Wazazi wangu wakija kwangu wanafanya maamuzi ya nini kifanyike!

Ndio maana ulivunja ndoa yako ya kwanza. Una gubu,umimi. Badirika

Pia kila jambo litazame in positive way. Ata kama limekuchefua kiasi gani
"Badirika" ndio nini? Mbona huko kwingine umeandika vizuri?

Ndio maana hakuna la maana ulilochangia humu.
 
Umeshafanya homework yako? Kesho shule....na ukajifunze kuandika.
 
Dada... sio lazma mwanaume. Kaa mbali na wanaokukera, wasaidie unapoweza kuwasaidia, waheshimu. Lakini kaa mbali, punguza mazoea. Kwa sababu, wana ubinafsi, usitegemee watakuelewa ukiwaambia. Sana sana watakuumiza zaidi pale utakapojaribu kuzungumza nao.

Utasikia kauli kama, "mimi ni mama yako", sijui oooh! "Nimekulea tumboni"....mara "mimi ndio nimekusomesha"
 
Pole sana Dada yangu. Ikumbukwe hawa ni binadamu na wana tabia nzuri na mbaya. Sio kwa sababu ni wakubwa basi tabia mbaya waliacha.La hasha ziko pale pale.

Kama unaweza hamia sehemu nyingine ikiwa unapoishi sio mjengo wako.

Umesoma kwa bidii na kufanya kazi kwa bidii naelewa mafanikio yako ni jitihada zako 80%.

Ni wakati na wewe unyoi maisha. Ulete Boy wako unayempenda mchakatane kisawa sawa kwa uhuru.

Hao wazee ni wazazi wako na u awapenda sana ila wasikupotezee furaha yako.

Jambo Lingine ikiwa wewe ni mtu wa Dini kama mimi Rastaman basi jaribu kuliombea hilo pepo liwatoke.

Naona kama wanaendeshwa na roho za vyura.
 
Pambana wazazi wote wa kibongo ndo wapo hvyo ukiona kwako kwaungua jua kwa mwenzio kwateketea
 
Pole sana dada.
........Tatizo lako ni kuwa una huruma sana, una roho nzuri na unajali sana.
Hii hulka ( tabia ) imenimaliza sana kiasi kwamba hivi sasa natafuta Chuo cha Kufundisha Uchoyo, Roho Mbaya na Ukatili ili nikasome.

99% ya Watu ambao nimekuwa nikiwapenda, nikiwaonea Huruma, nikijitoa kwa hali na Mali Kwao na hata Kuwasaidia iwe kwa Fikra ( Mawazo ) na hata Pesa kama nikiwa nayo ndiyo Wanaoongoza Kuniumiza, Kunichafua, Kunichukia na zaidi Kunifitinisha na Watu.

Kuna muda huwa namlaumu sana Mwenyezi Mungu kuwa ni kwanini Kaniumba kuwa mwenye Huruma, Utu, Upendo, Uaminifu na Ukweli halafu baadae hizi tabia zinageuka kuwa Fimbo ya Kunichapia na Kuniangamizia Kimaisha?
 
Ndio maana ulivunja ndoa yako ya kwanza. Una gubu,umimi. Badirika

Pia kila jambo litazame in positive way. Ata kama limekuchefua kiasi gani
Kichwa chako kibovu sana.
Huoni mzazi alivyo vululu vululu?
Mzazi hapaswi kukosa mipaka kiasi hiki.
Huyo mama ni mharibifu bila shaka ni Mmarangu au mrombo
 
1. Baadhi ya wamama wa kimeru
2. Wamarangu ni 90%
3. Warombo 40%

Wazazi hao niliowataja wanashida sana
 
Maza ni Mmarangu au Mrombo?
Huwa hilo tatizo lipo sana
 
Dada ukiendekeza ndugu, wazazi na kujibebesha mizigo utakufa masikini.
Wazee wako local kinoma Mana wanademand more ht ufanyeje hao piga Ban. Weka mipaka kwa kila Jambo / eneo Kuanzia pesa na mengineyo.
Shida Ni wewe kujikabidhi kwao, mwili wako akili yako mikononi mwao.
#Unapowavumilia unawafundisha namna ya kukutendea
 
