana tayari nina familia japo mwezangu palitokea mgogoro tukatengena.
Shida ipo hivi: Tangu nimeachana na mwenzangu ( kiukweli hakuna aneingia kwenye ndoa achane japo matatizo mengine hayavumiliki) ni kama wazazi wangu ni kitu walichokua wanakitaka maana wana access na mimi na wana nicontrol kama wanavyotaka jambo ambalo kwangu halijakaa sawa kuwaambia siwezi ila mimi pia kama mtu mwenye mji wangu kuna mambo ambayo naamini nimeyavuka nje ya control ya wazazi.
Kwa mfano bi mkubwa akija kwangu bila kuuliza ataingia kabatini na kuvaa nguo zangu magauni, kanga etc sioni kama limekaa sawa japo sisemi. Akija pia nakua sina uhuru na kwangu atapanga kila kitu tuleje, tuishije etc na sio mara moja nimesharudi toka kazini nikakuta sijawekewa chakula nyumbni kwangu mwenyewe mama akiwepo!!
Ikiwa nimepata la deal kazini na bi mkubwa akajua ataniambia nisipeleke pesa kwenye ujenzi bali niwape wao waweke kwenye biashara au watatue issue fulani( ikumbukwe hapo mimi huwapa pesa kila mwezi atleast 200k ama zaidi wakati mwingine mbali na kununua mahitaji, umeme etc) .Ikumbuke issue nyingine za kifamilia misiba, shuhuli etc nimebeba mie japo pia ninao ndugu wengine ila mimi ndio 70% wengine hizo zilizo baki.
Kiuhalisia mbali na kuwahudumia na mimi lazima maisha yaendelee tayari nina mji wangu, kuna wakati alininunia alipojua nimepata hela sijamuambia nikapeleka site. Bi mkubwa ameenda mbali zaidi akija hapa nyumbani hujenga mazoea na watu kiasi kwamba muda wote unakuta nyumba ina watu wengine hata siwafahamu na sio ndugu kitu ambacho sio sawa kwa usalama na privacy. ( Mfano wauza mboga, mara fundi cherehani mara watu wasaluni yani wote atataka awazoeeee kupitiliza)
Najitahidi sana wakija wazazi friji ipendeze na jikoni pawe vizuri wale wanachopenda ila atakula kisha atasema kabisa sijaridhika ikumbukwe yeye ndo ameamua kipikwe nini!! Hapo nitamuuliza nipike nini tena angalau afurahie.....daaaaah naumia kuna wakati mzee alikuja napika chakula saa ingine hagusi au anakula kidogo kisha anamwambia bi mkubwa sijala hapo ntapigiwa simu nisemweeee. Yani wakati mwingine najifungia ndani nalia tu.
Najua kwa baadhi sitaeleweka ila kuna pattern niiliisoma nikaumia kwamba kwa namna fulani huenda shida katika nyumba yangu ilisababishwa na wao kwasabau kwa bahati mbaya yule mwenzangu hakua vizuri sana kwa hiyo ni kama waliona hawanifaidi vya kutosha kwa hivyo kwa namna fulani hivi nilivyo kwao ni fursa.
Najua wengi mnaweza kunisema ila pia ni kitu nimekaa nacho zaidi ya miaka mili kinanisumbua. Naomba mnisaidie naishije ama nafanyaje?
Naomba mnisamehe kwa nitakao wakwaza au kuwaumiza na kuona sina shukrani kwa wazi ila kwa kwli najitahidi sana ila kuna namna fulani naumizwa pia.
Tupo wengi mkuuAsee, kumbe tupo wengi,
Familia za kiswahili sijui zikoje, Wazazi wanakusomesha, wanakupa kiwanja pale pale nyumbani kwao, Wanaanza kukulazimisha ujenge ilihali huna kipato, Unaamua kuondoka kwenda mbali kupambana maana wao walipokuwa na uwezo hawakukusapoti, Ukiwashirikisha kuwa kuna kibarua unataka ukajaribu babati yako wanakuvunja Moyo, tena wanawaeleza watu baki ambao hata siyo ndugu kuwa "anahangaika tu"
"Anajifanya mjanja, tumemsomesha analeta dharau, hatofika popote!.."
Sasa unajiuliza mimi ni mtoto wa kiume, naamua kwenda kupambana na maisha mbali huko, nyuma unasikia kwa watu wazazi wakikusema vibaya,.....
Kwa simulizi lake inaonyesha huyo bidada anaonekana ni yale majanamke yenye gubu na michoyo
Naunga mkono hoja.Una uhakika wazazi wako sio wanga au washirikina?
Najua ni ngumu kuamini lakini wazazi wa dizaini hiyo behind the scene huwa ni washirikina na wanamaagano yao either mtoto fulani au wote wasiwe mbali na himaya yao. Pambana it seems unakitu kikubwa ndani yako ambacho katika ulimwengu wa giza wanakihofiaAsee, kumbe tupo wengi,
Familia za kiswahili sijui zikoje, Wazazi wanakusomesha, wanakupa kiwanja pale pale nyumbani kwao, Wanaanza kukulazimisha ujenge ilihali huna kipato, Unaamua kuondoka kwenda mbali kupambana maana wao walipokuwa na uwezo hawakukusapoti, Ukiwashirikisha kuwa kuna kibarua unataka ukajaribu babati yako wanakuvunja Moyo, tena wanawaeleza watu baki ambao hata siyo ndugu kuwa "anahangaika tu"
"Anajifanya mjanja, tumemsomesha analeta dharau, hatofika popote!.."
Sasa unajiuliza mimi ni mtoto wa kiume, naamua kwenda kupambana na maisha mbali huko, nyuma unasikia kwa watu wazazi wakikusema vibaya,.....
Kwa issue hii kosa ni lako mwenyewe. Banisha kimya kabisa (kwa vile umeshajua hiyo ndiyo tabia ya mzazi wako).Ikiwa nimepata la deal kazini na bi mkubwa akajua ataniambia nisipeleke pesa kwenye ujenzi bali niwape wao waweke kwenye biashara au watatue issue fulani