Wazazi wawatishia watoto kifo endapo watafaulu mitihani ya Darasa la Saba

Wazazi wawatishia watoto kifo endapo watafaulu mitihani ya Darasa la Saba

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baadhi ya wazazi wilayani Makete mkoani Njombe wamedaiwa kuwatisha watoto wao wanaohitimu elimu ya msingi kufanya vibaya kwenye mitihani kwa madai kuwa wakifaulu wao watafariki dunia.

Ameeleza hayo Ofisa Mtendaji wa Kata ya Lupila , Tumwanukye Ngakonda kwamba baada ya wanafunzi hao kuhojiwa kutokana na mabadiliko yao ya kitaaluma kuelekea mitihani yao ya mwisho walidai kushinikizwa kufanya vibaya kwa kuhofia kuwapoteza wazazi wao kwa kigezo kwamba wakifaulu watashindwa kuwasomesha kutokana na hali mbaya ya kiuchumi.

"Kwa sababu ya changamoto hiyo Wilaya ya Makete tumejiwekea mikakati ya kusimamia ipasavyo elimu kwa kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu anaripoti na kuendelea na masomo ya Sekondari," amesema Ngakonda.

Ameongeza kuwa baada ya kugundua tatizo hilo wamechukua hatua ikiwa ni pamoja na utoaji elimu kwa wanafunzi kutokubali kufeli na katika elimu hiyo wamekutana na shuhuda mbalimbali ikiwemo wazazi kuwaambia kuwa endapo watafaulu hawatokuwa watoto wao.

Chanzo: Nipashe
 
Wanazuia watt wasisome miaka ijayo wataanza kulalamika mbona kabila fulan ni wao tu kila sehemu
 
Haya mambo ndio ninayokumbana nayo huku niliko.

Kuna jamii za Ajabu sana.

Kila siku wanaleta vikesi vya ajabuajabu ilimradi tu watoto wao wasipate elimu bado najiuliza malengo yao ni nini.
Huku niliko inafika Hatua mzazi anamwambia mtoto "nenda kaandike madudu kwenye karatasi ya kujibia" kisa hawezi mbilinge za viongozi kumlazimisha apeleke mtoto shule.

Watoto wanafeli sana viongozi wakubwa Wakija wanatuona wakina sie hatufanyi kazi kumbe changamoto ipo kwa wazazi wa hawa watoto hawataki watoto wao wapate elimu.
 
Kuna Njombe✅ Tabora✅ Iringa✅ Katavi✅ Geita✅ Hii Mikoa inahitaji uangalizi maalumu dhidi ya ustawi na elimu kwa watoto.
 
Baadhi ya wazazi wilayani Makete mkoani Njombe wamedaiwa kuwatisha watoto wao wanaohitimu elimu ya msingi kufanya vibaya kwenye mitihani kwa madai kuwa wakifaulu wao watafariki dunia...
Ndo mnawafananisha hizi jamii na watu wa kaskazin huwaga mnakosea sana
 
Back
Top Bottom