Kwanza kabisa pole sana, binafsi nimekuelewa sana sana, ninachokiona chanzo kikubwa cha kuachana na mume wako kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na wazazi wako. Hujasema kisa cha kuachana ila inaonyesha wazazi wako wamechangia kwa asilimia kubwa, ukitaka kuelewa hili mrudiane na mume wako utaona hilo vizuri.
Tabia za wazazi kama hawa nimewahi kuona kwa baadhi ya watu, wapo wazazi wana shida hii, sijajua ni nini ila ni tabia zinazokera sana.
Shida ipo kwao, wanashindwa kuelewa mipaka yao, wanafikiri wanaweza kufanya wanachojua wao. Kinachosumbua zaidi baba na mama ni kitu kimoja, angekuwa mama peke yake ungeweza kumsaidia kwa urahisi.
Wazo langu watumie watu wanaoaminika na wazazi wako waeleze kisa na mkasa, kisha wajue namna ya kuongea nao pasipo kujua uhusika wako.
Ukishindwa kuwapata hao watu watumie viongozi wako wa dini, wanaweza kuandaa semina ya wazazi kuwa na mipaka kwa watoto wao.
Usipofanya hivyo utapata mwanaume mwingine utaingia kwenye shida ile ile ya kuachana. Wanaume wachache watavumilia matendo ya wazazi wako wengine hawawezi.
Chumba chako kiwe na mipaka, funga chumba chako, wazazi waishie kwenye vyumba vyao ulivyowapa. Suala la mzazi kuingia chumbani kwako kuchukua nguo anayotaka sio heshima.
Kwahiyo tumia hao watu kutokana na mazingira yako, unaweza kumaliza changamoto yako.
 
Moja kati ya vingi ninavyo mshukuru mungu ni kunijaalia kuzaliwa na huyu mama yangu, aisee nashukuru mnoo, sababu naona wengine wanavyoteseka na wazazi wao, mzazj wa kiume alizikwa kitambo, kupitia stori nae hakuwa miyeyusho.

Kupata wazazi vivuruge ni mtihani watakuvuruga kweli kweli
Nakosa hata la kukushauri ukizingatia pepo zipo kwenye nyayo zao hatuna budi kuwanyenyekea tu, ili mradi tusiwatii katika mambo yasiyompendeza.

Jaribu kutafuta ndugu zako(wakubwa) ambao mnaivaa saana, uwaeleze jambo hili huenda wakawa na mawili matatu sababu walianza kuliona jua kabla yako, huwemda wanawajua wazazi vizuri zaidi yako.
 
Tatizo la wanawake wa Sasa wanataka kututawala kisa Hela hiyo SIYO ndoa.Mwanamke LAZIMA atawaliwe na mwanaume na UKITAKA ndoa idumu miaka mingi muoneshe mume wako ya KWAMBA unamsikiliza anachosema hapo UTAAMINI miujiza ya kuwa msikivu kwa mumewe. Ila unapojidai kuwa HUTAKI kumsikiliza mwanaume kisa vijimshahara vyako hapo inakuwa umebugi. Unateseka kwa sababu hukutaka kuonesha utiifu kwa mumewe. Sasa hivi UNATAMANI awepo mume lakini wazazi wako ndyo wamekuwa kama waume zako Sasa UTAPELEKESHWA SANA. Uache pia kuwa na gubu .Siku zote ukilikimbia zuri Baya huja umemuona mume wako hafai ngoja WAZAZI wakuonyeshe kazi watazidi kukukomoa mpaka UTAKOMOLEKA.
 
Upo mpole sana utapelekeshwa mpaka
Chumbani kwako si ufunge mlango ondoka na funguo,mim kwangu haji mtu hovyo na yeyote aje na adabu kubwa awe yeyote ,kwetu wote wananiogopa wanajua dakika moja au mbili nishavurugwa
 
Pole sana mdada wazazi wako wanakuonea wivu sijui? Maana huo sio upendo wa mzazi kwa mtoto hata kidogo,they want to take full control over you..which is not right.
Amua kitu waza kitu kustopisha all these nonsense.
 
Fanya kuomba likizo kazini. Rudi nyumbani kwa wazazi, waeleze kuwa Kuna kitu kibaya kimetokea kazini. Umesimamishwa au kufukuzwa kazi. Waambie Ni issue nyeti hawapaswi kufuatilia au kujihusisha kwa namna yoyote. Waambie ata akaunti zako umefungiwa. Kwa maana hauna chochote kwa mda huo.
Kama wapo kwa Nia nzuri na wewe utaona kwa kipindi hicho. Na ndo mda wa kujipanga na tabia tofauti na awali. Acha kuzungumzia masuala ya kazini. Ongea kwa kifupi lakini kwa kumaanisha.
Katika maisha, siku hizi watu wa karibu ndo wamekuwa chanzo katika migogoro mingi hasa kwa watumishi. Tena ukiwa ulisomeshwa imekuwa fimbo mbaya kwa wazazi na ndugu. HAWARIDHIKI
Jitaidi kuficha kipato chako. Jishushe, tafuta mme uheshimike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…